Ushauri na Mbinu Mbalimbali Kuhusu Uendeshaji wa Biashara ya Kuosha Magari (Car Wash)

Ninaleta hizo mashine toka UK na Germany (used) na kuziuza hapo Dar na mikoa ya jirani. Chinese products zipo madukani hapo Dar lakini durability yake ni ndogo sana. Kuna vijana wanaosha magari makubwa kule Kurasini, walikuja kwenye yard yangu mara ya kwanza na walipoona ni used machine wakaziacha na kuamua kuingia madukani kununua mashine mpya za mchina kwa 2.5M Tsh, baada ya miezi miwili walikuja tena kwangu na mpaka sasa wanadunda mzigo kama kazi na wamekuwa wananipa oda mara kwa mara. Kwa sasa nina mashine mbili zimebaki pale yard. Ni PM tuwasiliane ili nikupe maelezo zaidi.
weka namba mkuu tufanye biashara
 
Interested na hii mada, ila inasikitisha watanzania wengi hatujui kushare informations. Wenye kujua wanajibu juu juu sana, mtu hafunguki kabisa.

Taja Vifaa vyote, ikibidi bei zake, mpya na used pia elekeza vinapopatikana.

Kodi ya eneo la Biashara

Malipo ya wafanyakazi yapo vp

Bei unachaji vp?

Faida kwa siku inaweza simama ngapi?

Aina za car wash
 
USHAURI WA VIFAA VINAVYOHITAJIKA

Vifaa vinavyohitajika kwa kuanzia ni Pressure Washer hii bei yake inategemeana na ukubwa wa mashine yenyewe lakini niliwahi kuona moja Jengo la NHC posta Bei ikiwa ni laki sita kama miaka mitatu nyuma.

Kifaa kingine ni Vacuum hiki ni kwaajili ya kuvuta uchafu ndani nayo bei yake inategemea. Tatu MAJI unafikiria kazi au biashara hii basi ufikirie maji ya uhakika kama hakuna maji ya Dawasco basi kwa Dar kuna wale wanaouza kwenye Makenta.

Eneo ambapo biashara hii utaifanya hapa bei inategemea na eneo na mwenye eneo. Lakini pia kingine ni Sabuni maalumu za kuoshea magari hizi sifahamu wapo zinapatikana na bei zake sifahamu.

Vijana wa kufanya nao kazi ambao watakuwa wanaosha malipo mtakubaliana
Vitambaa vya kuoshea na kufutia magari
Polish na Airfresh

Baada ya hapo bei nadhani zinajulikana japokuwa zinatofautiana sehemu na sehemu lakini bei nayofahamu mimi ni Shilingi Elfu 10 kwa gari ndogo hizi Sedan, SUV hatchback nk.

Mengi nadhani wapo wanaoweza kuongezea kila la heri katika kulifanikisha hili
 
Ajabu mada sensitive kama hizi masaa mawili post hata hazifiki 15 ila sasa mwendawazimu mmoja aanzishe uzi hapa akizungumzia ukubwa wa makalio au udogo wa maumbile ya kiume ndani ya 30minute utakuta unasoma pages 4.

Sijui Watanzania maisha tunayachukuliaje!!!
nmecheka kwa uchungu sana. Daah yani ukianzisha mada za hivi hawaji kabisa. Bora wakuu mmeliona hili
 
nmecheka kwa uchungu sana. Daah yani ukianzisha mada za hivi hawaji kabisa, bora wakuu mmeliona hili

Au hata huu huu uzi we sema una car wash yako, unahotaji wafanyakazi ila wawe mabinti wenye makalio makubwa na unaulizia wapi utawapata, utaona mtiririko wa mauzoefu
 
USHAURI WA VIFAA VINAVYOHITAJIKA

Vifaa vinavyohitajika kwa kuanzia ni Pressure Washer hii bei yake inategemeana na ukubwa wa mashine yenyewe lakini niliwahi kuona moja Jengo la NHC posta Bei ikiwa ni laki sita kama miaka mitatu nyuma.

Kifaa kingine ni Vacuum hiki ni kwaajili ya kuvuta uchafu ndani nayo bei yake inategemea. Tatu MAJI unafikiria kazi au biashara hii basi ufikirie maji ya uhakika kama hakuna maji ya Dawasco basi kwa Dar kuna wale wanaouza kwenye Makenta.

