Naomba kuelekezwa namna ya kutengeneza Siki ya Mbilimbi

Jul 7, 2013
12
15
Habari za muda huu!

Samahani sana naomba kwa anaejua namna nzuri ya kuandaa siki ya mbilimbi iwe nzuri na tamu, kwa kutumia viungo mbalimbali kama vile nazi; pilipili; nyanya na kadharika.

Maana nina mti wangu hapa nyumbani umezaa sana na sijui namna bora ya kuandaa siki hiyo.
Najua humu ndani kuna wajuzi na wataalam wazuri tunaweza kuelekezana hatua kwa hatua.

Asante. Naomba kuwasilisha
 
Kuna aina mbili, tuanze na ya kupika.
Mahitaji
Mbilimbi
Nyanya
Kitunguu
Kitunguu saum
Tangawizi
Pilipili
Chumvi
Binzari ya njano

Hapa osha mbilimbi zako, tia chumvi na uzichemshe.

Zikiiva zichuje maji kisha ziweke kwenye maji baridi na uanze kuzitoa Moyo (vile vikamba vya ndani) huwa vina ukakasi.

Pembeni andaa pilipili, kitunguu saumu, tangawizi kiasi, kitunguu maji, nyanya kiasi na binzari ya njano (tumeric powder)

Visage vyote au katakata na upashe mafuta uviweke jikoni...
Mchanganyiko wa nyanya ukiiva weka zile mbilimbi ulizochemsha, vichanganye vizuri.

Ikiiva epua tayari Kwa kuitumia, unaweza Kula na mihogo, ugali, chipsi nk
 
Aina ya pili ni ya kuanika juani
Mahitaji
Mbilimbi
Nyanya
Kitunguu
Chumvi ya mawe
Binzari ya njano
Chombo kinachofunika vizuri

Hii utaosha mbilimbi zako, na uzikate vipande viwili kiurefu au vinne

Utaziweka kwenye chombo chenye nafasi na kinachofunika kisha utazitia chumvi (tumia chumvi ya mawe)

Kisha utakatia nyanya na kitunguu
Ongeza na binzari ya njano
Utafunika chombo vizuri na kuiweka juani.

Unaweza kuchukua Hadi wiki hivi kuwa tayari kuliwa.
 
Shukrani Mkuu.
Nimewahi kuila sehemu ni nzuri sana huku kwetu sijawahi ona acha nikaitafute sokoni nitengeneze.
Naomba kujua inaweza kukaa kwa muda gani ikishatengenezwa??
 
Unataka kujifunza kutengeneza siki ya mbilimbi au pilipili ya mbili
Siki kwa kingereza ni vinegar ambapo utengenezaji wake unatumia mida mrefu kidogo..waliosoma oxidation na fermentation wanaelewa
 
Back
Top Bottom