Naomba kufahamu IGP mpya ni mtu wa wapi na anasifa gani tofauti na wengine?

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Salamu wakuu.

Naomba kufahamu sifa za IGP mpya ni nani na kafanya vitu gani vya utofauti ambavyo ni tofauti na wengine hadi kuchaguliwa kuwa IGP.

Tafadhari
 
Ni mtu au binadamu kama wengine ,vitu vyake ndio unaviona hivyo ameingia kwa kuongeza ajira katika jeshi la polisi.

Pia inawezekana Mheshimiwa Kikwete anawalipa watu wake waliomsaidia kuingia Ikulu ukianzia na ubadilishaji wa Mawaziri huenda anatimiza ahadi za kumpa kila mtu nafasi ya ulaji maana ni wao kwa wao. waarabu wa pemba wanajuana kwa vilemba.
 
Jamaa Mnyaturu mengine watatujuza wengine. Mimi ning'eandamana endapo Thobias Andengenye ang'eteuliwa kushika mikoba hii.
 
Anatoka mkoa mkoa mmoja na Mwigulu Mchemba yaani mkoa wa Singida, ila wanatofautiana Mwigulu ni Mnyiramba wa wilaya ya Iramba na huyu mkuu wa polisi ni Mnyaturu kikabila.
 
Salamu wakuu.

Naomba kufahamu sifa za IGP mpya ni nani na kafanya vitu gani vya utofauti ambavyo ni tofauti na wengine hadi kuchaguliwa kuwa IGP.

Tafadhari

kwao Singida Kabila Mnyiramba husomi magazeti ndugu? halafu kuna umuhimu gani wa kujua kabila na atokako? ili mradi ni mtanzania tunasonga mbele sie sio wakenya, waganda wala wanyarwanda wenye kutanguliza kabila
 
Huyu si Mnyiramba bali ni Mnyaturu kama Lissu
 
Baba yake alikuwa na wake sita. Kila mwanamke alihangaikia kusomesha watoto wake. Alivyofaulu darasa la saba kwenda sekondari, alipewa ng'ombe akauze mnadani, wahuni wakamkomba hela zote,alirudi nyumbani kwa kilio.Jamaa ana hasira na majambazi toka utotoni,acha tu. Mama alimsomesha kwa biashara ya pombe za kienyeji(gongo?).
 
kwao Singida Kabila Mnyiramba husomi magazeti ndugu? halafu kuna umuhimu gani wa kujua kabila na atokako? ili mradi ni mtanzania tunasonga mbele sie sio wakenya, waganda wala wanyarwanda wenye kutanguliza kabila

usikariri wewe si kila anaetoka singida ni mnyiramba
 
Baba yake alikuwa na wake sita. Kila mwanamke alihangaikia kusomesha watoto wake. Alivyofaulu darasa la saba kwenda sekondari, alipewa ng'ombe akauze mnadani, wahuni wakamkomba hela zote,alirudi nyumbani kwa kilio.Jamaa ana hasira na majambazi toka utotoni,acha tu. Mama alimsomesha kwa biashara ya pombe za kienyeji(gongo?).

Hapo kwenye gongo pana ukweli??? Kama ni hivyo hoja ya Dr. Slaa kuna haja ya kuiangalia upya badala ya kuibeza.
 
Back
Top Bottom