Naomba kufahamishwa uhalali wa kimamlaka alionao WEO katika hili

baba francis

New Member
Mar 6, 2016
2
0
Ni wiki sasa imepita tangu Mtendaji kata alipochukua vifaa vyangu vya pool table kwa kosa la kufunguliwa kabla ya muda.

Lakini kila nikimfuata anadai hajisikii kunipa na atakapojisikia kufanya hivyo, atanitafuta yeye mwenyewe.

Je, mamlaka ya kisheria yanamtaka kufanya hivyo (kukaa na vifaa vyangu kwa muda huo wote) mpaka atakapojisikia kunipatia?

Na je nikiamua kununua vifaa vingine ili biashara yangu iendelee, athari zake ni zipi kisheria?
 
Ilitakiwa akupeleke mahakamani uadhibiwe kwa mujibu wa sheria zilizopo. Na ukishindwa kulipa fine ya halimashauri, unaweza fungwa
 
Mkuu muwekee mtego wa rushwa anataka mpunga 2 huo hana lolote.We chukua mpunga umpe upge kazi ushauri wa bure uktaka wa hela nenda kashtaki hakuna atae kusaidia hata mia.
 
Back
Top Bottom