Naomba Kamati ya Taifa Stars hii ya Makonda baada ya Mechi ya Jumapili igeuke iwe Kamati ya saidia TANESCO Dar

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,545
108,861
Kama kuna Taasisi ambayo kwa sasa nikiri wazi wazi hapa Jamvini kuwa inanikera na endapo nami ningepata tu angalau Mafunzo ‘ Kiduchu ‘ ya Kigaidi kutoka Kwake aliyekuwa Mtaalam na Bingwa wa Ugaidi duniani Marehemu Osama Bin Laden ningeanza nayo kwa ‘ Kuilipua ‘ nap engine hata kumlipua Mhusika wake Kimamlaka basi ni TANESCO.

Haiwezekani na inakera sana kwani Umeme unakatwa ‘ Kiholelaholela ‘ tupu kama siyo ‘ Kipopoma ‘ kabisa na kinachoniuma zaidi GENTAMYCINE ni kwamba huwa hakuna hata taarifa yoyote ya awali ambayo Sisi Wateja Wao huwa wanatuambia ili nasi tujiandae. Kwakweli TANESCO mnatutesa vilivyo Wanakazi wa Mkoa huu wa Dar es Salaam kwa hii Kata Kata yenu ambayo huwa haina muda.

Hivyo basi namwomba mwenye Mkoa wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye kwa sasa yupo ‘ busy ‘ na Timu ya Taifa ya Tanzania ( Taifa Stars ) inayojiandaa na Mchezo wake Siku ya Jumapili kwamba baada ya huo Mchezo basi tunamuomba Yeye na hiyo Kamati yake watusaidie Sisi Wakazi wa Dar es Salaam tuwe na Umeme wa uhakika au Wao ( Kamati hiyo ) ndiyo wawe wasimamizi Wakuu wa TANESCO kwani naamini hawatashindwa Kitu na Umeme Kukatikakatika itakuwa sasa ni Historia.

Inaudhi na Kukera mno tu kwani ukijirudia zako mchana kutoka Mihangaikoni na kutaka ujifariji na Feni yako hasa ikijulikana kwa sasa Dar es Salaam Joto limeshika Kasi huku ukiwa umejilaza zako TANESCO wanakata Umeme ghafla haya hujakaa sawa tena Usiku unamsadia GENTAMYCINE Junior na ' Homework ' zake TANESCO wanakata Umeme mara tena umeshikwa zako na Haja Kubwa hivyo umeenda zako Msalani / Chooni / Maliwatoni unaanza tu Kujisaidia zako huku ukituuliza Akili yako na Kutafari Maisha yalivyo mara ghafla TANESCO tena wanafanya yao ( wanakata Umeme ) matokeo yake hata Rada yako ya Ubongo ilipokuelekeza ushushe Mzigo wako ( Nnya ) inapotea na matokeo yake unashushia pembeni na hapo bado kuna Zoezi la Kunawa Mikono gizani bado linakusubiri.

Naomba Kuuliza hivi TANESCO Sisi Wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam tumewakoseeni nini? Kwanini mnatutesa hivi kwa Kutukatia hovyo na mara kwa mara Umeme hadi mnatuunguzia Mali zetu na kuturudisha tena katika Umasikini tunaojaribu Kuukimbia? Halafu Wewe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Makonda na huyo Waziri husika Kalemani hivi hizi Lawama na Kero za TANESCO hamzipati? Hivi kwa ' Upuuzi ' huu unaofanywa na TANESCO Watanzania wakikerwa na Serikali yao ambayo ipo chini ya CCM na wakamchukia hadi Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli watakuwa wanakosea au mtawalaumu?

Ukiona hadi GENTAMYCINE naandika Kitu cha namna hii jua yamenifika na nimekera sana tu. TANESCO mjirekebishe upesi,

Nawasilisha.
 
