sungura23
Member
- Apr 1, 2013
- 52
- 73
Habari wakuu? Natumaini wote ni wazima.
Wakuu naomba kwa mwenye kufahamu taratibu za kukomboa (to claim) mafao ya NSSF iwapo mtu ulikuwa unafanya kazi na mwajiri alikuwa akipeleka michango.
Mwaka 2017 hadi 2019 nilipata fursa ya kufanya kazi kwenye sekta ya masuala ya hospitality. Mwajiri wangu alikuwa akipeleka michango yangu na baada ya mkataba wangu kumalizika nikarejea dar. Baada ya kurejea dar sikuwahi kuwa na ajira rasmi ambayo inapeleka michango yangu NSSF. Hvyo tangu 2019 hadi mwaka huu uanachama wangu una akiba ileile ya miaka miwili ya mwajiri wangu kwenye sekta ya hospitality niliyofanya 2017 mpaka 2019.
Jana nimeingia kwenye portal ya NSSF kwa namba yangu ya uanachama nimeona installment zangu zote pamoja na akiba ambayo bado sijaikomboa (unclaimed balance). Vyote viko sahihi na mwajiri wangu aliwasilisha michango yangu yote ya mkataba wangu wa miaka miwili.
Maswali yangu:
1. Je ninaweza kuiokomboa hii akiba?
2. Je taratibu zake ni zipi?
3. Kuna madai kuwa huko NSSF kuna usumbufu mno, je ni kweli? Yaani hata kama una akiba yako lakini ni shughuli mpaka wakupatie chako. Haya madai ya kuwa kuna usumbufu nimepewa na watu wasiopungua watatu, ikiwa mmojawapo nilikuwa nae huko kwenye hyo kazi tuliyofanya miaka miwili.
4. Na iwapo wakikulipa kuna makato yoyote?
5. Na wanalipa kwa which mode of payment? Wanakuwekea kwenye akaunti? Au bank cheque?
Naomba msaada wenu wakuu
Ahsanteni