Naomba kufahamishwa bei ya Mashudu ya alizeti

Habari wakuu

Ningependa kufahamu bei ya mashudu ya alizeti pamoja na soko la uhakika kwa hapa Dar es Salaam.

Ahsante
Mkuu ungejazilizia nyama nyama kidogo kwenye swali lako

Unataka mashudu ununue au unayo unayauza?

Mashudu ni malighafi ya kutengenezea vyakula vya mifugo soko lake kubwa ni viwanda vya vyakula vya mifugo ambavyo vipo kwa wingi Kenya na wana bei angalau kidogo

Wanunuzi wengi husafirisha kwenda kenya huko kuna soka la uhakika na ndio linatoa bei ya manunuzi hadi huku Tz

Mashudu yanapanda na kushuku kulingana na msimu na uhitaji wa viwanda kwa wakati husika

Kwa wastani viwanda vya kenya vinanunua kuanzia sh 800 hadi 500 kwa kilo moja ya mashudu
Wachuuzi wengi hununua kulingana na bei hizi

Ikiwa watanunua labda kwa sh800 kwa kilo basi huku bongo watanunua hadi kwa sh 500 kwa kilo hapo wakiweka usafiri labda sh 100 kwakilo na gharama zingine hadi kufika Kenya unakuta kilo moja ina cost labda 600, faida inakua ina range kati ya sh 150 hadi 250 kwa kilo
Hapo akiwa na kilo zake 35,000 ambazo ndio ujazo wa wastani wa magari makubwa ya kubeba mzigo anapata faida flani nzuri
Siri ya hii biashara ni wingi wa mzigo kwakuwa faida ni ndogo kwa kilo ila wingi utakubeba

Kwa kadiri unavyokua mzoefu kwenye biashara ndivyo utakavyokua mzuri pia kwenye kupunguza gharama ili mzigo ufike na wastani mzuri wa bei kwa kilo

Wanunuzi wa bongo viwandani sina uzoefu nao sana maana wana magumashi nyingi sana ukipeleka mzigo kwao yaani faida yote itaishia kwa wajanja wajanja wanaojifanya wana connection na kiwanda
Wakenya hawana sana longolongo viwandani
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom