Naomba kueleweshwa suala la ndege ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi ya Tanzania Bara kupokelewa Zanzibar

Zanzibar ni nji Tanganyika siyo nji. Hivyo kwa ufupi nji ya Zanzibar ndiyo inayoitawala Tanganyika baada ya kukubali kupoteza utambulisho wake na utaifa
 
NAOMBA KUELEWESHWA SUALA LA NDEGE YA WIZARA YA UJENZI NA UCHUKUZI YA TANZANIA BARA KUPOKELEWA ZANZIBAR.

ZAA = Zanzibar
TAA = Tanzania BARA

Naomba kueleweshwa kwa Uhuru wa mawazo "the right to express my opinion under Article 18 of the Constitution of Tanzania of 1977" kuanzia zamani hakuna pa kuongelea hadi zama za G55 ,Mchungaji Mtikila na sasa kwenye social media utapata mengi kuhusu malalamiko ya watanzania bara.

Tafuta habari ya ndege kupokelewa Zanzibar kisha soma maoni au nenda kwenye Political platforms mbalimbali,

Hoja sio MATUMIZI
Bali swala la Ujenzi na uchukuzi sio la MUUNGANO
Kwanini swala sio la MUUNGANO likafanyike Zanzibar??
Lini swala lisilo la MUUNGANO la Zanzibar litafanyika Tanzania BARA??
Ukiondoa Waziri wa Ndani Ulinzi Nje hakuna Waziri mwingine yeyote anahusika na chochote kule Zanzibar.

Pia TGFA na ATCL hawahusiki lolote kule Zanzibar sababu wapo Chini ya Wizara ya Ujenzi na uchukuzi isiyo ya MUUNGANO
Hapa MAMLAKA za Viwanja vya ndege Zanzibar wanayo yao
Usajili wa vyombo VYA usafiri wao
Kila kitu cha Ujenzi na uchukuzi chao wao wenyewe pekee DAIMA DUMU,

Ni vizuri wajue kuwa hizo ndege ni za Wizara ya Ujenzi na uchukuzi ya Tanzania BARA huko Zanzibar ni MAPOKEZI tu
Wasije anza sema SMZ imenunua ndege hizo
Hakuna kitu huninyima usingizi Kama Muungano tulionao, sie TANGANYIKA ni Mateka wa Zanzibar, ardhi mtanganyiki hapati Zanzibar, ajira,

KATIBA MPYA INAYOKUJA, CHA KWANZA NATAKA NIKUWEKA MUUNGANO SAWA JAPO YAPO MENGI NATAKA , MH RAIS SSH TUARAKISHIE KATIBA MPYA ,Tena mh hakikisha inatoka iyobora ya kutupeleka miaka 100 mbele


Nakuhakikishia ukifanya hivyo legacy utakayoiacha ndani ya nchi ,itakumbukwa KWa miaka Mingi Sana,
 
Hii ndo move aliyoshindwa kuicheza Nyerere pamoja na kuwa na upper hand kwenye negotiations zilizopelekea integration na zanzibar.....babu sijui alikuwa anawaza nini. Sasa unajikuta unatumia pesa nyingi ku-run serikali inayohudumia watu milioni moja unaipa status ya nchi wakati ungeweza kuipa status ya mkoa na kuondoa hizi kelele kelele zinazoendelea sasa.

Hata mkoa hawafai.

Zanzibar inaingia Sikonge mara 14.

GDP ya Kahama inaipita GDP ya Zanzibar mara kumi.

Wazanzibar kwa ujumla wao ( 1.2mil) hawajazi wilaya ya Kinondoni (1.7 mil)).

Wanawezaje kuwa na hadhi ya mkoa, achilia mbali nchi?
 
Kupitia huu Uzi nimeona jinsi gani sisi wa huku bara tulivyo wabinafsi na tuna roho mbaya....
Unawajua wenye chuki ubinafsi na zaidi CHOYO tena uliopotiliza katika huu unaoitwa muungano ambao sehemu moja kila kitu chao ni chao mwenyewe na sio sehemu ya muungano?? Ni Wazanzibari.

Kwa ufupi hawajachanga chochote kwenye muungano mambo yao yote na kila kitu chao wanacho na wamejifungia nacho na kila kizuri kipya kinachojitokeza kwao wanajifungia nacho wao pekee daima dumu,ni Wazanzibari.
 
Mimi ni MwanaCCM na ni Analytical Minded CCM member
Hivyo upenda kusaidia CHAMA changu cha CCM na SERIKALI yake kila eneo lenye changamoto na malalamiko ili kama itawapendeza Viongozi wetu wakuu wafanyie kazi ipasavyo kwa maslahi Mapana ya CCM SERIKALI zake TAIFA zima na Vizazi vijavyo.
 
Kuto kujadili / kuhoji Muungano ndio kero zinaongezeka, maana hiyo kutokuhoji tu nayo ni kero, lazima ifike mahala review ifanyike tena kwa kukusanya maoni kwenye sekta zote zinazohusu Muungano.
 
