Wakuu naomba kufahamu kama nitajitahidi kuwekeza na kujiajiri katika uanzishaji wa shule ya awali. Kama kuna sheria na kanuni zozote ambazo zinatakiwa kufuatwa naomba kufahamishwa hapa. Pia msaada wa vitu kama gharama na mambo mengine ya msingi kwa wenye uzoefu. Eneo ambalo nafikiria kufanya huo mradi ni Dar.