Naomba kufahamishwa mchakato wa kusajili jina na kufungua akaunti ya pamoja BRELA

kendy

JF-Expert Member
Apr 30, 2015
246
500
Habari zenu wadau wa Biashara,

Naomba kujua yafuatayo:

Nimefungua biashara ndogo lengo langu ni ili ije kuwa kubwa. Ninashirikiana na mke wangu hivyo nataka tuwe na jina moja la biashara tofauti na majina yetu (kwa mfano kuunganisha majina, mfano Thomas na Catherine tuunganishe na iwe TOMCAT),hivyo nataka nikasajili BRELA hilo jina la biashara, tuwe na akaunti moja ya benki kwa ajili ya biashara tu.

Nitafanyaje ili niweze kufanikisha hilo? Nimeshaanzisha biashara tayari, leseni ya biashara ilinitaka niandike jina moja tu, na tayari nimepata leseni kwa jina langu.

Je ili niweze kupata jina la biashara na tuwe na akaunti ya pamoja kama nilivyoeleza hapo juu itawezekana. Nia ni ili nikisafari, mke wangu asimamie biashara, na mke wangu akisafari nisimamie biashara. Je nifuate njia gani ili kufanikisha lengo hilo?

Naomba kuelekezwa process za kusajili jina na kufungua akaunti ya pamoja.

Asanteni.
 
konda msafi

JF-Expert Member
Sep 5, 2018
1,124
2,000
Ingia kwenye website ya brela ujisajili. Mle utakuta option za kufungua biashara unayoitaka. Basically unaweza kufungua biashara kama mtu binafsi au kampuni. Kufungua kama mtu binafsi haina complication sana. Utahitaji kuwa na TIN na barua kutoka serikali ya mtaa unakohitaji kufungulia hiyo biashara. Kama ni kampuni hii iko complicated.
 
konda msafi

JF-Expert Member
Sep 5, 2018
1,124
2,000
Ukishapata usajili kutoka Brela ndio unaweza kwenda bank kufungua account ya hiyo biashara.
 
encyclopaedia Tanzaree

JF-Expert Member
Sep 10, 2017
479
500
Ingia brela.go.tz nenda kwenye ONLINE BUSINESS NAMES halafu chagua create new account. Utatengeneza akaunti ya online halafu utaingia kwenye account yako na kubonyeza sehemu wameandika START then NEW E-APPLICATION then New business name. Kwakuwa mpo wawili utachagua PARTNERSHIP kwenye upande wa OWNERSHIP then utaendelea na kuingiza taarifa za owners.
Utahitajika kuwa na namba za NIDA zako na MWENZAKO.
Huitaji TIN namba kusajili jina BRELA ila itahitajika TRA wakati wa kutengeneza TIN ya pamoja.
Ukikwama popote usisite kuuliza nitakupa majibu, hizo ndio kazi zangu.
 
kikiboxer

JF-Expert Member
Dec 22, 2017
1,013

Mkuu naomba namimi nidandie huu uzi.
Tayari nimesajiri jina juzi wamenipa certifucate ya registration.
Sasa nataka kwenda TRA nina TIN binafsi je hii watabadilisha au itabidi nipatr ya biashara nq pia kuna documents gani za kwenda nazo hapo TRA ili nipate kukamilisha
 
encyclopaedia Tanzaree

JF-Expert Member
Sep 10, 2017
479
500
Mkuu naomba namimi nidandie huu uzi.
Tayari nimesajiri jina juzi wamenipa certifucate ya registration.
Sasa nataka kwenda TRA nina TIN binafsi je hii watabadilisha au itabidi nipatr ya biashara nq pia kuna documents gani za kwenda nazo hapo TRA ili nipate kukamilisha
Hilo jina umesajili BRELA kama partnership au individual?
Kama kwenye extract inasoma jina lako peke yako utatumia TIN ile ile yenye jina lako sema wata update TIN certificate yako na kuongeza hilo jina la biashara.
Mfano jina lako ni COVID BARAKOA MATESO na jina lako la biashara ni KITAKASA INVESTMENT basi TIN yako itasomeka COVID BARAKOA MATESO (T/A) KITAKASA INVESTMENT hiyo (T/A) maana yake ni "TRADING AS"
documents zinazotakiwa ni;
1. Cert. Of Registration and extract from Registrar.
2. Barua ya serikali ya mtaa unapofanyia biashara.
3. Copy ya Kitambulisho (hasa cha utaifa)
4. Mkataba wa pango la biashara uwe umesainiwa na Mwanasheria na akupe receipt ya EFD.
5. kama BRELA umesajiliwa kama partnership itahitajika PARTNERSHIP DEED ( kutoka kwa mwanasheria).
 
Muuza simu used

JF-Expert Member
Aug 23, 2017
3,488
2,000
Habari zenu wadau wa Biashara,

Naomba kujua yafuatayo:

Nimefungua biashara ndogo lengo langu ni ili ije kuwa kubwa. Ninashirikiana na mke wangu hivyo nataka tuwe na jina moja la biashara tofauti na majina yetu (kwa mfano kuunganisha majina, mfano Thomas na Catherine tuunganishe na iwe TOMCAT),hivyo nataka nikasajili BRELA hilo jina la biashara, tuwe na akaunti moja ya benki kwa ajili ya biashara tu.

Nitafanyaje ili niweze kufanikisha hilo? Nimeshaanzisha biashara tayari, leseni ya biashara ilinitaka niandike jina moja tu, na tayari nimepata leseni kwa jina langu.

Je ili niweze kupata jina la biashara na tuwe na akaunti ya pamoja kama nilivyoeleza hapo juu itawezekana. Nia ni ili nikisafari, mke wangu asimamie biashara, na mke wangu akisafari nisimamie biashara. Je nifuate njia gani ili kufanikisha lengo hilo?

Naomba kuelekezwa process za kusajili jina na kufungua akaunti ya pamoja.

Asanteni.

Limbwata itakuwa imehusika kwa asilimia 100,kwanini usifungue kampuni kupitia majina ya watoto wako?!utakuja kunishukuru baadae
 
drkinga

JF-Expert Member
Sep 16, 2013
422
250
Hilo jina umesajili BRELA kama partnership au individual?
Kama kwenye extract inasoma jina lako peke yako utatumia TIN ile ile yenye jina lako sema wata update TIN certificate yako na kuongeza hilo jina la biashara.
Mfano jina lako ni COVID BARAKOA MATESO na jina lako la biashara ni KITAKASA INVESTMENT basi TIN yako itasomeka COVID BARAKOA MATESO (T/A) KITAKASA INVESTMENT hiyo (T/A) maana yake ni "TRADING AS"
documents zinazotakiwa ni;
1. Cert. Of Registration and extract from Registrar.
2. Barua ya serikali ya mtaa unapofanyia biashara.
3. Copy ya Kitambulisho (hasa cha utaifa)
4. Mkataba wa pango la biashara uwe umesainiwa na Mwanasheria na akupe receipt ya EFD.
5. kama BRELA umesajiliwa kama partnership itahitajika PARTNERSHIP DEED ( kutoka kwa mwanasheria).
Msaada tutani Mkuu... Naomba kujulishwa... Kwa mujibu wa taratibu na sheria .. Inawezekana Kusajili Kampuni Ukiwa mtu mmoja tu??
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom