Naomba kuelemishwa juu athari ya kupiga Ng'ombe chapa

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
2,056
2,515
Naomba sana kuelemishwa juu athari ya kupiga ng'ombe chapa. Naona ni agizo hili limetolewa na Mamlaka ya juu kuwa kila mfugaji apige ng'ombe wake wote chapa. Binafsi kwa uelewa wangu ng'ombe anapopigwa chapa ni wazi unaharibu ngozi yake na baadaye ngozi ya ng'ombe husika inapouzwa inauzwa kwa bei ndogo kwa sababu ya alama iliyopo kwenye ngozi na hasa ngozi zinazouzwa nchi za nje. Sasa basi naomba kuelemishwa ni kwa nini tunapiga chapa ng'ombe huku tukifahamu kuwa upigaji chapa unapunguza thamani ya ngozi?.
 
Ni kweli, lakini chapa hii inachukua kisehemu kidogo sana, pia sijui kwanini serikali imeamua kufanya hivi, tena kwa msisitizo mkubwa kiasi hicho, kwani kuna sehemu nilienda nikakutana na baadhi ya wafugaji ambao hawajapiga chapa, wakawa wananiambia wameambiwa walipe faini mil2 au kifungo jera.
 
Ni mwendo wa kuziwezesha halmashauri kimapato tu.
kama ni alama za ulinzi si wafungwe gps tracer location mfugaji ajue ng'ombe wake wapo wapi?nawaza
 
Ukiacha kushuka thamani kwa ngozi pia kuna ishu ya mateso na unyanyasaji wa wanyama, kama ng'ombe angekuwa na uwezo wa kusimulia maumivu anayoyapata sidhani kama wafugaji wangekubaliana na hilo zoezi..
 
Ni kweli, lakini chapa hii inachukua kisehemu kidogo sana, pia sijui kwanini serikali imeamua kufanya hivi, tena kwa msisitizo mkubwa kiasi hicho, kwani kuna sehemu nilienda nikakutana na baadhi ya wafugaji ambao hawajapiga chapa, wakawa wananiambia wameambiwa walipe faini mil2 au kifungo jera.
Kupiga chapa inasaidia mambo mengi sana ikiwamo , wizi, magonjwa nk

Sehem inayopigwa chapa n ndogo sana hivyo haiwez kuathiri
 
Ni mwendo wa kuziwezesha halmashauri kimapato tu.
kama ni alama za ulinzi si wafungwe gps tracer location mfugaji ajue ng'ombe wake wapo wapi?nawaza
Mkuu unafikiri GPS kwa ng'ombe mil 21 itagharimi kiasi gani? Je, serikali inazo hizo hela?
 
Nikuzitambua ng'ombe za wilaya Fulani na nyingine na za Tanzania na nchi nyingine ili kizuia wizi na uhamaji ovyo wa wafugaji .
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom