Naomba kuelekezwa taratibu za kazi za uchimbaji wa madini Mererani

Mkongo 1

JF-Expert Member
May 31, 2020
302
352
Wakuu habari za majukumu,

Wana JF, nina wazo la kujilipua kwenda Mererani nataka kwenda kua mchimbaji niwe nazama longo. Naomba kujua taratibu za kazi za machimbo hayo ukoje, na sina mwenyeji huko. Mwenye kujua chochote kuhusu machimbo hayo naomba anipe muongozo.

Karibuni
 
Ulipotaja kuwa ni machimbo nimejua unatafuta Tanzanite
sasa fanya yafuatayo ambao ni mipango niliyoikuta mwaka 1984 enzi hizo kukiwa na miji km Cairo na Lubumbashi
  • Tafuta pesa ya kukutosha kuishi miji hiyo ya machimbo angalau nauli na ya kula tu
  • ukifika omba kibarua chochote kwa matajiri wa hapo, (kuzamia shimoni wanaitwa wanaApolo)
  • ukiajiriwa huko ndipo unaweza kujua wanaitafutaje hiyo Tanzanite ukikutana na wajuzi wanaweza kukufundisha u-nyoka kwa ajili ya wizi wa mchanga wa mawe (hapo lazima uwe na cherenge na ungo)
 
Asante mkuu na pesa labda natakiwa kua na kiasi gani make mie Niko dar kwa sasa ndio ninawazo la kwenda huko
 
Nna mtu namjua ni stering wa mgodi mmoja hko
Sema huko si pamchezomchezo mzee
Ndomana nakuliza ushawahi kuzama chini

Ova
Kaka nimezama chini migodi ya dhahabu ambayo ni Buziba,mwabomba Nyaruyeye so Niko na experience ya kuzama chini nakujua pako vipi kama ikiwezekana mkuu njoo DM unipe connection nitashukuru kamanda
 
Kaka nimezama chini migodi ya dhahabu ambayo ni Buziba,mwabomba Nyaruyeye so Niko na experience ya kuzama chini nakujua pako vipi kama ikiwezekana mkuu njoo DM unipe connection nitashukuru kamanda
Cheki pm

Ova
 
kuna member waliomo humuhumu JF watakuelekeza matajiri wa mashimo ya Tanzanite ukazamie huko. usafiri ni nauli yako tu kutoka Dar hadi Tengeru, sijui km sasa kuna kituo pale KIA cha shortcut kuingia Mererani.

Chakula ni cha kawaida kuna migahawa mingi tu, pesa ikipungua mtajipikia. Kazi si mchezomchezo, na Tanzanite ni ya kubahatisha unaweza maliza miaka 10 usipate kuiweka mkononi km Laizer Bilionea alivyosota.

Ndio maana ukaulizwa unaweza kuzamia shimoni??? umesema unaweza. Huko shimoni kuna mengi, kuna mitobozano. kuiba shimo la wengine au kutengeneza njia ya kufuata mashimo yanayotoa, mara pwaa mmefumaniwa, mara pwaa maji yameingia kama ulichimba dhahabu utakuwa unaelewa.

Ngoja niwatafute member wa Mbuguni nitakuPM watakukaribisha
 
Hebu fatilia haya unaeza pata moja mbili tatu.

Kwanza panaitwa MIRERANI au ukishindwa itamka hivyo sema MERERANI,usitumie herufi L kwenye R.

Inapatikana mkoani Manyara ila pembezoni sana karibu na Mkoa wa Arusha au kilimanjaro(Moshi). Itategeme unatokea upande gani ila ukifika Arusha au Mosh nauli yake ni 2,500 kufika Mirerani.

Utakapo fika omba mtu akuelekeze mahali panaitwa Kijiweni(hapo ndo sehemu ambayo watu wachache huuza madini yao na wanaonunua wapo(mabroka) .
Utakapo fika mface broka yoyote mueleze azma yako hiyo ya uchimbani na muombe akuunganishe kwenye mgodi anao ufahamu yeye.

Tahadhari huyo broka atakapo kuunganisha lazima atakufanya kama lengo lake, yaani huwaga wanataka siku ukija fanikiwa uje umuuzie yeye madini(sasa hapa ndo anapoweza kukuliza mana dini wakuta la M20 anaeza kupa M5). Hi inatokana wengi kutojua dhamani ya madini na huwa wanatabia ya kuwahudumia hao wachimbaji kwa kuwasaidia mambo madogo kama ya Betri,tochi na maji ya kunywa n.k , hivyo ni kama anakuhonga ili siku ukipata uje ufanye nae kazi.

Kingine ni kuwa lazima utengeneze kitambulisho cha Mwana Appolo yaan mchimbaji hivyo ukishapata mgodi wakuchimba ndo utaanza fatilia hizo process ili wakati unakuja ingia getini unapita nacho(utambulisho).

Changamoto iliyoko ni kwamba unaeza fanya hiyo kazi hata miaka 10 hujawahi shika milioni. Ukipata sana ni ki jilaki ambacho unaamua kujipoza na nyama ... Na kwa wewe ambae huna mwenyeji unaeza kuta maisha yako yote ni kuwa huko migodini unalala huko huko miaka yote(hakuna vitanda lakini ni kwenye viroba alafu huko ndo makao makuu ya kunguni duniani).

