Naomba kuelimishwa nini hatma ya Balozi wa Marekani kufuatia anguko la Trump?

Muju4

JF-Expert Member
Oct 27, 2014
5,322
7,160
Nawasalimu wanabodi,

Baada ya matokeo ya uchaguzi wa Marekani kutoka na Trump kuangukia pua, ningependa wajuzi wa mambo ya Diplomasia mnipe muongozo katika swali langu hapa chini:-

Je, baada ya President elect Biden kuapishwa tutegemee Balozi wa Marekani kukusanya mabegi na kurudi kwao Marekani na hivyo kupata Balozi mteule mpya?

Naomba msaada wenu,

Asanteni sana.

Uchaguzi umeisha sasa tuijenge nchi
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 
Balozii kisa alikemea uchaguzi wetu unafikiria atafukuzwa baada ya Trump kushindwa pole sana
Daah! Nimeombwa kuelimishwa mie sipo huko kabisa.

Otherwise

Uchaguzi umeisha sasa tuijenge nchi
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 
Kwanini kwanza umeulizia huyu balozi wa TZ,unataka aondoke au utaki aondoke?
 
Utashangaa mwenyewe hata akija Balozi mwingine. Marekani inaendeshwwa kwa misingi fulani siyo utashi wa mtu kama Jiwe.
 
Kwanini kwanza umeulizia huyu balozi wa TZ,unataka aondoke au utaki aondoke?
Sasa nitamuuliziaje wa Yemen na mimi naishi Tanzania?

Nisaidie kidiplomasia changes za Rais huwa zinakuaje?

Uchaguzi umeisha sasa tuijenge nchi
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 
Itategemea...

Is he a career diplomat or some political appointee?!

Kama ni political appointee basi anaweza kubadilishwa lakini kama ni career diplomat, basi anaweza kubaki!

All in all, kwa kiasi kikubwa, ingawaje Senate nayo ina nafasi yake, bado itategemea na Biden mwenyewe ikiwa ataona bado anastahili kuiwakilisha US ndani ya Tanzania, au hapana!!!
 
Balozi Donald J. Wright kitaaluma ni daktari na amefanya kazi zake nyingi za taaluma yake kwenye sekta ya afya.

Balozi Wright jina lake lilipendekezwa na Donald Trump ( ambae ni marafiki) mwaka 2019 kwenye kamati ya seneti ya mahusiano ya nje, na akapitishwa mwezi January 2020 na seneti hiyo ikampitisha baada ya kumpigia kura mwezi februari 2020.

Uteuzi wake niliweza kuuchukulia kuwa ni wa kumfungulia "business opportunities" bwana Wright akiwa Tanzania na tumemwona katika shughuli mbalimbali za kijamii alizojaribu kuzifanya.

Aliapishwa rasmi kuwa balozi mwezi April 2020 na akawasilisha hati za utambulisho kwa raisi Magufuli mwezi August 2020.

Baada tu ya kuwasilisha hati zake za utambulisho akaanza harakati zake za kisiasa ndani ya nchi mwenyeji na alichokifanya sote twakifahamu.

Hivyo balozi Wright hajasomea na kupitia taaluma za kidiplomasia na si mwanadipolomasia kitaaluma kama alivyo mzee wetu Bernard Kamilius Membe ambae alipikwa pale Kurasini.

Hivyo, twaweza kusema kwamba balozi Wright hana uzoefu wa masuala ya kidiplomasia kwa kushiriki bega kwa bega shughuli za kisiasa ndani ya nchi husika kinyume na mkataba wa Vienna au Vienna Convention on Diplomatic Relations.

Hivyo serikali ya Tanzania inaweza kuwa ilikuwa ikiangalia njia mbalimbali za kukabiliana na hitilafu aloonyesha balozi na hii ya kubadilika kwa uongozi huko Washington kunaweza kuwa mwanya kwa serikali yetu kutumia Article 9 ambayo itamtangaza balozi huyo kuwa "persona non grata", hivyo kuitwa Washington haraka.
 
Nawasalimu wanabodi,

Baada ya matokeo ya uchaguzi wa Marekani kutoka na Trump kuangukia pua, ningependa wajuzi wa mambo ya Diplomasia mnipe muongozo katika swali langu hapa chini:-

Je baada ya President elect Biden kuapishwa tutegemee Balozi wa Marekani kukusanya mabegi na kurudi kwao Marekani na hivyo kupata Balozi mteule mpya?

Naomba msaada wenu,

Asanteni sana.

Uchaguzi umeisha sasa tuijenge nchi
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
Siku zake zinahesabika, anafungasha muda si mrefu. (Mimi binafsi simpi hata miezi miwili).

1604774656689.png

Kwa huzuni kubwa Trumpet akielekea kwenye golf course yake ..... ...... sore loser.
 
Balozi Donald J. Wright kitaaluma ni daktari na amefanya kazi zake nyingi za taaluma yake kwenye sekta ya afya.

Balozi Wright jina lake lilipendekezwa na Donald Trump ( ambae ni marafiki) mwaka 2019 kwenye kamati ya seneti ya mahusiano ya nje, na akapitishwa mwezi January 2020 na seneti hiyo ikampitisha baada ya kumpigia kura mwezi februari 2020.

Uteuzi wake niliweza kuuchukulia kuwa ni wa kumfungulia "business opportunities" bwana Wright akiwa Tanzania na tumemwona katika shughuli mbalimbali za kijamii alizojaribu kuzifanya.

Aliapishwa rasmi kuwa balozi mwezi April 2020 na akawasilisha hati za utambulisho kwa raisi Magufuli mwezi August 2020.

Baada tu ya kuwasilisha hati zake za utambulisho akaanza harakati zake za kisiasa ndani ya nchi mwenyeji na alichokifanya sote twakifahamu.

Hivyo balozi Wright hajasomea na kupitia taaluma za kidiplomasia na si mwanadipolomasia kitaaluma kama alivyo mzee wetu Bernard Kamilius Membe ambae alipikwa pale Kurasini.

Hivyo, twaweza kusema kwamba balozi Wright hana uzoefu wa masuala ya kidiplomasia kwa kushiriki bega kwa bega shughuli za kisiasa ndani ya nchi husika kinyume na mkataba wa Vienna au Vienna Convention on Diplomatic Relations.

Hivyo serikali ya Tanzania inaweza kuwa ilikuwa ikiangalia njia mbalimbali za kukabiliana na hitilafu aloonyesha balozi na hii ya kubadilika kwa uongozi huko Washington kunaweza kuwa mwanya kwa serikali yetu kutumia Article 9 ambayo itamtangaza balozi huyo kuwa "persona non grata", hivyo kuitwa Washington haraka.
Asante sana Mkuu elimu haina mwisho.

Uchaguzi umeisha sasa tuijenge nchi
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 
Back
Top Bottom