Tabutupu
JF-Expert Member
- Nov 26, 2010
- 13,107
- 18,323
Jamani kwa wale mlio katika ndoa na wote wawili mnafanya kazi.
Mnafanyaje katika kuchangia budget ya familia yenu na kutatua matatizo ya familia zenu mliko toka bila upande mmoja kulalamika au kujihisi upande mmoja ndo unapendelewa. Samahani familia zenu mliko toka hazihusiki sana lakini kwa mazingira mengi ya Tanzania bado zinahitaji msaada kutoka pande zote mbili.
Kuna wengine eti kwa kuwa katoa mahali basi mwanamke haruhusiwi kujihusiha na familia yake aliko toka. Na je nalo hili lipoje.