Mwanzoni jifunze kunyamaza ili kusoma uone maisha ya huko camp(mgodini) yalivyo ila mbeleni usiwe mpole sana maana kule ni ubabe kidogo.
Pia madini yanaeza kutoka bosi akapiga zaidi ya Bilioni ila mkaambulia laki 2 au 3. Na jitaidi kuhoji maswali yenye kuonsha kama umshamba hufahamu mengi ili wayakujibu kijinga na kama umuelewa utajifunza kupitia hivyo. ila ukijidai umjanja kuna possibility kutopata natasi muhimu za juu maana wanatakaga kuwa na watu ambao ni hamnazo ili wawatumikishe itakavyo Yaan mtu anaeza beba kofia(kiroba) cha madini yenye dhamani ya zaidi bilioni na hadi kumfikishia bosi bila hata kuchukua chenga ya milioni 50.

Kila la heri mkuu
 
Hebu fatilia haya unaeza pata moja mbili tatu.

Kwanza panaitwa MIRERANI au ukishindwa itamka hivyo sema MERERANI,usitumie herufi L kwenye R.

Inapatikana mkoani Manyara ila pembezoni sana karibu na Mkoa wa Arusha au kilimanjaro(Moshi). Itategeme unatokea upande gani ila ukifika Arusha au Mosh nauli yake ni 2,500 kufika Mirerani.

Utakapo fika omba mtu akuelekeze mahali panaitwa Kijiweni(hapo ndo sehem ambayo watu wachache huuza madini yao na wanaonunua wapo(mabroka) .
Utakapo fika m face broka yoyote mueleze azma yako hiyo ya uchimbani na muombe akuunganishe kwenye mgodi anao ufahamu yeye.

Tahadhari huyo broka atakapo kuunganisha lazima atakufanya kama lengo lake yaan huwaga wanataka siku ukija fanikiwa uje umuuzie yeye madini(sasa hapa ndo anapoweza kukuliza mana dini wakuta la M20 anaeza kupa M5) hi inatokana wengi kutojua dhamani ya madini na huwa wanatabia ya kuwahudumia hao wachimbaji kwa kuwasaidia mambo ya Betri,tochi na maji ya kunywa hivyo ni kama anakuhonga ili siku ukipata uje ufanye nae kazi.

Kingine ni kuwa lazima utengeneze kitambulisho cha Mwana Appolo yaan mchimbaji hivyo ukishapatw mgodi wakuchimba ndo utaanza gatilia hizo process ili wakati unakuja ingia getini unapitw nacho.

Changamoto iliyoko ni kwamba unaeza fanya hiyo kazi hata miwka 10 hujawahi shika milioni. Ukipatavsaja ni ki jilaki ambacho unaamua kujipoza na nyama ... Na kwa ww ambae huna mwenyeji unaeza kuta maisha yako yote ni kuwa huko migodini unalala huko huko miaka yote(hakuna vitanda lakini ni kwenye viroba alafu huko ndo makao makuu ya kunguni duniani).

Mwanzoni jifunze kunyamaza ili kusoma uone ilivyo ilq usiwe mpole sanaaa kule ni ubabe kidogo
Pia madini yanaeza kutoka bosi akapiga zaidi ya Bilioni ila mkaambulia laki 2 au 3.

Kila la heri mkuu
Asante mkuunimekupata vilivyo
 
Wewe kamata sululu yako na beleshi (koleo au chepe) uende, mambo mengine yatajipanga huko kwa huko..
 
Mkongo 1 kanyaga twende huwezi potea hapo Mererani, mwanamume ni kupambana achana na sisi tunaotafuta utajiri kupitia mitandao tafuta karai na cherenge kaanze na nyoka hutakosa ya kula
1594467371658.png
 
Cherenge ndio nini mkuu
Cherenge ni km nondo kubwa ambayo mbele imechongoka kwa kazi maalumu ya kutobolea miamba ambapo utahisi hapo kuna jiwe, kwa hiyo unagonga mwamba ili kufuata njia/mkanda, ukipekecha unapata unga au mawe hayo,
Pia cherenge tunatumia km ngao mkono wa kulia kupangua mitunduru wakati tunafukuzwa na walinzi usiku, na karai unaweka mkono wa shoto kukinga kichwani na kulinda macho, bila hivyo utapofuka macho, usiku hatutumii tochi
 
Cherenge ni km nondo kubwa ambayo mbele imechongoka kwa kazi maalumu ya kutobolea miamba ambapo utahisi hapo kuna jiwe, kwa hiyo unagonga mwamba ili kufuata njia/mkanda, ukipekecha unapata unga au mawe hayo,
Pia cherenge tunatumia km ngao mkono wa kulia kupangua mitunduru wakati tunafukuzwa na walinzi usiku, na karai unaweka mkono wa shoto kukinga kichwani na kulinda macho, bila hivyo utapofuka macho, usiku hatutumii tochi
Kumbe kuna seleka sio la kitoto huko ground
 
Back
Top Bottom