Naomba kufahamu bei ya kilo moja ya vanila inauzwa sh. ngapi?

ngalanga

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
1,782
1,882
Umofya kwenu wadau humu ndani.

Twende kwenye maada ! Ni hivi wakuu mimi nipo huku Njombe na ningependa niwashirikishe juu ya uvumi wa bei ya zao tajwa hapo juu,kuna kikundi cha watu huku kimejitanabaisha kuwa ni taasisi(jina kapuni)kinapita kikiwahamasisha wakulima kulima zao la vanila wakidai kuwa bei imepanda yaani kilo moja ni shillingi million moja na nusu,nimepigwa butwaa !

Ukitaka mbegu wanakuuzia wao wenyewe na hiyo miche yake ni ghali sana(mche mmoja wanauza 20000/=) imagine unachukua miche 100 ! calculate hapo,hiyo miche wanadai ni very costful eti kwavile wanaichukua toka Kagera hadi hapa kwetu Njombe ! .Na wana vijana wao wanaofika kukupandia hiyo miche na gharama ya huduma hiyo unailipia kwenye hiyo taasisi yao.

Niseme kifupi kuwa gharama ni kubwa sana tena sana kwa hapa mwanzoni za huo uwekezaji.Kingine wanachowasadikisha watu including wakulima wanadai hilo zao wao ndo watakuja kuwa wanunuzi kwa wakulima.Swali ni je ni kweli kilo moja ya vanila ni shilling million moja na nusu(sh 1500000/=)? .

Ukweli wa bei ya soko kwa sasa ni shilling ngapi kwa kilo moja ya vanila? .

Karibuni wakuu kwa maoni yenye tafiti juu ya hili zao na hizi propaganda zinazosambaa huku Njombe
 
Niliskia Naibu waziri wa kilimo alitahadharisha kwamba bei ya hilo zao kwa kilo si zaidi ya sh 20,000/= hivo tuwe makini tusijekua sisi ndiyo fursa
 
Back
Top Bottom