*SABABU ZINAZOWEZA KUSABABISHA KUKATIKA KWA UMEME*

*1. Utangulizi*
Kwa muda mrefu kumekuwa na uelewa kutoka kwa wateja wetu kuwa kila umeme unapokatika TANESCO WAMEKATA. Nimeona ni vyema tukatoa
Maelezo kwa ufupi ili wateja wetu waelewe sababu za kiufundi na zisizo za kiufundi, zilizo ndani ya uwezo wa TANESCO na zisizo ndani ya uwezo wa TANESCO.

*2. Sababu za TANESCO Kukata Umeme*

TANESCO itakata tu umeme endapo kuna sababu zifuatazo *BILA* kuwataarifu wateja:-
a) Kuna mali inaungua (Mf. nyumba, kiwanda au mtambo)
b) Kuna mtu kanaswa na umeme.
c) Dharura _emergencies_ (imeelezwa hapo chini namba 4)

*3. TANESCO itakata umeme baada ya kuwataarifu wateja - _Planned Interruptions_ endapo:-*

a) Kuna matengenezo Kinga yaliyopangwa kufanyika ili kuimarisha miundombinu _Planned Preventive Maintanance_ (Mf. Kubadili nguzo zilizooza, kubadili waya chakavu, kubadili transfoma ili kuongeza uwezo wa umeme nk)
b) Matengenezo ya kila mara _Routine Maintanance_ (Mf. Kukata miti inayogusa line za umeme, kukagua vikombe na vifaa vingine kwenye line)
c) Kumuunga mteja mkubwa kwenye line ya msongo mkubwa wa umeme 11kV au 33kV

*4. SABABU zinazoweza kusababisha umeme kukatika kwa dharura _Emergency cases_* nyingi ni Unplanned Interruptions

a) Za kiasilia _Natural Calamities_ (Mf. Radi kupiga transfoma, mvua au upepo mkali kuangusha nguzo, kukata waya, miti au minazi au matawi ya miti kuangukia line, mafuriko, wanyama kama komba, nyani, nyoka, kunguru kunasa kwenye mifumo ya umeme nk.

b) Hujuma za kibinadamu _Sarbotage_
(Mf. Transfoma kuibiwa mafuta, kuibwa nyaya za umeme, nguzo kuchomwa moto na kuanguka, nguzo kubwa kuibiwa vyuma na kuanguka, magari kugonga nguzo za umeme na kuanguka, malori marefu kwenda juu kukata waya za umeme, wateja kukata miti ikaangukia kwenye line nk.

Hizi ni baadhi tu ya sababu za msingi zinazoweza kusababisha umeme Kukatika. Hivyo ieleweke kuwa sio kila KUKATIKA KWA UMEME -TANESCO wamekata ni suala pana linalohitaji kujua sababu. Wakati mwingine kwa maelezo hayo hapo juu, Umeme unakatika hata TANESCO inabidi kufuatilia mifumo ili kujua sababu za kukatika.

*5. Hitimisho*
Tunajua jukumu la TANESCO ni kuhakikisha wateja wanapata umeme wa uhakika, pia ni ukweli kuwa mifumo mingi ya TANESCO ni ya muda mrefu hivyo inahitaji ukaratabati wa mara kwa mara na uwekezaji mkubwa ambao sote tumeona jitihada zinazofanywa na Serikali ili TANZANIA iwe na umeme wa uhakika.

Tunaomba umma uelewe sababu hizi na kuwa kama viongozi tunaamini hakuna mfanyakazi wa TANESCO anaweza kulihujumu Shirika kwa kukata umeme bila sababu au kukata umeme bila kufuata maagizo na utaratibu wa kukata line uliowekwa. Sio kila mfanyakazi au fundi anaweza kukata umeme. Upo utaratibu tena wakati mwingine wa kimaandishi unaompa fundi ruhusa, kabla ya kukata umeme. Kama yupo na anafahamika ( _Kama baadhi ya wateja wetu wanavyotuhumu_) tunaomba ushirikiano wenu ili tuweze kumshughulikia kwa taratibu za kisheria na tutakuwa tumelisaidia Shirika na serikali kwa ujumla.

TANESCO
_*Tunayaangaza Maisha Yako*_
 
Back
Top Bottom