Eneo ambapo biashara hii utaifanya hapa bei inategemea na eneo na mwenye eneo. Lakini pia kingine ni Sabuni maalumu za kuoshea magari hizi sifahamu wapo zinapatikana na bei zake sifahamu.

Vijana wa kufanya nao kazi ambao watakuwa wanaosha malipo mtakubaliana
Vitambaa vya kuoshea na kufutia magari
Polish na Airfresh

Baada ya hapo bei nadhani zinajulikana japokuwa zinatofautiana sehemu na sehemu lakini bei nayofahamu mimi ni Shilingi Elfu 10 kwa gari ndogo hizi Sedan, SUV hatchback nk.

Mengi nadhani wapo wanaoweza kuongezea kila la heri katika kulifanikisha hili
Aiseee kuna uwezekano hii biashara inalipa
Sana kama gar ndogo n 10 bhas
Hi biashara iko na faid nzur
 
Au hata huu huu uzi we sema una car wash yako, unahotaji wafanyakazi ila wawe mabinti wenye makalio makubwa na unaulizia wapi utawapata, utaona mtiririko wa mauzoefu
Watakuelekeza mpaka mjumbe wao wa nyumba 10
 
Habari za wakati huu wana JF natumaini ni wazima wa afya nielekee moja kwa moja kwenye mada, naomba ushauri kuhusu biashara ya car wash faida na changamoto zake kuna vitu nahtaji kuvjua kabla cjawekeza.

Mahali ni Dodoma
 
Poleni mihangaiko wakuu.

Nina idea ya kuanzisha biashara ya kuosha magari (car wash) ya kisasa kati ya mikoa mitatu i.e Dar Es Salaam, Tanga au Pwani (Kibaha/Mlandizi) sasa ningependa kujua mlolongo wa gharama za uanzishaji lakini pia uendeshaji wake kwa maana ya (management) lakini pia bila kusahau Faida zake na changamoto zake. Binafsi Pesa ya capital itapatikana na ipo tu ya kutosha. Nakaribisha maoni na ushauri wenu wakuu. Ahsanteni!!!
 
Sina sana experience. Ila naweza shauri kitu hapo.

Kwanza Uwe na pressure washer. Ukipata za umeme naona ni nzuri zaidi ukicompare na zile za kutumia mafuta.

Ukiweza kutega eneo la karibu na barabara nadhani itakuwa safi zaidi. Halafu unaweza ukaweka na huduma ya choo cha kulipia hapo hapo kwa ambao watakuwa sio wateja wako.

Penye wengi hapaharibiki neno. Wengine watakuja kujazia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuhusu iyo biashara, Mtaji ni pressure washer na Eneo (Paved area) issue ya kuandaa eneo tunaweza tusiwe na gharama bayana ila unaweza tafuta eneo la kukodi au kununua kisha ukasakafia kwa zege na kuweka Lanes kama 4 hivi kwa ajili ya kuosha magari watatu au manne kwa wakati mmoja. Tafuta bati, tengeneza cannopy vizuri mambo yawe sawa.
 
Sina sana experience. Ila naweza shauri kitu hapo.

Kwanza Uwe na pressure washer. Ukipata za umeme naona ni nzuri zaidi ukicompare na zile za kutumia mafuta.

Ukiweza kutega eneo la karibu na barabara nadhani itakuwa safi zaidi. Halafu unaweza ukaweka na huduma ya choo cha kulipia hapo hapo kwa ambao watakuwa sio wateja wako.

Penye wengi hapaharibiki neno. Wengine watakuja kujazia.
Shukrani sana kwa mchango mkuu Ubarikiwe sana. Nadhani naaza kupata mwanga wa pa kuanzia.
 
Kuhusu iyo biashara, Mtaji ni pressure washer na Eneo ( Paved area) issue ya kuandaa eneo tunaweza tusiwe na gharama bayana ila unaweza tafuta eneo la kukodi au kununua kisha ukasakafia kwa zege na kuweka Lanes kama 4 hivi kwa ajili ya kuosha magari watatu au manne kwa wakati mmoja. Tafuta bati, tengeneza cannopy vizuri mambo yawe sawa
Ubarikiwe sana mkuu. Umenipa madini ya kuanzia. Shukaran sana.
 
Back
Top Bottom