Naomba Kufahamu juu ya kilimo cha Machungwa katika mikoa ya Pwani, Tanga au Morogoro

evance hubert

Member
Oct 14, 2012
36
20
Poleni na mihangaiko ya kila siku.

Naomba kama kuna mtu anauelewa juu ya kilimo cha matunda machungwa kwa mikoa ya Tanga, Kibaha na morogoro (hata sehemu moja).

Anisaidie kunijuza juu ya ukulima huu kuanzia kwenye:
1. Aina bora ya machungwa yanayokubali sana maeneo hayo.

2. Gharama za upatkanaji wa mashamba.

3. Utunzaji wa miti ya machungwa kabla ya kuzaa mpka wakati wa kuvuna.

4. Gharama za vibarua na ulinzi wa shamba.

5. Changamoto zinazoweza kuvamia kilimo cha machungwa.

6. Upatikanaji wa masoko.
1498201575285.jpg
 
Attachments

  • 1498201564755.jpg
    1498201564755.jpg
    10.5 KB · Views: 304
Mimi nipo Muheza Tanga na mkulima mdogo wa machungwa. Mbegu zipo nyingi ila zinazotumika kwa sasa ni msasa na valencia. Tofauti yake ni kwamba msasa unakomaa mapema na unakulazimisha kuuza mapema mbegu hii hulimwa na wakulima wenye kipato cha chini ambao hawawezi kuvumilia njaa. Bei yake shambani huanzia Tsh 20 mpaka Tsh 50. Valencia ndio mbegu inayopendwa na wakulima wengi kwani inaweza kukaa muda mrefu shambani. Pia chungwa linaweza kuuzwa mpaka Tsh 100 au zaidi ya hapo.

UNAPATAJE FAIDA?
Ukiwa na shamba ekari moja inaweza kuingia michungwa 80 ambao utakapokomaa vizuri unaweza kuzaa hata machungwa 1000.
Wekea umezaa machungwa 800 zidisha mara michumgwa 80 unapata 64000 zidisha mara 100 kama ni valencia unapata Tsh 6400000/=

GARAMA ZA KUHUDUMIA
Shamba la michungwa litahitaji huduma za ukaribu katika miaka mitatu ya mwanzo baada ya hapo itakuwa ni kulimia tu na kufanya usafi Mwingine kama prunning ambazo hazifiki hata laki tano kwa mwaka. Kumbuka hapo nimepiga hesabu ya ekari moja tu.

CHANGAMO

Machungwa hasa valencia uwezekano wa kushambuliwa na magonjwa ni mdogo sana changamoto kubwa ni wezi na machungwa kuanguka kama utakuwa unasubiri bei kubwa.

SOKO
Zamani soko la machungwa lilikuwa ni changamoto kubwa kwani mikoa iliyokuwa inapokea machungwa ilikuwa ni Dar na Arusha tu ila kwa sasa soko ni kubwa mpaka Nairobi na mombasa kwa mfano inafikia kipindi ukiwa na machungwa shambani wateja wanakusumbua wewe.

UPATIKANAJI WA MASHAMBA
Mashamba yanapatikana ila kwa tabu na bei yake iko juu kidogo.

KUHUSU WAFANYAKAZI
Wafanyakazi wanapatikana pia unaweza kujenga nyumba ya kawaida shambani na Mtu akakaa huko huko kwa Ulinzi.
Nafikiri nimekujibu japo kidogo.
Pia nimepiga hesabu ya ekari moja na pia mchungwa unaweza kuzaa mara mbili kwa mwaka.
 
Mi na mashamba Vigwaza pwani ni kichanga tifutifu ni ardhi nyeusi

Je inafaa wakuu mnishauri
 
Vigwaza machungwa yanakubali ila changamoto ni kwamba hayawezi kukaa kwenye mti mda mrefu hivyo utakuwa unauza kwa bei ya hasara sio kama muheza
 
Fika muheza ndani ndani kuna kijiji kinaitwa mashewa mashamba ni bei rahisi tofauti na yaliyopo barabara kuu ya Tanga _segera
 
Mimi nipo Muheza Tanga na mkulima mdogo wa machungwa. Mbegu zipo nyingi ila zinazotumika kwa sasa ni msasa na valencia. Tofauti yake ni kwamba msasa unakomaa mapema na unakulazimisha kuuza mapema mbegu hii hulimwa na wakulima wenye kipato cha chini ambao hawawezi kuvumilia njaa. Bei yake shambani huanzia Tsh 20 mpaka Tsh 50. Valencia ndio mbegu inayopendwa na wakulima wengi kwani inaweza kukaa muda mrefu shambani. Pia chungwa linaweza kuuzwa mpaka Tsh 100 au zaidi ya hapo.

UNAPATAJE FAIDA?
Ukiwa na shamba ekari moja inaweza kuingia michungwa 80 ambao utakapokomaa vizuri unaweza kuzaa hata machungwa 1000.
Wekea umezaa machungwa 800 zidisha mara michumgwa 80 unapata 64000 zidisha mara 100 kama ni valencia unapata Tsh 6400000/=

GARAMA ZA KUHUDUMIA
Shamba la michungwa litahitaji huduma za ukaribu katika miaka mitatu ya mwanzo baada ya hapo itakuwa ni kulimia tu na kufanya usafi Mwingine kama prunning ambazo hazifiki hata laki tano kwa mwaka. Kumbuka hapo nimepiga hesabu ya ekari moja tu.

