Fahamu kuhusu Kilimo cha Strawberries

Kuna Mada humu inaelezea hizi kwamba DAR hazikubali,kuna ukanda wake maalum
Na ndio maana Arusha huko wanalima sana,sijui hazihitaji Joto
 
Aiseeeee izo mbegu kenya, south africa hukosi tafuta kampuni kubwa za mbegu ongea nao wakuagizie alafu icho nikilimo cha green house ukilima kiholela utapata kitu
 
Salamu sana Wakuu katika Jukwaa hili.

Leo nimepanda hapa Jukwaani nikiwa nahitaji msaada kutoka kwenu. Naomba kujuzwa Juu ya zao hili la Strawberry, nimepata kusikia kwamba kuna baadhi ya Maeneo ambayo zao hili hukubali na maeneo hayo ni kama Vile Iringa,Morogoro, Kilimanjaro, Arusha na Tanga na mimi naishi Kilimanjaro Hivyo ningependa kujaribu kilimo Hichi na panaponikwaza ni wapi Nitapata Mbegu ama miche. Tafadhali naomba kwa yeyote anaeweza Kunipatia mahali nitakapoweza kununua/kupata miche hii tuwasiliane na pia kwa yeyote mwenye Ujuzi katika Kilimo cha zao hili nae anipe maufundi hapa hapa Jukwaani ili na wengine wajue.

Natanguliza Shukrani zangu za Dhati.
 
Nenda Peramiho Songea mkoa wa Ruvuma. Kuna wakulima wadogo wa zao hilo. Ukifika mjini Songea, panda basi dogo pale stendi ya mjini linaloenda Peramiho; litashika barabara iendayo Mbinga, halafu gari litachepuka kuelekea Peramiho baada kutembea kama kilometa 25 hivi; sina uhakika sana wa umbali huo. Likisha chepuka utaenda kama kilomita moja utavuka mto mdogo. Baada ya hapo utaenda mbele kama mita 20 kushoto utaona kibao kikionesha wakulima wa zao hilo. Wanalima kwa miaka mingi. Unaweza kupata uzoefu wao katika shughuli hiyo huko. Ninakutakia kila la kheri. Asante.
 
Kama ukienda Singida ukipita manyoni kuna jamaa alikuwa analima anauza nje sijui alikuwa anapata wapi mbegu hata mi nataka ni zao lenye pesa sana
Yeah last week nliiona mshkaji kanunua gram 500 kwa shiling 10000 za kitanzania so what am I waiting????
 
Bado maelezo hayatoshi, sijui watanzania kwa nini tuna kosa information, Shukrani kwa wadau mliotuelekeza peramiho na singida, ngoja niendelee kutafuta information
 
Strawberry ni moja ya matunda luxury sana ambao mara nyingi sana hulimwa kwa ajili ya ku export nje.

Ila siku za hivi karibun kwa sababu ua kuku wa Middle class na muingiliano na wageni basi utamaduni wa kuyala umekuwa ni mkubwa sana miongoni mwa jamii.

AINA YA STRAWBERRY

Aina kuu ni Fragaria genus.

Na hapo kwenye Fragaria genus utakutana na;

1. Chandler,
2. Domanil
3. pajaro
4. Douglas
5.Tioga selva
6. Rabunda
7.Tri-Star
8.Tribute

Kila aima ina sifa zake nzuri na mbaya zake pia na ziko za ukanda wa joto sa a na ukanda wa Baridi sana.


MATUMIZI

Strawberry ina matumizi mengi sana nitataja machache.

1. Kutengenezea Icecream- Mahoteli makubwa huanunua kwa ajili hiyo ya Icecream.

2. Ftesh Juice- Wanunuzi ni Mahoteli na majumbani.

3. Processed Juice- Hii ni juice iliyo packiwa

4. Yogurt- Viwanda vya kusindika maziwa wanatumia sana na ndo wanunuzi wakuu wa haya matunda.

5. Watengeneza keki- Kudecorate keki

6.Decoration kama maua ya kupamboa ukumbini.

7. Manukato

8. Kuliwa kama Freshi fruit

9. Jam

10.Sauces

13. Madawa na kadhalika.

Strawberry inapenda sana maji kiasi kwamba kama maji ni ya kutafuta kwa tochi basi usijaribu kulima hii kitu.

MBEGU

Strawberry huoteshwa miche yaani yenyewe hutoa miche ambayo huogwa runner na hizo runner huoteshwa tena.

KULIMA
Inakubali maeneo mengi sana isipokuwa maeneo yenye joto kari make haizwezi himili joto la zaidi ya 30c.

SOKO LAKE

Soko lake lipo ila mtu akiamua kutengeneza Jam mwenyewe au Ice cre basi anaweza pata pesa ziadi ya mara 4 ambayo angepata kama angeuza matunda.

0c9dae5d3d1b822feafe1717adddbef7.jpg


447516f03ac6e31783307fc7b6e717ad.jpg
 
Safi sana, umenipa idea ya kumpa mtu zawadi, anapenda sana kipimo cha kwenye containers kama hilo box hapo.
 
Back
Top Bottom