Naomba kuelewa mapato ya acre moja ya kila zao kwa mwaka: kahawa, korosho, migomba na parachichi

Silicon Valley

JF-Expert Member
Mar 6, 2012
1,092
1,116
Members wakulima na wazoefu wa hayo mazao,

Naomba kuelewa kama muongozo kwa ufupi mapato ya wastani kwa mwaka kwa kila zao hapo juu.

Naomba tu share uzoefu wetu kwa manufaa yetu sote.
 
Members wakulima na wazoefu wa hayo mazao,

Naomba kuelewa kama muongozo kwa ufupi mapato ya wasitani kwa mwaka kwa kila zao hapo juu

Naomba tu share uzoefu wetu kwa manufaa yetu sote
Parachichi moja shambani ni 100/=
Sokoni ni 500/=
Shamba hekari moja unalima miti 1000
Mti mmoja unazaa parachichi 1000-1500

Fanya 1000 × 1000 × 500 = 500,000,000/= (kwa bei ya sokoni)

Kama mnataka mali mtaipata shambani
 
Mkuu kati ya hayo mazao uliyoyataja nakushauri usilime mazao ambayo bodi inakupangia bei na mahali pa kuuza. Lima parachichi kubwa kwa umbo uza mwenyewe au zile za hass uuzie kampuni. Lima migomba, ndizi uza mwenyewe. Kahawa kama utakaanga na kuuza mwenyewe ila tafuta mbegu ya kisasa.
 
Kahawa inaingiza miche 500-700 kwenye heka.
Kuna baadhi ya mashamba wanapanda miche ya vikonyo mpaka miche 1500.
Mti mmoja wa kahawa ukiwa mkubwa unaweza kutoa mpaka kilo 5 za kahawa iloyo kobolewa(kuna Mkenya aliwahi kuniambia kwao mti mmoja unatoa hadi kilo 20 ya kahawa iliyo kobolewa) cha muhimu ni matunzo ya mche.

Sasa piga hesabu mwenyewe,pia ulizia eneo uliopo kilo sh ngapi.

Parachochi-sijui.

Korosho heka moja inapandwa miche 27.

Mti mmoja mkubwa unaweza kutoa kilo 112 kwa mujibu wa wataalam wa kituo cha utafiti wa Naliendele Mtwara, wao wana mti unazaa kilo 112 za korosho.
Bei mwaka huu sijui.

Kwa maswali zaidi kuhusu kulimo na ufugaji tuwasiliane 0713925634.
 
Parachichi moja shambani ni 100/=
Sokoni ni 500/=
Shamba hekari moja unalima miti 1000
Mti mmoja unazaa parachichi 1000-1500

Fanya 1000 × 1000 × 500 = 500,000,000/= (kwa bei ya sokoni)

Kama mnataka mali mtaipata shambani
Mtaani hii tunaita Spreadsheet Agriculture ambayo kwa mahesabu yako, Mkulima anatengeneza 100M. Hata ingekuwa nusu ya hivyo, mi nakwambia hata BoT wasingepata wafanyakazi! Yaani Ekari 10 mkulima atengeneze Sh 1,000,000,000/=! Hata Kikwete asingekuwa Msoga mida hii! Rostam Azizi nae wala asingehangaika na Taifa Gas! Hata huyo Rais wangu trillioni za kwenye ndege angezipeleka kwenye maparachichi! Da' Lily Tony ingekuwa keshakimbia SUA kabla hatujamjua hapa JF na hivi sasa ingekuwa anamiliki Private International Airport! Mbeya na Iringa na kote wanakolima maparachichi kungekuwa na mabomba ya maziwa mitaani! Kilimo cha bhangi kingekufa na mapusha wote wangehamia kwenye udalali wa maparachicihi! Wamakonde kwa kupenda kujichanganya! Akina Mangi na Nshomile wangetelekeza migomba na mibuni na hivi sasa wangejazana Mkoa wa Njombe, Iringa na kwingineko! Watani zangu Wahehe ingekuwa wameshaachana na hawa wala n'nya wa barabarani na hivi sasa wangekuwa wanapiga 👇 👇 👇

Dog.png
 
Parachichi moja shambani ni 100/=
Sokoni ni 500/=
Shamba hekari moja unalima miti 1000
Mti mmoja unazaa parachichi 1000-1500

Fanya 1000 × 1000 × 500 = 500,000,000/= (kwa bei ya sokoni)

Kama mnataka mali mtaipata shambani
Nimecheka sana,shamba la Hekari moja ni miti 70 mpaka 100 tu
 
Nimecheka sana,shamba la Hekari moja ni miti 70 mpaka 100 tu
Hii principle not practical Njombe maana miti haitanuki haraka kama mbeya.
Miti 80 kwa Njombe mopka ikafunge ni miaka 5+. Rungwe ardhi yake haikauki ila Njombe inakauka na muda mwingine umwagie.
Kuna jamaa yangu yeye ameweka miti 150 kwa heka na atakuwa inaipunguza kadri inavyo banana.
Binafsi nimeongezea line kwenye ile 8x8 hivyo utakuwa 4x4 heka 2 sasa utakuwa na miti 250. Hii ni pilot kwa project zinazofuata kwa hio naendelea kujifunza kwa vitendo Mwanzoni nilisikiliza ushauri ila sasa hivi shamba linanishauri nilinifanyie nini.
 
Tukiwa tunafanya utafiti huwa tunaanza na nadharia kwanza halafu baadae tutathibitisha nadharia kwa vitendo.

Ingia shamba mkuu uchumi mali
Kilimo ndio kazi yangu! Mjini nazuga tu! Kilimo cha parachichi nakijua hata uniamshe usiku wa manane,mwanzo mwisho!
 

Attachments

  • IMG_20230525_141241_026.jpg
    IMG_20230525_141241_026.jpg
    1.4 MB · Views: 33
Parachichi moja shambani ni 100/=
Sokoni ni 500/=
Shamba hekari moja unalima miti 1000
Mti mmoja unazaa parachichi 1000-1500

Fanya 1000 × 1000 × 500 = 500,000,000/= (kwa bei ya sokoni)

Kama mnataka mali mtaipata shambani
Unauhakika unacho kinena
 
Back
Top Bottom