Mambo ya MUUNGANO ni MANNE tu lakini bado pia Zanzibar wanayo back up zake
ULINZI ( hapa wao wana vikosi MAALUM vya smz)
NDANI (Vikosi MAALUM vya SMZ)
FEDHA ( pia wana Wizara yao ya Fedha, Zanzibar REVENUE Board)
NJE ( hapa
Hivyo kwa Masuala hayo juu ndio maeneo shirikishi ya muungano tu

Nje ya mambo hayo mengineyo yote Zanzibar ni NCHI kamili.

Hivyo ukiwa unatoa bidhaa Zanzibar kuleta Bara jua unatoa kwenye NCHI kamili ambayo tayari imechukua ushuru na KODI zake yenyewe kwa ajili yake.
Hivyo huku Bara nao wanatakiwa wachukue KODI na USHURU wao wenyewe pia
Na hapa ndio chanzo cha MAGENDO kila kona na kujaa kwa bandari bubu kuanzia Tanga mpaka Mtwara.

Mtu anataka kushushia mzigo wa Sukari Mafuta Maziwa na bidhaa mbalimbali karibu kontena kadhaa mfano pale Mbweni malindi kwenye bandari bubu au Kwingineko mafichoni badala ya bandari rasmi pale posta as regards to Tax related practices and Price penetration Strategies
 
Mfano hai,unaweza kuingiza gari Znz na likasajiliwa badae ukaamua kulileta Bara. Litakapofika Bara utapaswa kutengeneza kadi ili kuruhusu kusajiliwa Bara kwa vile kila upande wa JMT una sheria yake ya usajili wa magari na pia kuweka takwimu sa magari yanayoingia nchini ili kujulikana yalipo. Kadhia utakayotengeneza inaweza kutozwa kodi ikiwa kuna tofauti (tofauti ya iliyolipwa Znz na inayopaswa kulipwa Bara na tozo ya Usajili) hasa ukizingatia kwa kuwa viwango vya kodi ya VAT ni tofauti baina ya pande mbili.
 
Hoja hapa sio kuvunja muungano bali ni kusaidia CCM na SERIKALI yake kuonyesha mafanikio na changamoto ili maboresho yafanyike.
Mimi ni Economy and Business related person hivyo najua kuwa kwenye eneo hili ndipo kwenye changamoto kubwa sana ya maswala ya MUUNGANO kubwa sana.

Eneo hilo ndio tatizo kubwa kuliko yote maana huku BARA kuna WAWEKEZAJI wa makampuni na viwanda ili kuyalinda mfano bodi ya sukari inatoa vibali kwa viwanda husika kuleta tani 20 kutoka nje wakati uzalishaji wa ndani ni tani 80 ili kufika tani 100 zinazotakiwa kwa matumizi ya Tanzania bara.

Sasa unakuta huko Zanzibar kupitia bodi yao ya sukari nao wanatoa kibali cha tani 100 kutoka nje sababu hawana viwanda wakati mahitaji yao tani 10 tu hivyo hiyo 90 inalazimishwa kuletwa bara nje ya Utaratibu na kwa kutumia sea smugglers / smuggling kama lose cargo.

Utaratibu huu ukiendekezwa ndio utaleta MGOGORO mkubwa sana kwenye MUUNGANO maana WAWEKEZAJI wa Viwanda wa bara watashindwa biashara sababu ya smugglers kutoka Zanzibar wanajaza SUKARI ya bei RAHISI kutoka nje
 
Mambo yote ya Ujenzi na uchukuzi sio maswala ya MUUNGANO.
Kila upande unafanya mambo yake ya Ujenzi na uchukuzi wao wenyewe.

Zanzibar kuna Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na uchukuzi

Tanzania bars kuna Wizara ya Ujenzi na uchukuzi

Kila mmoja na bajeti yake miradi yake kwenye mipaka yake ya kazi.

Bandari pia sio swala la MUUNGANO

Kuhusu bandari kila mmoja anajitegemea
Zanzibar kuna Zanzibar Ports Corporation
Tanzania Bara kuna Tanzania Ports Authority

Wao wana
Zanzibar Revenue Board
Bara kuna
Tanzania Revenue Authority.

Huku BARA tumeweka ukuta wa makuti wanaingilia mambo ya bara
Huku ya Zanzibar wameweka ukuta wa Zege hakuna wa bara kujihusisha na chochote cha Zanzibar
 
BANDARI sio swala la MUUNGANO ndio maana hauwezi kuingiza gari Zanzibar ukaja nalo Tanzania Bara.

Rejea Mambo MANNE
ULINZI
NDANI
FEDHA
NJE
 
anzia kitendo cha makame mbarawa kuteuliwa kuwa waziri anaehusika na hizo ndege
 
Back
Top Bottom