Naomba kufahamishwa kuhusu mkopo wenye riba ndogo kutoka Hazina

MUBIKU

JF-Expert Member
Oct 24, 2014
276
376
Wakuu habari za muda huu, leo ni siku ya mapumziko poleni na mihangaiko ya juma zima. Kama kichwa cha habari hapo juu kinavyojieleza nilipenda kufahamu juu ya mkopo kutoka Benki kuu ya Tanzania (HAZINA).

Hii ni kutokana na ukweli kwamba maisha bila kuchukua mkopo huwezi kufikia malengo kwa muda mfupi, hivyo basi kama ilivyo ada mtego mkubwa wa wafanyakazi wa Serikalini ni kudumbukia kwenye mikopo kutoka mabenki ya kibiashara ambayo yamejaaa Riba kubwa mnoo inayopelekea maumivu kwa mtumishi.

Aidha ningependa kufahamu kuhusu juu ya huo mkopo kutoka HAZINA maana nimeskia ni mkopo wenye riba ndogo sana , hivyo wakuu kwa wenye uelewa kuhusu hilo naomba anijuze ili niende nikapate huduma hiyo.

Ahsanteni na karibuni kwenye mjadala huu.
 
Hiyo mikopo Ni kwa taasisi za fedha na sio watu binafsi ..

Bank hukopeshwa na Bank Kuu sio wewe.
Sivyo mkuu.. watu binafsi wanapata mkopo wa hazina muda sana tangu enzi za nyerere, sharti tu uwe mfanyakazi serikalin.. na riba ni nafuu sana(3%)..sema hii fursa ilikua haifiki chini huku..ilikua inaishia kwenye ngazi za juu za uongoz kwenye wizara.

Na Hazina kuu na Bank kuu ni vitu viwili tofauti.
 
Sawa
 
Huo utaratibu uliotangazwa juzi na BoT, ni kwa ma bank ya biashara ambayo yatakuwa yanapata mkopo kwa riba ya 3% na wao wanautoa kwa sekta binafsi kwa riba isiyozidi 10%, ila sharti ni kwa wale wanaoingiza pesa hiyo kwenye sekta ya kilimo tu.
 
Hivi unaifahamu Serikali yetu wewe?

Ni kweli, kiutaratibu BoT ndiyo yenye jukumu la kupanga namna ya uendeshaji wa Benki zote nchini, ikiwemo kupanga kiwango cha riba za mikopo. Lengo ni kudhibiti wananchi wasidhurumiwe. Hii imekuwa ikifanywa na BoT mara nyingi tu.

Lakini, Je, inatekelezwa?

Benki gani ikubali kutoa mkopo kwa riba ya 3-10%? Benki ipi hiyo kati ya hizi ambazo ndiyo ziko hadi huku vijijini (NMB, TpB, CRDB, NBC). Hayo ni "changa la macho" tu ndugu yangu au waswahili husema ni kiini macho.

Riba ni kuanzia 18% kwenda juu, tena unapewa na masharti kibao yasiyo rafiki. Waulize watumishi wa sekta ya umma!
 
Hivi unaifahamu Serikali yetu wewe?
Ni kweli, kiutaratibu BoT ndiyo yenye jukumu la kupanga namna ya uendeshaji wa Benki zote nchini, ikiwemo kupanga kiwango cha riba za mikopo. Lengo ni kudhibiti wananchi wasidhurumiwe. Hii imekuwa ikifanywa na BoT mara nyingi tu...
Unataka kusema kwamba mabenk yana sauti kuliko BoT?, Hapa kipingamizi kikubwa ni kuwa Serikal ilikuwa inatoa mitaji kwa Benk za biashara kwa Riba kubwa.

Hivyo basi kwavile wenyewe serikali wamekiri kupunguza riba kwa benki hizo automatically hii itaruhusu benk hizo kupunguza riba yaan ni win win situation maana tukumbuke benk za kibiashara zinataka faida , serikal pia inataka faida ila wanachi wake wasiumie.
 
Hiyo mikopo Ni kwa taasisi za fedha na sio watu binafsi ..

Bank hukopeshwa na Bank Kuu sio wewe.
Inawezekana huna tarifa sahihi ukweli ni kwamba hiyo fursa ipo kwa wafanyakazi kupata hiyo mikopo kutoka hazina na cha muhimu ni kufika sehemu husika yaani halmashauri kupata mwongozo.
 
Hiyo mikopo Ni kwa taasisi za fedha na sio watu binafsi ..

Bank hukopeshwa na Bank Kuu sio wewe.
Mkuu acha kumpotosha muhusika kwa jambo usilolijua vyema-Kiufupi ni kwamba mikopo hii hutolewa kwa wafanyakazi wa taasisi za umma kwa riba ya 3% ingawa upatikanaji wake ni changamoto mno mno,kupata ni bahati kidogo.
 
Huko jikoni huwa kuna mikopo mitamu sana ila taarifa zake hubaki siri, lazima uwe na koneksheni ndio ujue.
 
Sivyo mkuu.. watu binafsi wanapata mkopo wa hazina muda sana tangu enzi za nyerere, sharti tu uwe mfanyakazi serikalin.. na riba ni nafuu sana(3%)..sema hii fursa ilikua haifiki chini huku..ilikua inaishia kwenye ngazi za juu za uongoz kwenye wizara.

Na Hazina kuu na Bank kuu ni vitu viwili tofauti.
Hao Hazina Saccos riba yao siyo 3%.
Ni 13%-15%.
Soma hapo chini 👇👇

Screenshot_20210821-093310.png
 
Kwa watumishi Ni rahisi kumkopa mwajiri kwakuwa mkopo wa mwajiri hauna riba unakopa mshahara wako unakatwa taratibu
 
Back
Top Bottom