Naomba kufahamu ajira za makatibu tarafa

M CM

JF-Expert Member
Nov 25, 2012
2,493
1,472
Hivi ajira za makatibu tarafa hutolewa wakati gani? Na ili upate nafasi hii unatakiwa uwe na qualification gani? pia naomba kufamishwa hao makatibu wanalipwa kiasi cha mshahara?
 
Hakuna muda maalumu wa ajira hizi, ila kwa uelewa wanguajira nyingi za serikali zinatolewa baada ya kupita kwa bajeti ya serikali hivyo basi vibali vya ajira vinatolewa kuanzia mwezi wa 10. kwa vigezo vya sasa ili uwe katibu tarafa unatakiwa uwe na degree au advance diploma katika fani za sanaa,uchumi, biashara,sheria, takwimu, mazingira.
Mshahara wa kuanzia ni TGS D ambayo kama 440,000 or 460,000 hivi (siyo actual figure but around that much).
Kwa utaratibu wa sasa ajira serikalini zinatangazwa na Sekretarieti ya Ajira Serikalini, nakumbua walitangaza nafasi nyingi zaidi ya 100 za maafisa tarafa mwezi wa 6, sijafuatilia kama walishafanya usaili.
Changamoto kubwa za kazi hizi ni kukubali kufanya kazi mbali nje ya miji nadhani karibu asilimia 95% ya maafisa tarafa wanafanya kazi wilaya ambazo zipo nje ya makao makuu ya mikoa.
Kwa sasa maafisa tarafa karibu wote wanatumia usafiri wa pikipiki, kuna kipindi serikali ilifikiria kuwapatia gari ndogo aina ya suzuki ila ikasitisha mpango huo, ikaona si vyema kuwapatia magari watu ambao hawana ofisi nzuri, kwa sasa serikali inampango wa kujenga ofisi nzuri za maafisa tarafa tanzania nzima manake nyingi ni mbovu sana
 
Dah' nimependa ulivyoshuka mkuu,,,!
Nahisi wewe ni journalist!
Big up.
 
Hapana ndg mimi na Afisa Utumishi nipo ofisi ya waziri mkuu, hii thread ipo kunako fani ,tunadili na tawala za mikoa na serikali za mitaa ambapo makatibu tarafa wapo, i know inside outside of the issue. Naitumia vizuri JF kuujuza umma

na sisi wachumi huwa tunalipwa sh ngapi huko serikalini?
 
sina swali la nyongeza, ama kweli jf ndo kilaki2. gud mr leo. walio fanyiwa usahli mwez wa6 wamesha ripot kazn. tangu mwez 10
 
Hapana ndg mimi na Afisa Utumishi nipo ofisi ya waziri mkuu, hii thread ipo kunako fani ,tunadili na tawala za mikoa na serikali za mitaa ambapo makatibu tarafa wapo, i know inside outside of the issue. Naitumia vizuri JF kuujuza umma

Afisa utumishi ebu nisaidie, mwenye fani ya uandishi wa habari anaweza kuajiriwa kama WEO?
 
Kwa mujibu wa muundo wa utumishi serikalini kama ulivyoainishwa kwenye Waraka wa Maendeleo ya Utumishi wa Mwaka 2002 sifa za kuajiriwa kama WEO Daraja la ii ni muombaji lazima awe na shahada ya sanaa yenye mwelekeo wa sayansi ya jamii (social Science) Utawala, public Administration and local government, Sheria au Sifa nyingine inayolingana na hizo kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na serikali na mshahara wake utakuwa tgs d kwa mwezi.
Na sifa za kuajiriwa kama WEO daraja la iii ni kuhitimu kidato cha nne au sita na kuhudhuria mafunzo ya stashahada yenye mwelekeo wa sayansi ya jamii (social science) Utawala, Public Administration, local government,stashahada ya sheria au sifa nyingine inayolingana na hizo kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na serikali.

Kutokana na sifa tajwa hapo juu unaweza pima mwenyewe uwezekano wa wewe kuajiriwa kwenye kazi hiyo kutokana na sifa zinazotakiwa na sifa ulizokuwa nazo wewe

Hapana ndg mimi na Afisa Utumishi nipo ofisi ya waziri mkuu, hii thread ipo kunako fani ,tunadili na tawala za mikoa na serikali za mitaa ambapo makatibu tarafa wapo, i know inside outside of the issue. Naitumia vizuri JF kuujuza umma

hapo hamna ajira mkuu nifanyie mpango ntakupa ata ya chai.
 
Siku hizi Sekretarieti ya ajira serikalini ndio inaajiri kwa niaba yetu pamoja na taasisi nyingine za serikali, sio rahisi sana kumfanyia mtu mpango, zamani kabla ya hii sekretarieti ingewezekana kufanyiana mipango. Mambo yote siku hizi skretarieti ya ajira serikalini na mimi kule sina mtu wa karibu wa kusaidia kwa hilo.
 
Kwanini makatibu tarafa wana mishahara midogo hivyo inalingana na watendaji wa kata ilhali wao ni ngazi ya juu kuliko WEO?
 
Hapana ndg mimi na Afisa Utumishi nipo ofisi ya waziri mkuu, hii thread ipo kunako fani ,tunadili na tawala za mikoa na serikali za mitaa ambapo makatibu tarafa wapo, i know inside outside of the issue. Naitumia vizuri JF kuujuza umma

Nakupongeza sana Mkuu kwa moyo wako mzuri ambao umetumia nafasi yako kutuelimisha sisi ambao hatuko kwenye system. Endelea hivyo hivyo Mkuu, naipenda JF kwasababu ya watu kama wewe. Big up Man!
 
Hapana ndg, mimi na Afisa Utumishi, nipo ofisi ya waziri mkuu, hii thread ipo kunako fani, tunadili na tawala za mikoa na serikali za mitaa ambapo makatibu tarafa wapo, i know inside outside of the issue. Naitumia vizuri JF kuujuza umma

Godwin, uko ofisi nzuri. Hebu nisaidie takwimu zifuatazo ambazo ni latest: Tanzania kuna mikoa, wilaya, tarafa, kata, vijiji, vitongoji na mitaa mingapi? Na je, kwa sasa tunao watumishi wa umma wangapi walio kwenye official government payroll? Nimepitia website kadhaa za serikali inayosema sasa inatembea hatua za e-government lakini nimekwama kupata majibu ya maswali haya. Pls, help.
 
Back
Top Bottom