Naomba kufahamishwa kuhusu kanisa la New Life in Christ

Online Pastor

JF-Expert Member
Sep 7, 2017
1,949
2,000
Wapendwa,

Nimekuwa nikikutana na kanisa hili katika huduma zangu za kiroho na muda mwingi sikulipeleleza sana.

Ila hapo jana nilikutana na muumini wa kanisa hili,japo hakujieleza vizuri na kulipambambanua kanisa lake,ila nilipata mwanga kidogo.

Mwenye kuwajua vizuri hawa jamaa naomba afunguke zaidi.
 

Hazchem plate

JF-Expert Member
Feb 25, 2011
10,317
2,000
Msichanganye sana wakuu. Now days kuna Makanisa na kuna ministry/ huduma.

Kwa kifupi makanisa ambayo yapo tanzania yanajulikana. Ambayo ni popular ni kama RC, Waprotestant wote eg. KKKT, Moravian, Anglican na Baptist pia kuna makanisa ya maaruufu kama ya kilokole Eg. EAGT na TAG au assembies na waambata wao, Pia kuna Wasabato, Orthodox na mengine.

Ambayo yanasajiliwa ma masajili wa makanisa pale wizara ya mambo ya ndani. Ambapo kunakuwa na majimbo au Dayosis. Na pia lazima yawe yalikuja ki missionary.

Now days kuna hizi ministry A.K.A Huduma za kiroho.
Hizi mtu binafsi huanzisha either yeye kwa wito wake au ufadhili wa watu wa nje. Sasa hizi husajiliwa katika Category yake tofauti na makanisa ya kawaida kwa mujibu wa sheria.

Mf. Ni hiz ministry zenye wachungaji wakubwa na wenye majina makubwa nadhani wote mnazifahamu sima haja ya kumnominate mtu hapa.

Sasa kwa swali la mtoa mada sijui amelenga nini. Ila nadhani iyo ni ministry na sio kanisa kwa maana ambayo nimeieleza hapo juu thou Yote tunaita makanisa tuu

Sijui muuliza swali anataka kujua nn. Ila nadhan kwa brief iyo kila mtu atapata concept kidogo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom