Naomba kueleweshwa kuhusu fedha zinazotumika kujenga mradi wa SGR

uncle

JF-Expert Member
Dec 10, 2007
322
184
Kuna suala naona silielewi kwenye ujenzi wa SGR kila Rais Magufuli anapohutubia hupenda kujipambanua kuwa mradi wa SGR serikali inatumia fedha zake za ndani.

Lakini kwa kusoma sehemu mbalimbali naona kama tunakopa hela toka Mabenki ya nje mfano kipande cha Dar - Moro, kuna hela zimetoka mabenki ya Uturuki na Leo hii nimesoma kuwa Standard Chartered Bank wametoa hela kwa ajili ya kipande cha Moro- Makutupora.

Sasa huo mchanganyiko siuelewagi kabisa
 
Ni simple tu; kwani anaposema corona imekwisha unafikiri ni kweli hakuna corona au ni propaganda za kisiasa tu? Kwa yeye kuwa rais huwa anafikiri watanzania wote ni wajinga sana.

Hata mawaziri wake kila siku wanadhalilika kwa namna anavyowatendea, ni propaganda tu hakuna wakati nchi imekuwa na madeni makubwa kama awamu hii.
 
Wewe ukikopa hela inakuwa siyo ya kwako sio? Au ukikopa huwaga Hulipi?
Tofautisha Grant na Loan hiyo Mikopo Tutailipa sisi sisi wananchi hivo tunajenga kwa Pesa zetu ni kama wewe leo ukope Bank afu ujenge nyumba utasema bank imekujengea nyumba au utasema nimejenga nyumba?
Jiwe,Kabudi na Pole Pole wanasema SGR inajengwa kwa hela za ndani tena cash money,tena Jiwe akaenda mbali zaidi kuwakashifu watangulizi wake hasa Kikwete kwa kukopa hela na kufanya miradi ya maendeleo.
 
Hii nchi ngumu hakuna utakachofanya ukakubalike.

Hela ingeweza kutoka na kazi isifanyike, sijui hapo tungesemaje.

Hongera sana Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli,

Fanya kazi tu, pengine thawabu utapata Mbinguni siyo duniani hapa.
 
Kuna suala naona silielewi kwenye ujenzi wa SGR kila Rais Magufuli anapohutubia hupenda kujipambanua kuwa mradi wa SGR serikali inatumia fedha zake za ndani.

Lakini kwa kusoma sehemu mbalimbali naona kama tunakopa hela toka Mabenki ya nje mfano kipande cha Dar - Moro, kuna hela zimetoka mabenki ya Uturuki na Leo hii nimesoma kuwa Standard Chartered Bank wametoa hela kwa ajili ya kipande cha Moro- Makutupora.

Sasa huo mchanganyiko siuelewagi kabisa
Jibu hili hapa leo;

Screenshot_20201216-121630_Parallel Space.jpg
 
Magufuli anajuwa kuwa anatawala Watanzania ambao ndiyo watu wenye uelewa mdogo kuliko wote katika Afrika Mashariki. Ndiyo maana anakopa Benki za nje mnashanglia. Na siku ya uzinduzi anasema tumejenga kwa hela zetu mnamshangilia pia
 
Wewe ukikopa hela inakuwa siyo ya kwako sio? Au ukikopa huwaga Hulipi? Tofautisha Grant na Loan hiyo Mikopo Tutailipa sisi sisi wananchi hivo tunajenga kwa Pesa zetu ni kama wewe leo ukope Bank afu ujenge nyumba utasema bank imekujengea nyumba au utasema nimejenga nyumba?
Safi sana mkuu
 
Anamaanisha kwamba pesa zinazotumika zinatokana na pato la ndani na mikopo anayochukua italipwa kwa pato la ndani bila usaidizi kutoka nje. Hakuna Nchi itakayoombwa kutusaidia kulipa deni litokanalo na Ujenzi wa SGR.
Kuna suala naona silielewi kwenye ujenzi wa SGR kila Rais Magufuli anapohutubia hupenda kujipambanua kuwa mradi wa SGR serikali inatumia fedha zake za ndani.

Lakini kwa kusoma sehemu mbalimbali naona kama tunakopa hela toka Mabenki ya nje mfano kipande cha Dar - Moro, kuna hela zimetoka mabenki ya Uturuki na Leo hii nimesoma kuwa Standard Chartered Bank wametoa hela kwa ajili ya kipande cha Moro- Makutupora.

Sasa huo mchanganyiko siuelewagi kabisa
 
Hii nchi ngumu hakuna utakachofanya ukakubalike.

Hela ingeweza kutoka na kazi isifanyike, sijui hapo tungesemaje.

Hongera sana Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli,

Fanya kazi tu, pengine thawabu utapata Mbinguni siyo duniani hapa.
Umeielewa mada kweli?
 
Back
Top Bottom