Naomba kuelekezwa namna ya kutuma Pesa kutoka Burundi kwenda Tanzania

nyanda5

Member
Nov 25, 2014
49
40
Jamani naombeni msaada kwa anaefahamu namna ya kutuma pesa kutoka Burundi kwenda Tanzania.

Mimi ni Mtanzania, kuna biashara ninafanya na rafiki yangu wa Burundi sasa changamoto ninayokabiliana nayo ni namna kuhamisha pesa ya Burundi kuja Tanzania. Kuna 5 Million ya pesa za Burundi nataka kuitoa Burundi nipate kwa TZS lakini benki za hapa Tanzania hawakubali kubadilisha pesa ya Burundi ikiwa cash, wanasema hadi iwe kwenye akaunti.

Tanzania bank zote hawakubali pesa ya Burundi. Nilitaka kutuma kwa ECOCASH hii ni sawa na M-Pesa ya Burundi lakini mawakala Burundi wanasema hawaruhusiwi kutuma pesa nje ya nchi wanarushusiwa kupokea tu.

Ukienda bank kutaka kubadili pesa ya Burundi unapewa exchange rate mbaya yaani unaishia kupata $-USD kiduchu yaani pesa yote inakata unabaki na hata dola 1000 haifiki.

Naomba ushauri kama kuna mdau yoyote anajua namna ya kutoa pesa ya Burundi kuwa TZS.
 
Kama ipo burundi mwambie akutumie kwa western union or monegram yeye atatuma pesa ya burundi wewe utapokea Tsh. Next time ujifunze pesa uwe unabadilishia nchi husika nunua USD ndo usafiri na dola
 
uko Burundi si kuna tawi la bank ya CRDB ume jaribu kuona kama unapata msaada apo?
 
Sasa kama yuko karibu na border ya Tanzania has a kabanga anaweza kukutumia kwa m-pesa maana kuna mawakala wa m-pesa hata ndani ya burundi

Hata yeye amenijuza hivyo sema sasa mawakala wa mpesa wananyonya maana wanatoa 60,000 kwa kila laki moja ya Burundi. Yaani nusu ya kiwango ambacho mtu unapata kwa exchange rate ya halali. kama kukiwa hakuna namna itabidi kuwatumia haohao
 
yuko mji gani hapo Burundi
 
Yupo Bujumbura
Kama vipi afadhari alipe nauli mpaka border ya Kobero akutumie maana nauli ni elfu 20 kwenda na kurudi ila kama vipi hiyo aifanye kesho maana akianza safari sasa hivi atafika jioni sana na hayo manoti yanaweza mletea shida
 
Border ya Kobero wanabadili kwa exchange rate kiasi gani? Laki moja ya Burundi unapata Tsh ngapi mkuu? Kama utakuwa unafahamu hilo.
 
Hili tatzo la kubadilisha fedha n tatzo sana hasa nchi za east Africa mm Nina yuan 1500 had Leo hii nahangahka nazo hakuna benk inayokubali kibadili pesa hii
 
Back
Top Bottom