CHANGAMO

Machungwa hasa valencia uwezekano wa kushambuliwa na magonjwa ni mdogo sana changamoto kubwa ni wezi na machungwa kuanguka kama utakuwa unasubiri bei kubwa.

SOKO
Zamani soko la machungwa lilikuwa ni changamoto kubwa kwani mikoa iliyokuwa inapokea machungwa ilikuwa ni Dar na Arusha tu ila kwa sasa soko ni kubwa mpaka Nairobi na mombasa kwa mfano inafikia kipindi ukiwa na machungwa shambani wateja wanakusumbua wewe.

UPATIKANAJI WA MASHAMBA
Mashamba yanapatikana ila kwa tabu na bei yake iko juu kidogo.

KUHUSU WAFANYAKAZI
Wafanyakazi wanapatikana pia unaweza kujenga nyumba ya kawaida shambani na Mtu akakaa huko huko kwa Ulinzi.
Nafikiri nimekujibu japo kidogo.
Pia nimepiga hesabu ya ekari moja na pia mchungwa unaweza kuzaa mara mbili kwa mwaka.
Hi! Msimu gani unafaa kupanda? Miche /mbegu ni tsh ngapi kwa ekari moja
 
Asante kwa kutujuza.

Kwenye picha naona machungwa na machenza yaliyo mazuri sana. Jee unaweza kutupa elimu kama hiyo kuhusu machenza?
 
Fika muheza ndani ndani kuna kijiji kinaitwa mashewa mashamba ni bei rahisi tofauti na yaliyopo barabara kuu ya Tanga _segera
nawezapata connection ya wauza mashamaba huko Mheza bei zake, haina ya umiliki wa mashamba huko panafikika muda wote????
 
Mkuu kule Ni milimani lakini panafikika vizur tu
Unataka uanze kulitumia lini mkuu
Mwezi wa pili nina safari ya Tanga, Mailkumi, Mheza kicheba, na Pangani wish nikifika kicheba nipate connection ya kufika huko na kujua taratibu mazingara ya uwekezaji na kuona mawili matatu, but mail kumi ninashamba pale nilinunua mwaka jana lina michungwa sema ni ya Asili.
 
Mkuu kama una shamba maili kumi kwanini usibadilishe ukapanda mbegu ya kisiasa?

OK tutawSiliana mimi wiki hii nataka nipande kule Amani kwenye mshamba ya Chai nitateremka February nafkiri Kuna kipande nmepata kikiwa kikubwa nitakupa pia
 
Mimi nipo Muheza Tanga na mkulima mdogo wa machungwa. Mbegu zipo nyingi ila zinazotumika kwa sasa ni msasa na valencia. Tofauti yake ni kwamba msasa unakomaa mapema na unakulazimisha kuuza mapema mbegu hii hulimwa na wakulima wenye kipato cha chini ambao hawawezi kuvumilia njaa. Bei yake shambani huanzia Tsh 20 mpaka Tsh 50. Valencia ndio mbegu inayopendwa na wakulima wengi kwani inaweza kukaa muda mrefu shambani. Pia chungwa linaweza kuuzwa mpaka Tsh 100 au zaidi ya hapo.

UNAPATAJE FAIDA?
Ukiwa na shamba ekari moja inaweza kuingia michungwa 80 ambao utakapokomaa vizuri unaweza kuzaa hata machungwa 1000.
Wekea umezaa machungwa 800 zidisha mara michumgwa 80 unapata 64000 zidisha mara 100 kama ni valencia unapata Tsh 6400000/=

GARAMA ZA KUHUDUMIA
Shamba la michungwa litahitaji huduma za ukaribu katika miaka mitatu ya mwanzo baada ya hapo itakuwa ni kulimia tu na kufanya usafi Mwingine kama prunning ambazo hazifiki hata laki tano kwa mwaka. Kumbuka hapo nimepiga hesabu ya ekari moja tu.

CHANGAMO

Machungwa hasa valencia uwezekano wa kushambuliwa na magonjwa ni mdogo sana changamoto kubwa ni wezi na machungwa kuanguka kama utakuwa unasubiri bei kubwa.

SOKO
Zamani soko la machungwa lilikuwa ni changamoto kubwa kwani mikoa iliyokuwa inapokea machungwa ilikuwa ni Dar na Arusha tu ila kwa sasa soko ni kubwa mpaka Nairobi na mombasa kwa mfano inafikia kipindi ukiwa na machungwa shambani wateja wanakusumbua wewe.

UPATIKANAJI WA MASHAMBA
Mashamba yanapatikana ila kwa tabu na bei yake iko juu kidogo.

KUHUSU WAFANYAKAZI
Wafanyakazi wanapatikana pia unaweza kujenga nyumba ya kawaida shambani na Mtu akakaa huko huko kwa Ulinzi.
Nafikiri nimekujibu japo kidogo.
Pia nimepiga hesabu ya ekari moja na pia mchungwa unaweza kuzaa mara mbili kwa mwaka.
Asante kwa darasa
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom