Naomba kuelewesha kuhusu treni inavyosafirishwa kutoka inakonunuliwa mpaka kufika Afrika

Sammy1961

JF-Expert Member
Dec 23, 2019
298
303
Habari wana jamii forums

Kama ilivyo hapo juu ninataka kujua au kupata ufumbuzi.

Je, ni kwa namna gani unaweza kuinunua treni kutoka mabara ya America na kuweza kuifikisha hapa ilhali hakuna barabara ya moja kwa moja ya treni kutoka America mpaka huku Afrika?
 
1603122216604.png
1603122250234.png
1603122335650.png
1603122351404.png
1603122390340.png
1603122442083.png
 
Bila bahari maisha sijui yangekuwaje.

Maana usafiri wa mizigo mingi mikubwa kwa masafa marefu ni meli.
 
Una umri gani Mkuu?
Je Treni umewahi kuiona au unasimuliwa tu au kuiona kwenye Picha? Tuanzie hapo
Nadhani hapa hujamsaidia mleta mada instead ni sisi wanajamvi tukuulize kwanza wewe umri wako ili tuufahamu uelewa wako ktk kuchanganua mambo hasa kutambua maswali na kuyajibu sahihi!

Mleta mada,kama ulishawahi kuona karakana zinamofungwa pikipiki au Bajaj au mashine mbali mbali ndivyo treni inavyoletwa,huja ikiwa vipuri tu na kuunganishwa mwanzo wa kituo chake kimoja baada ya kingine mpaka kinakuwa chombo.

Hope nimesaidia kidogo nilipokosea watasahihisha wengine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
.............Nadhani hapa hujamsaidia mleta mada instead ni sisi wanajamvi tukuulize kwanza wewe umri wako ili tuufahamu uelewa wako ktk kuchanganua mambo hasa kutambua maswali na kuyajibu sahihi!

Mleta mada,kama ulishawahi kuona karakana zinamofungwa pikipiki au Bajaj au mashine mbali mbali ndivyo treni inavyoletwa,huja ikiwa vipuri tu na kuunganishwa mwanzo wa kituo chake kimoja baada ya kingine mpaka kinakuwa chombo.

Hope nimesaidia kidogo nilipokosea watasahihisha wengine.

Sent using Jamii Forums mobile app
Upo sahihi mkuu.

Sent from my TECNO WX3 using JamiiForums mobile app
 
Vinaletwa na meli mkuu kutoka huko vilipotengenezwa. Mfano Tanzania tulinunua vichwa vya treni (Diesel Electric Locomotives) toka nchi ya Marekani katika kampuni ya Electromotive Diesel (EMD) huko La Grange illoinnis aina ya GT38LC-3 ila kilichotokea vilijengwa tu hapo South Africa ila components za muhimu zaidi Kama Diesel Engine, Air compressor, Main Generator, Control Panel n.k vilitoka U.S.A ila vitu baadhi vilijengwa hapo hapo South Africa tunasema underlicence.

Baada ya kukamilika vililetwa vichwa 13 vya mwanzo na tukavipa identification number Kama 90 class vilishushwa hapo bandarini Dar es salaam.

Vingine 11 vilikuja kuleta tafrani fulani kuwa havina mwenyewe..
 
Back
Top Bottom