Naomba kueleweshwa: Wapinzani wanapambana na Hayati Magufuli au Rais Samia?

matumbo

JF-Expert Member
Jul 9, 2011
7,225
3,944
Kila nikitazama mijadala kwenye mitandao ni kama wapinzani bado wapo kwenye mapambano na hayati Magufuli.

Rais na mwenyekiti wa sasa wa CCM mama Samia ni kama hawana tatizo naye, anawakosha sana na wanamtumia kuwaumiza wafuasi wa Magufuli.

Kwa wataalam wa siasa hii ina maana gani kwa siasa za upinzani?

Tutegemee battle ya wapinzani na Magufuli mpaka wakati wa uchaguzi 2025 au hapo katikati wataamishia vita yao kwa mama Samia?

Binafsi naona siasa za Magufuli zitatawala sana awamu hii maana naona Samia kaamua mapema kujifungamanisha na Magufuli.
 
Wapinzani wanapambana na mtu bila.kuelewa adui yao ni ccm matokeo yake tunarudi kulekule
Wameweka nguvu kubwa kwa Magufuli mpka wamesahau nini wanachotaka. Na uzuri mama Samia ameshausoma mchezo amefanikiwa kulishawishi kundi la Magufuli na wapinzani pia amewaweza tayari, siasa za Samia na upinzani zitakuwa nyepesi sana akiendelea hivi hivi kuwa controversial.
 
Mkuu kwa mujibu wa machadema na wapinzani wengine, matatizo yote aliondoka nayo Magufuli kwahiyo sasa hivi mambo yote ni safi na ccm ni mbele kwa mbele.

Yani sasa hivi kwaufupi ni kwamba baada ya kifo cha Magufuli wapinzani sasa wako ikulu na hata uchaguzi wa 2025 watashinda kwa kishindo maana ccm na mifumo yake kaondoka nayo Magufuli.

Tukiwaita hawa jamaa nyumbu wanakasirika.
 
Kma ulikuwa hujui wapinzani wametega samia labda wewe hujaelewa
Hapana, Samia amewazidi akili anaicheza game ya upinzani na ya Magufuli kwa wakati mmoja. Makundi yote yapo dilemma ila lenye kushinda litakuwa la Magufuli sababu wote awa na Samia ni ccm na kuna maeneo watapishana ila ikifikia lengo la kubaki madarakani lao ni moja na tofauti uwa zinawekwa kando.
 
Wameweka nguvu kubwa kwa Magufuli mpka wamesahau nini wanachotaka. Na uzuri mama Samia ameshausoma mchezo amefanikiwa kulishawishi kundi la Magufuli na wapinzani pia amewaweza tayari, siasa za Samia na upinzani zitakuwa nyepesi sana akiendelea hivi hivi kuwa controversial.
Waliweka nguvu kubwa kwa Magufuli kwa sababu ccm ilishakufa na Magufuli naye kashafariki hivyo sasa hivi wanaanua matanga tu.
 
Shujaa alikuwa anaweza kwenda pale Jitegemee-Mabibo akasema mbunge wa Ubungo, chapa kazi, maendeleo hayana chama, akatoka na msafara wake, akafika Kimara-Stop over akasema hawezi kujenga barabara kwa sababu walimchagua John Mnyika kutoka Chadema kuwa mbunge. Jamaa alikuwa ni mtawala anaeweza kujisahau ndani ya dakika 15 alichosema awali..... 😃
 
Iko hivi, wapinzani wanajua Magufuli aliwamaliza wakakosa sera na kutupwa kule. Wakakosa hoja, na ushawishi. Wakadharaulika na kukosa kura. Hii yote ni kutokana na uzalendo, ujasiri, ubunifu, uchapakazi, utambuzi, akili na maono ya Magu.

Na kwa sababu siyo wabunifu ikabidi wakimbilie mitandaoni na kuanza kutukana, kupiga propaganda za kuchafua, lakini kwa miaka 5 haikuwasaidia! Watanzania wakaonyesha support kubwa sana kwa Magu.

Ndiyo maana hata baada ya kifo cha Magu bado wanateswa sana na kivuli cha Magu. Wanatumia nguvu sana kuonyesha Magu si kitu. Lakini kuna tofauti kubwa Kati ya propaganda na uhalisia! Na bahati mbaya mambo aliyoyafanya ni halisi na siyo superficial Kama lawama zao. Huwezi ukakosoa ujenzi wa miundo mbinu ambao hata kipofu anaona umepunguza foleni, umerahisha usafiri, umepunguza gharama za usafiri na maisha! Uwezi ukakosoa nidhamu ya watumishi wa umma kuimarika kwa kiasi kikubwa, huwezi ukalazimisha kwamba uchumi haujakuwa, huwezi ukadanganya kwamba majambazi wameongezeka, ajali zimeongezeka, rushwa imeongezeka wakati vyote hivyo vimepungua kwa kasi ya ajabu.

Kwa hiyo wanavyompamba SSH ili aache mbinu za Magu ambazo ni proved zimewapiga mieleka miaka 5, kwa mahesabu kwamba akilegeza watapata upenyo.
Na wakikata upenyo Muda ukifika utaona watakavyomshambulia SSH!
 
Back
Top Bottom