Naomba elimu na ushauri kuhusu kalenda yangu, baada ya kunywa emergency pills

Lis

JF-Expert Member
Jun 2, 2012
471
345
Heshima kwenu doctors, naomba kuelimishwa juu ya hili tafadhali:-

Binafsi Nina mzunguko wa siku 27 wa hedhi, ninautumia kujua siku zangu za hatari na salama.
Lakini mwezi huu ilitokea nikafanya katika siku ya hatari, na ikanibidi ninywe emergency pills, sikuwa na jinsi.

Swali langu ni je, naweza kuendelea kufuatilia kalenda yangu kwa ajili ya kujua siku salama na hatari?au baada ya kunywa hizo pills, ndo nimeharibu mzunguko wangu siwezi kujua danger and safe days?

Kama munguko wangu utakuwa hauleweki nifanye ili nirekebishe mzunguko wangu uwe sawa?

Thanks.
 
Emergence pills like P2 one of side effects ni kubadili mzunguko wa hedhi. Itachukua muda kurekebika kwa mzunguko ikitegemea na stability ya hormones zako.

NB: kama huna plan ya kuzaa watch out as danger days hubadilika badilika!
 
So hapo huwezi kufuata kalenda no lazima condom itumike tu? Au nitajua vipi danger days?
 
Kwa ninavyojua mzunguko utabadilika so kama huwa unanote kwenye calendar siku zitabadilika na inawezekana hata mzunguko ukapungua ama kuongezeka... hautaweza kufuata calendar ya siku zote.

Mara nyingi mzunguko unakaa sawa(kama utakaa sawa kama mwanzo) baada ya miezi mitatu.
 
Hakikisha unakunywa maziwa na maji mengi kupunguza madhara ya hiyo sumu uliokunywa.
Nje ya mada, unamiaka mingapi mkuu?
 
Unaweza lakini ukiona kuna mabadiliko usipaniki vumilia mpaka mwezi ujao itakaa sawa
Mkuu nimerudi kuuliza Tena, coz nimepata hedhi mapema kabla ya tarehe zangu, lakini kinachoniogopesha Ni damu chache Sana, kiasi kwamba siku ya Kwanza at least ilitoka kiasi Cha kujaa pedi moja, siku ya pili ilikuwa chache zaidi, na siku ya tatu Ni vitone tu, je hi inaweza kuwa Ni moja ya effects za P2? Au ndo nishanasa tayari?
 
Lea yeyote mwenye uelewa na hili tafadhali naomba kuelimishwa
 
Back
Top Bottom