Utaratibu unaotumika kuanzisha huduma ya maabara na zahanati binafsi

Kig

JF-Expert Member
Aug 13, 2012
1,076
456
Poleni kwa majukumu ya kila siku wadau wote wa jamiiforums hasa ukumbi huu wa JF Doctor.

Naamini JF doctor kuna watalaamu wengi na watu wenye uzoefu katika masuala ya afya na shughuli zinazoendana na afya ya binadamu. Kwa muda mrefu nimekuwa na wazo la kuanzisha maabara au dispensary lakini sijui taratibu za kuanzisha hii huduma. Mimi sijasomea udaktari wala mambo ya afya lakini napenda sana kusaidia jamii hasa katika swala la afya.

Nikianzisha huduma hii itabidi niajiri watalaamu kwenye fani husika (yaani laboratory technicians, doctors and nurses) ili kutoa huduma bora ya vipimo vya magonjwa mbalimbali, ushauri wa kitabibu na tiba kwa wagonjwa.

Naomba wenye uzoefu mnisaidie au mnipe maelezo kuhusu utaratibu mzima kuanzisha huduma kama hii (vifaa ninavyohitaji, mazingira kuweka huduma, usajili wa huduma yangu nk).

Natanguliza shukrani.

WADAU WENGINE WANAOHITAJI UFAHAMU WA BIASHARA HII
Habari ya77 wanaJF, Nakuja kwenu ili npate msaada wa kimawazo juu ya wazo langu la kibiashara la kufungua dispensary.

Mimi nina mtaji wa million kumi napenda kujua kiasi hicho kinatosha?? Na vitu vipi ni vya lazima kabla ya kuanza biashara hiyo hapa naitaji kujua vifaa vya lazma ikiwezeka na bei zake sokoni.

Changamoto zake na pia kama watapatikana wadau especially drs and sr./ nurses.
Poleni na majukumu ndugu zangu,

Nataka kuanzisha Dispensary kwa ajili ya kutoa huduma ya afya maeneo ya kijijini penye wakazi zaidi ya 10,000.
Naomba wenye utaalamu wanisaidie common requirements yaani vifaa na vitu vingine muhimu pamoja na vigezo vyake

Pamoja na makadirio ya gharama zote ili kuanzisha dispensary.

Kama kuna huge documents nitumie.

Asanteni sana.

MICHANGO YA WADAU
Muhimu sana
1. Electronic microscope
3. Centrifuge machine (manual)
3. Glucometer
4. Vitanda vinne futi tatu na godoro zake, mashuka na mackintosh
5. Drip stands nne
6.viti viwili na meza mbili +examination bed (s)
7. Mabenchi kwa ajili ya kusubiria/simple wooden chairs
8. Dawa za kuanzia

JENGO
1. Maabara
2.consultation room(s)
3. Two rest rooms (me +ke)
4. Store
5. Dirisha/chumba cha dawa
6. Chumba cha sindano / dressing/ surgical aid room

Tuanzie hapa!
Kiongozi hii ni biashara nzuri na hutajuta kuianzisha ukiwa serious. Nina rafiki zangu waliokwishaianza wanashuhudia kwamba inawalipa pamoja na kuwa ni huduma kwa jamii.

1. Kwanza muone RLT (Regional Laboratory Tecnologist/technician) atakupatia form za kujaza na utaratibu mwingine wa kuhusu jengo
2 Maombi yako yatakuwa forwarded kwenda wizara ya afya kwenye bodi ya maabara binafsi (PLHLB-Public Health Lab Board). Hii ndiyo mamlaka itakayofanya ukaguzi na kusajili maabara yako.

3. Wafanyakazi watakuwa wataalam wa maabara (idadi na qualification inategemea level ya maabara unayofungua). You may also need a cashier na mtu usafi (attendant)

Nadhani kwa kunzia inatosha.

Good luck!
Kwa million 10 hutaweza

Kwanza mahitaji ni lazima ujue mahitaji ya dispensary linahitajika jengo lisilo la makaz yan non residential building lisilopungua vyumba 8
Consultation room 1
Dressing room 1
Reception
Observation Room1
Injection Room 1

Na assume kwamba utajua na huduma za wagonjwa wa nje yan OPD kwahyo kuna resting room kma mbili
Nurse station 1
Unaweza weka office 1
Room ya files 1

Unaweza weka Phamarcy au Dispensing Room 1

Pia ili uongeze kipato lazima uwe na Lab Room mbili na size imekua determined na wizara

Kwahyo kma utaamua jenga nyumba yako hyo 10 m itaishia kwenye kununua mchanga na kokoto kma utaamua kodi nyumba ya size hyo ten millon inaweza kua kodi ya mwaka auu zaidi.

Sasa tunakuja kwenye vifaa bare in mind kwamba vifaa vya hospitali ni very expensive.

