Naomba kuelimishwa nini hatma ya Balozi wa Marekani kufuatia anguko la Trump?

Wanasiasa huku Africa hawana aibu, na bado ataenda kanisani bila kujali madhila na maumivu ya wengine simply hawako chama chake
Changieni mada husika wakuu mpo OP kabisaa.

MAENDELEO hayana vyama ila MAENDELEO ya KWELI utayapata CCM.
 
Unachosema kuhusu Mkataba wa Vienna si sahihi. Kila serikali ya nchi inaamua yenyewe itamteua nani. Akiteuliwa na kutajwa kwa serikali ya nchi nyingine, nchi ile (inayompokea) inaweza kumkataa (ambayo kwa kawaida hawafanyi maana inaleta matatizo katika uhusiano) . Mengnevyo hupokelewa ndiya balozi. kama alipita kwenye chuo cha nini au alifuga kuku au nini- Hii haidhuru kisheria, si sehemu ya mkataba wa Vienna. Ukiona tofauti, heri ulete nukuu!

Jisomee hapa: UNTC
Sielewi ulichokisema ila mimi nimekuelezea haki ya nchi husika yaani "host nation" kutangaza persona non grata kwa balozi ambae hawana imani nae.

Hizi ni provisions na zipo 53.

Hiyo ipo katika Article 9 ya mkataba huo.

Outline of Provisions​

The treaty is a broad record consisting of 53 articles. Here are some of the important Articles mentioned under the Vienna Convention on Diplomatic Relations, 1961:

Article 9 of the Vienna Convention on Diplomatic Relations states that the host country, whenever and for any reason, can pronounce a specific individual of the diplomatic staff to be non-acceptable. The sending state shall recall this individual within a reasonable timeframe or, in any case, this individual may lose his or her diplomatic immunity.

Hivyo hata "sending county" ifanyeje host nations anapoamua ndio huwa uamuzi wa mwisho kwa kufuata mkataba huu.

NB: kwa faida ya wengi

"Host Nation" ni nchi mwenyeji na "Sending state" ni nchi inayotuma balozi.
 
Sielewi ulichokisema ila mimi nimekuelezea haki ya nchi husika yaani "host nation" kutangaza persona non grata kwa balozi ambae hawana imani nae.
Soma ulichoandika "balozi Wright hana uzoefu wa masuala ya kidiplomasia kwa kushiriki bega kwa bega shughuli za kisiasa ndani ya nchi husika kinyume na mkataba wa Vienna au Vienna Convention"
Kuwa na uzoefu au kukosa uzoefu wa maswali ya kidiplomasia si kitu kinachojadiliwa katika mkataba huo. Haidhuru kisheria.
Kila kuhusu kumkataa balozi (persona non grata) ni kitu kingine, hii ni sawa kabisa, tena ni lazima maana nchi haiwezi kumshika au kumkamata balozi , inaweza tu kumwambia aondoke.
Ila tu ulianza na mambo mengine ambayo si sahihi, yaani swali la uzoefu au mafunzo.
 
Mkuu,

Nafikiri maelezo niliyoyatoa yamejitosheleza uzuri tu bila konakona.

Huyo balozi hakuwahi kuwa balozi huko nyuma hadi alipoteuliwa mwaka 2019.

Na nimetanabaisha kwamba ni rafikie Donald Trump kwa maana kwamba alimteua kwa misingi ya urafiki.

Sasa wasemaje huyo mtu ni mwanadiplomasi na ana uzoefu?

Kwa mfano, mbona hatujaona mabalozi wa Ujerumani na Uingereza wakifanya "actively" alichokuwa akifanya yeye mitandaoni?
 
HAyo ni mawili tofauti. Kama balozi anaweza kazi yake au la, ni kitu kingine. Tena inategema jinsi unavyoiona. Mfano wakati wa uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi pale Kenya, balozi wa Ujerumani alijitoea kufanya kazi ya dereva kwa wagombea wa upinzani kwa sababu maisha yao ilikuwa hatarini, kuna stori 2,3 jinsi alivyoenda kuangalia maandamano ya upinzani, wakati polisi ilianza kutumia siaha kali alimchukua kiongozi kwenye gari lake la kidiplomasia. Rais Arap Moi alifoka.
Mimi nilijibu tu sentensi yako kwamba kutokuwa na uzoefu wa kazi ya diplomasia kunapinga mashariti ya Mkataba wa Vienna. si vile.
Kumtangaza balozi kuwa non grata inaweza kutokea kwa balozi yeyote, kama alitangulia kufagia barabara au kama ana PhD ya diplomasia au kama ni profesa. Kisheria haidhuru.
 
Asante kwa mchango mzuri tupatieni elimu.

MAENDELEO hayana vyama ila MAENDELEO ya KWELI utayapata CCM.
 
Balozi kama hatakiwi na host Country huwa anaondolewa mara moja hakuna mahojiano. Mfano kwa serikali ya Marekani, Mabalozi wao huwa wanaondolewa mara nyingi wakati Rais anapokuwa kutoka chama kimoja kuwa madarakani na kingine kuingia. Mfano Republicans wakishinda wanaweka mabalozi ambao wanatumikia sera za Republicans. Vile vile Democrats mara nyingi wanaweka wakwao. Hilo linatokea kwenye all strategic countries. Baada ya Republicans kupoteza urais utaona Balozi wao anaweza kubadilishwa haraka sana japo kuwa hajamaliza mwaka. Haya yanatokea sana tu ni kwa sababu wengi hawajui kwamba yanatokea. Alipoingia Trump mabalozi wengi wa USA nchi nyingi tu waliondolewa/kubadilishwa. Biden naye atawalima wengi tu, vibarua vinaota mbawa kama uyoga.

Mfano Sara Kuku alivyoondolewa.
 
Kimsingi ni kweli unachosema kuhusu utaratibu wa mabalozi wa Marekani.
Ila tu si kweli ukisema "Hilo linatokea kwenye all strategic countries" (pamoja na kutumia Kiswahili kibaya). Si vile.
Hii inaweza kutokea kama nchi fulani inamteuea balozi kama cheo cha kisiasa kinachoweza kutolewa na kuondolewa kwa hiari ya kiongozi. Marekani ni mfano mmoja. Pale ni kweli raisi mpya mara nyingi (si wakati wote) atamteua rafiki, mwanasiasa au mfadhili wa kampeni yake kuwa balozi na kumtuma. Rais anayefuata atateua wengine (mara nyingi, si kote). Mfumo huu hautegemei kama nchi ni "strategic" au la, unategemea utaratibu wa ndani kwao.
Lakini katika nchi nyingine haiwezekani au angalau si kawaida. Pale mabalozi huteuliwa kati ya watumishi wa idara ya ng'ambo , ambao wameshakuwa na maarifa ya kutosha katika kazi ya ubalozini mbalimbali. Kwa Kiingereza huitwa "career diplomats". Kwa hiyo hakuna sababu ya kuwabadilisha kufuatana na vipindi vya kazi vya rais au vya kiongozi wa kisiasa, wanafuata utaratibu wa kawaida wa wizara yao. Wakati mwingine waziri mpya analeta watu wake kwa ajili ya nchi maalum akipenda kubadilisha mwelekeo wa siasa yake pale, hivyo balozi aliyepo anahamishwa mapema, lakini harudi kwenye biashara yake jinsi ilivyo Marekani.
 
Back
Top Bottom