Naomba kazi katika uzoefu huu nilio nao ikiwa nitakufaa

Master Kutu

Member
Jun 8, 2021
77
174
Habari ya leo wakuu,mimi ni kijana wa kiume mwenye miaka 29,nna mke na mtoto mmoja, elimu yangu ni kidato cha nne naishi Dar.
Nimejitokeza hapa kuomba kazi utakayo ona naweza kufanya kwako kulingana na uzoefu nilio nao.

1. USAFI WA KAWAIDA AINA ZOTE

Naweza kufanya usafi wa kawaida nyumbani kwako, ofisini, kiwandani ama sehemu yoyote ile ikiwa ni pamoja na kufua nguo na kunyoosha, kusafisha sofa nyumbani kwako, kusafisha seats za gari na kwa gari yote, kusafisha madirisha,milango iliyo na uchafu sugu,rangi za kuta n.k

2. USAFI KWA UCHAFU SUGU ULIO SHINDIKANA

Naweza kufanya usafi wa ziada ulio shindikana kufanywa na wewe ama wasaidizi wako ofisini,ama watu watu wa house keeping katika Hotel,naongelea masink yaliyo fubaa ama kuwa na uchafu sugu naweza kung'arisha na kurudisha kuwa sink jipya kabisa, Tiles zilizo fubaa ama kuwa na uchafu sugu pia nang'arisha na kurudisha kuwa mpya kabisa tiles za chini na zajuu, naweza kung'arisha milango iliyo pauka kw uchafu sugu,makabati ya jikoni yaliyo pauka kutokana na mafuta pia nang'arisha.
Natengeneza dawa mwenyewe zenye uwezo wa kufanya kazi hizo kwa ufanisi wa hali ya juu kwahyo ikiwa tuta fanya kazi wote inaweza kukupunguzia gharama maana tuta nunua mali ghafi kwa bei ndogo na dawa tukitengeneza tuta tumia muda mrefu.

3. COUNTER

Naweza kufanya kazi katika bar, Supermarket,duka la bidhaa za jumla na vinywaji, ofisi za kuuza vitu mbalimbali mfano kampuni na Viwandani maana nna uzoefu katika kupiga hesabu na kuhakiki mzigo uliopo,mzigo unao ingia,jumla ya mzigo,ulio uzwa,baki ya mzigo baada ya mauzo na thamani ya jumla ya fedha kwa mzigo ulio uzwa hapo ikiwa ni pamoja na kufuatilia kila wakati uwepo wa mzigo eneo la mauzo ili kuzuia upotevu wa mali unao sababisha hasara.

4. USIMAMIZI WA BIASHARA NA MASOKO
Naweza kufanya kazi ya usimamizi wa biashara,maana nime fanya kwa muda wa miaka miwili nikihusika na usimamizi wa biashara na masoko, hapo ikiwa ni Katika kusimamia watumishi wote ofisini,eneo la kazi la kila mmoja,ufanisi wa kazi pamoja na malipo halali ya wateja, mauzo na masoko ya bidhaa na huduma za kampuni yetu kwa wateja wetu ikiwa ni pamoja na kufuatilia kufikia target kwa team ya mauzo, kusimamia matangazo sehemu mbalimbali tulizo lipia kwa kusikiliza tangazo lime rushwa hewani mara ngapi kwa siku na kusimamia matangazo ya kulipia katika social media ili kuongeza ufanisi katika kampuni yetu.

5. FUMIGATION
Naweza kuua wadudu wa aina zote ikiwa ni pamoja na kunguni,mende, viroboto, mchwa,fuko,panya n.k.Pia natumia dawa zangu nnazo tengeneza mwenyewe zina uwezo wa kuua wadudu kwa sekunde 30 tu.

6.KAZI YA CUSTOMER CARE
Naweza kudumisha mahusiano mazuri na wateja wetu kwa kuwasikiliza wana taka tuwafanyie nini ili wafurahie huduma zetu, maongezi mazuri ya lugha kwa wateja wapya na wazamani ili wote kuwa fanya wajisikie vizuri kuhudumiwa nasi siku zote,hawa wapya watamani kuendelea kupata huduma zetu kama hao wa zamani.

Mfano: mteja anaweza lalamika kuwa chakula ni kidogo ukichukua sahani yake nakwenda nayo jikoni hata bila kuongeza uka mrudishia ana amini ume muongeza hivyo nafsi yake ina furahia hilo badala ya kugombana kwa maneno kuwa vitu vime panda bei.
Ikiwa uta penda kufanya kazi namimi mkoa wowote nakuja na unaweza kunipa mwezi mmoja tu wa majaribio ili uone ukweli wa haya nnayo ongea yapo ama la ,au ukanifanyia interview kujua zaidi kuhusu uwezo wangu Katika hizo kazi.Number yangu 0684601370
 
Back
Top Bottom