Tukija kwenye staffing wizara inatoa mwongozo kua mtu haruhusiwi kuendesha kituo cha afya hadi kila kitu kiwe in onder ikiwa umekamilisha idadi ya wafanyakazi na jengo na vitu vingine kwa hyo kma unaanza itakubid uwe na wafanyakaz wote hata kma sio wote vyeti vitahitajika ili kushawishi wizara ikube kibali kumbuka vyeti vina cost hela kila mwez minimum ni laki 3.

Wafanyakaz wanaohitajika kwenye zahanati, msimamiz au mganga mfawidhi sio lazima awepo kwenye kituo permanent huyo ni MD.

Tabibu hawa ndio wanakuowepo mara nyingi kwenye zahanati ma clinical officer CO

Nurses utahitaji mkunga mid wife na assistant nurses kama 3

Pia kuna mfamasia kma utafungua phamarcy au mteknolojia wa phamarcy kma utakua na dispensing tu.

Pia kma utaakua na maabara utakua nw mteknolojia wa maabara na msaidizi wake

Hapo nmeeleza kwa kifupi

Ila kabla ya kuingia kwenye hii biashara ni bora ujue biashara ya hospital au zahanati ina running cost kubwa so ili ku maintain quality na uwe honest unaweza kuta profit ina break even na running cost.

Ningekua ni wewe kwa huo mtaji ningejaribu fungua phamarcy pekee kwa kua phamarcy ni kma duka running cost ni ndogo.
1. Kuwe na cheti cha Daktari aliesajiliwa Tanganyika
2. Sajili Premise yako wizara ya afya
3. TIN
4. Business Licence
5. Hkikisha una vifaa vyote kabla ya ukaguzi. Vikiwemo kitanda cha mapumziko, examination room, Darubini ya kitabibu, yaani vifaa vya maabara Kwa ujumla na manesi wenye sifa wasiopungua wanne.
 
Habari ya77 wanaJF, Nakuja kwenu ili npate msaada wa kimawazo juu ya wazo langu la kibiashara la kufungua dispensary.

Mimi nina mtaji wa million kumi napenda kujua kiasi hicho kinatosha?? Na vitu vipi ni vya lazima kabla ya kuanza biashara hiyo hapa naitaji kujua vifaa vya lazma ikiwezeka na bei zake sokoni.

Changamoto zake na pia kama watapatikana wadau especially drs and sr./ nurses.
 
Kwa tsh mill kumi naweza kufungua dispensary nkaajiri watumishi na kupata faida?? Ntapenda nkipewa breakdown ya vitu vinavyotakiwa.....
 
Ni DISPENSARY wala si DISPENCERY kama ulivoandika, andika collectly ili uonekane kuwa upo serious na kitu unachotarajia kufanya otherwise tutakuona na mzushi unayepima kina cha maji kwa kujifanya unataka kufungua DISPENSARY, makosa madogo kama hayo ndio ambayo yanaweza kukufanya ukampatia mtu dawa tofauti na ugonjwa anaoumwa, otherwise wish you all the best in your plans to open the DISPENCERY.
 
sawa, ngoja arudi tumhoji.

Muhimu sana
1. Electronic microscope
3. Centrifuge machine (manual)
3. Glucometer
4. Vitanda vinne futi tatu na godoro zake, mashuka na mackintosh
5. Drip stands nne
6.viti viwili na meza mbili +examination bed (s)
7. Mabenchi kwa ajili ya kusubiria/simple wooden chairs
8. Dawa za kuanzia

JENGO
1. Maabara
2.consultation room(s)
3. Two rest rooms (me +ke)
4. Store
5. Dirisha/chumba cha dawa
6. Chumba cha sindano / dressing/ surgical aid room

Tuanzie hapa!
 
Mkuu pamoja na ushauri ambao wadau wanakushauri hapa..ni vyema pia ukapata uzoefu kidogo kwa kuwatembelea waliokwisha anzisha hizi Dispensary..

Kila la kheri..!
 
Ni DISPENSARY wala si DISPENCERY kama ulivoandika, andika collectly ili uonekane kuwa upo serious na kitu unachotarajia kufanya otherwise tutakuona na mzushi unayepima kina cha maji kwa kujifanya unataka kufungua DISPENSARY, makosa madogo kama hayo ndio ambayo yanaweza kukufanya ukampatia mtu dawa tofauti na ugonjwa anaoumwa, otherwise wish you all the best in your plans to open the DISPENCERY.

Kwanini msitumie lugha adhimu ya Kiswahili? Wewe mwenyewe umechemka! umemwelimisha kimakosa! Sio "collectly" jirekebishe kwanza kabla hujaanza kumwshambulia mwenzio.

Yeye ametoa wazo lake, pongezi kwa waliompa ushauri, binadamu wengine mmeumbwa kutosaidia wenzenu. Wapeni moyo wanaotaka kujiongezea kipato ili umaskini upungue au upotee kabia hapa Tanzania.
 
Back
Top Bottom