Naomba kufahamishwa ngazi za mishahara kwa wenyeviti mbalimbali wa bodi hapa nchini

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,292
2,000
Salamu ndg zangu.Poleni na stress!

Kumekuwa na teuzi mbalimbali kwenye nafasi za Mwenyekiti wa Bodi fulani fulani.Mfano Bodi ya Maziwa. Bodi ya Nyama.Bodi ya Mfuko fulani nk nk.

Hawa huteuliwa na Mh Rais.

Naomba kujua stahiki za wenyeviti wa bodi interms of:

1. Mshahara

2. Posho za vikao

3. Kupewa gari la serikali

4. Kupewa nyumba ya serikali

5. Nguvu yao nk nk

Asanteni sana

tapatalk_1512572306411.jpeg
 
BigBro

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,509
2,000
Hawalipwi mishahara, wanachukua posho katika kila vikao wanavyokaa, ila posho zao ndefu kidogo kuanzia 500,000 to 1.5 M. Sisi kwetu alikuwa anachukua 900,000 kila kikao plus mafuta na posho ya dereva wake. Vikao vilikiwa kila baada ya miezi miwili.
 
mnengene

JF-Expert Member
Nov 21, 2011
1,913
2,000
Hii ya posho ya vikao, nakumbuka msajili hazina ulitoa waraka kupinga kulipwa kwa posho za vikao.
Alielekeza kila mjumbe wa bodi kulipwa kitu kinaitwa ada ya ukurugenzi ( director fee) .Ambayo inalipwa kwa mwaka
Hakuna muongozo wa kiasi cha fedha kwenye ada ya ukurugenzi uliotolewa na serikali hivyo mashirika yanatofautiana kwenye kulipa.
Kuna mashirika unakuta yanalipa ada ya ukurugenzi mwenyekiti labda million 60 kwa mwaka, wajumbe million 40, mengine mwenyekiti million 15 ,wajumbe million 10.
Fedha hii mara nyingi kwenye mashirika mengi inagawiwa mara 4, kwa utaratibu kwamba msajili ameweka utaratibu wa bodi za mashirika kukutana isizidi mara 4 kwa mwaka labda kuwe na jambo la dharura, kwa hiyo kwenye kila kikao wanapewa hiyo sehemu ya ada ya ukurugenzi.
Kuna baadhi ya mashirika yanatoa posho ya nawasiliano kwa wajumbe wa bodi, hii nayo inatofautiana baina ya mashirika, kuna mashirika mwenyekiti wa bodi anakula million 3 kwa mwezi kama posho ya vocha, wajumbe wanakula 2.5 kila mwezi.
Aidha kuna mashirika yanagharamia semina mbali mbali kwa bodi, mfano ppra wameandaa semina kuhusu masuala ya manunuzi huko aicc arusha basi shirika linaweza kugharamia wajumbe wa bodi wahudhurie semina hiyo.
Kiufupi ujumbe wa bodi hauna mishahara ni posho tu na inategemea na uhai wa shirika.
Ujumbe wa bodi unalipa kwenye mashirika makubwa kama tanapa, bandari, mifuko ya hifadhi
Aidha mahusiano ya wajumbe na katibu wa bodi _ CEO wa shirika nayo yana determine ulaji kwa bodi members, kama bodi haina uhusiano mzuri na CEO anaweza kuwabania,
Mara nyingi wajumbe wa bodi wanajipendekeza kwa CEO ili awaandalie mazingira mazuri ya kupiga posho
 
Slim5

JF-Expert Member
Jan 7, 2014
25,564

Kumbe mianya bado ipo? Utamaduni wetu mzuri sana. Hakuna kuzungumza wakati wa kula!
 
Mlaleo

JF-Expert Member
Oct 11, 2011
11,279
2,000
Kama nina udhaifu wa fikra basi wewe una udhaifu zaidi.

Kwa sababu umeshindwa kujibu swali la mtu mwenye udhaifu wa fikira.
Bora udhaifu wangu wa kutomjibu Chizi. maana ni Busara kwani kujibizana naye nami nitaonekana Chizi pia
 
Al-Watan

JF-Expert Member
Apr 16, 2009
11,922
2,000
Bora udhaifu wangu wa kutomjibu Chizi. maana ni Busara kwani kujibizana naye nami nitaonekana Chizi pia
Wewe ni chizi kweli kweli.

Unaandika hunijibu mimi chizi, usije kuonekana na wewe chizi, wakati unanijibu.

Unaithibitishia dunia kwamba wewe ni chizikweli kweli.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom