Naomba design za nyumba jamani!

Mbeba Maono

Senior Member
Jun 24, 2008
108
7
Jamanieee, samahanini, pamoja na kwamba nitakuwa naiba haki miliki ya watu, naombeni kama kuna mtu mwenye ramani za kujenga nyumba, yaani design za nyumba, muwe mnatuwekea hapa tuweze kudownload ili tujenge nyumba zetu nzuri. kama kuna mtu anayeweza akatuwekea hapa aina ambazo zitatufaa kwa weather ya hapa tz, nitashukuru. asanteni.
 
.... natumaini watakusaidia wachora ramani tulionao hapa jf, as long as lengo siyo kuporomosha majengo ya ghorofa 10 kwa gharama za shs. millioni 300 tu!!
 
Asante mkuu. unafikiri naweza kuzipata hapa kwenye website? nitype nini ili ni download mwenyewe? Ni nyumba za kuishi za watu wa hali ya katu mzee, yaani middle class people. sio magorofa.
 
.... aina ambazo zitatufaa kwa weather ya hapa tz, nitashukuru. asanteni.

...challenge iliyopo na architect wako, ni mchoro na kujenga nyumba ambayo haitakuwa na corridor ndeeeefu/nyingi ambazo matokeo yake ni joto, kiza na mbu.

Ni maoni yangu tu.
 
Jamanieee, samahanini, pamoja na kwamba nitakuwa naiba haki miliki ya watu, naombeni kama kuna mtu mwenye ramani za kujenga nyumba, yaani design za nyumba, muwe mnatuwekea hapa tuweze kudownload ili tujenge nyumba zetu nzuri. kama kuna mtu anayeweza akatuwekea hapa aina ambazo zitatufaa kwa weather ya hapa tz, nitashukuru. asanteni.

Unajua kuwa utakuwa unafanya ufisadi lakini unapwaga tu!

Ushauri wangu tembelea ofisi za ma architects bongo ( wasiliana na Architects and Quantity Surveyors Registration Board kwa orodha yao), ongea nao, angalia kazi zao, ongea na wateja wao halafu chagua atakayekufaa. Huyo utakayemchagua, kaa naye umweleze mahitaji yako, mpeleke kwenye kiwanja na muhimu sana bajeti yako (ijumuishe malipo yake kwa ajili ya design na kusimamia ujenzi). mkishakubaliana yote haya ingia naye mkataba utakaoweka wazi malipo yake na kukulinda wewe kama yatakuja tokea matatizo mbele ya safari. Uwe tayari kuchukua hata zaidi ya mwaka kupata ramani inayokufaa. Usiogope kukataa ramani ambayo haikidhi mahitaji yako lakini msikilize anapokupa ushauri wa kitaalamu. Hizo ramani za kwenye mawebsite si za mazingira yetu na mara nyingi zimelipuliwa. Za NHC, unfortunately, are no better. Kumbuka kuwa kwa wengi wetu nyumba ni the largest investment utakayoifanya maishani mwako kwa hiyo inastahili uangalizi mkubwa. Dezo zina hasara zake kama tulivyoshuhudia hivi karibuni.

Kila la heri.
 
You Need To Pay Professional Fees By The Way. However, You Cap Prepare Your Own Sketch And Give It To Architect, Naye Atakupa Ushauri Muafaka
 
Jamanieee, samahanini, pamoja na kwamba nitakuwa naiba haki miliki ya watu, naombeni kama kuna mtu mwenye ramani za kujenga nyumba, yaani design za nyumba, muwe mnatuwekea hapa tuweze kudownload ili tujenge nyumba zetu nzuri. kama kuna mtu anayeweza akatuwekea hapa aina ambazo zitatufaa kwa weather ya hapa tz, nitashukuru. asanteni.

Ndugu yangu Mbeba Maono,

Kama walivyoshauri watu wengine, nitaongezea kwa kusema kuwa ni vigumu kupata nyumba inayoweza kukidhi matakwa yako kwenye internet.

Kuna vigezo vingi vya kuzingatia kabla hujapata nyumba inayokidhi matakwa yako. Baadhi ni hivi hapa:

Sehemu ambayo kiwanja chako kipo:
Kwa mfano ramani ya nyumba inayotakiwa Sinza ambako tayari nyumba zingine zimejengwa na huna nafasi ya parking na fensi haiwezi kufanana na ile itakayofaa Boko ambako una eneo la kumwaga.

Kiasi cha hela ulizo nazo.
Uwezo wako pia unachangia kujua aina ya nyumba inayokidhi matakwa yako.

Mazingira ya kiwanja chako,
kama kipo mlimani, tambalale, au kwenye mpomoromoko, au kwenye ardhi ngumu au kwenye majimaji kama Jangwani, sababu hizi zitachangia aina ya design ya nyumba inayokufaa. Kuna viwanja msingi tu unaweza ukala hela zako zote ulizonazo.

Hizi ni baadhi ya sababu chache zinazosababisha nyumba zisifanane, ukichunguza sana hata maghorofa yetu yanayoanguka unaweza ukakuta ni kwa sababu wahusika hawakuweza kufanya utafiti wa kutosha wa aina ya nyumba inayofaa kwenye kiwanja husika.

Ukitaka usaidiwe zaidi weka maelezo kamili ya kiwanja chako hapa pamoja na picha yake nina imani JF inakila aina ya watu including clazy architects ambao wanaweza kukusaidia, (though I am not sure if somebody can offer his service at free of charge, anyway try your lucky) kama uko Dar basi kama walivyoshauri wengine nenda kwenye Board of QS & Architects utasaidiwa zaidi.

Lakini ile tabia ya kusema hii ramani ninaipenda na ndio hii inanifaa inaweza isifae kwenye mazingira ya kiwanja chako. Hebu tubadilike na tujenge tabia ya kuwatumia watalaam wetu tuliowasomesha kwa pesa za wakulima na wafanyakazi. Ukipata ramani inayokufaa wasiliana na mimi nikupe gharama ya nyumba yako; However, consultancy will be at cost.

Nsaliwe Njimba
Construction Economist.
 
How to get a bulding working drawings at a low cost?
Wapo ma-architects wanao-copy kazi waliyofanya kwa mteja mmoja na kufanya few modifications kumtengenezea mteja mwingine. Hii inanipa picha kwamba hata mtu mwenye kipato kidogo angeweza kumtumia architect kwa bei atakayomudu.

What kind of pricing plans architects have/use?

.
 
Ni kweli kuna website zina offer michoro ya bure. Lakini siku zote ujue mazingira ilipo nyumba iliyo na mchoro kwenye internet ni tofauti na ya kwetu. Kama hata ukiona mchoro unaokufurahisha katika internet wewe jaribu kuuchukua na kumuonyesha archtecture wa hapo Bongo na yeye atakupa ushauri mzuri zaidi.
Nyumba inahitaji uangalifu mkubwa kama alivyokushauri Fundi Mchundo. Ni life time investment. Ukiifanyia mchezo ina render regrets baadaye.
 
Unajua kuwa utakuwa unafanya ufisadi lakini unapwaga tu!

Ushauri wangu tembelea ofisi za ma architects bongo ( wasiliana na Architects and Quantity Surveyors Registration Board kwa orodha yao), ongea nao, angalia kazi zao, ongea na wateja wao halafu chagua atakayekufaa. Huyo utakayemchagua, kaa naye umweleze mahitaji yako, mpeleke kwenye kiwanja na muhimu sana bajeti yako (ijumuishe malipo yake kwa ajili ya design na kusimamia ujenzi). mkishakubaliana yote haya ingia naye mkataba utakaoweka wazi malipo yake na kukulinda wewe kama yatakuja tokea matatizo mbele ya safari. Uwe tayari kuchukua hata zaidi ya mwaka kupata ramani inayokufaa. Usiogope kukataa ramani ambayo haikidhi mahitaji yako lakini msikilize anapokupa ushauri wa kitaalamu. Hizo ramani za kwenye mawebsite si za mazingira yetu na mara nyingi zimelipuliwa. Za NHC, unfortunately, are no better. Kumbuka kuwa kwa wengi wetu nyumba ni the largest investment utakayoifanya maishani mwako kwa hiyo inastahili uangalizi mkubwa. Dezo zina hasara zake kama tulivyoshuhudia hivi karibuni.

Kila la heri.

Good advise Mchundo!!!! Rahisi ni aghali sometimes...
 
Ni kweli kuna website zina offer michoro ya bure. Lakini siku zote ujue mazingira ilipo nyumba iliyo na mchoro kwenye internet ni tofauti na ya kwetu. Kama hata ukiona mchoro unaokufurahisha katika internet wewe jaribu kuuchukua na kumuonyesha archtecture wa hapo Bongo na yeye atakupa ushauri mzuri zaidi.
Nyumba inahitaji uangalifu mkubwa kama alivyokushauri Fundi Mchundo. Ni life time investment. Ukiifanyia mchezo ina render regrets baadaye.

...ushauri mzuri, kwani hizo websites zinakupa idea tu, hazina vipimo vyote...vile vile kwa wanaosema hazikubaliani na mazingira ya kwetu mkipata nafasi nawashauri m search zaidi humo, utagundua kuna sunbelt houseplans, mediterranean houseplans etc, ideas zinakupa changamoto ya kujifunza kuliko tabia ya 'kufunga milango' ya ufahamu.

tafuta mchoro unaoupenda wewe, mchoraji akushauri na akuchoree, kisha mjenzi akujengee, badala ya kutafutiwa mchoro, au hao ma architect wakuchagulie mchoro. Nyumba ni yako kaka.
 
Sikio la kufa kweli halisikii dawa. Hizo unazozitaja ni namna nyumba zilivyo na si kuwa zinashahibiana na mazingira ya kwetu. Ukisikia mediterranean mara nyingi ni za vigae na kuta zimepakwa chokaa! Pamoja na hayo wapi kweli kuna hali ya hewa ya mediterranean?

Tunaposema mazingira ni lazima uelewe si hali ya hewa tu bali ni jinsi tunavyotumia nyumba. Namna mgeni anavyopekelewa na unyeti wa vyumba tofauti unategemea culture ya watu. Kwa wenzetu vyumba vya kulala viko wazi kwa kila mtu wakati kwetu sisi chumba cha wazazi ni mwiko! Kwa wenzetu jiko ni sehemu ya sebule wakati sisi hatutaki mgeni aone mama alivyokaa akikuna nazi. Bado hujaweka imani kuwa wali lazima ufunikiwe mkaa! Au maharage hayapikiwi kwenye jiko la umeme. Aliyetayarisha ramani hizo hawezi kujua kuwa unategemea mama mkwe atakuja kukaa na nyie wakati wa utu uzima wake! na vitu vingine vingi. Bado hatujaweka namna ya ujenzi. Sisi tunatumia matofali ya zege wakati wenzetu wanatumia mbao, matofali ya udongo, mawe n.k. Kwa nini usikae na mtaalam akakushauri badala ya kukimbilia michoro ya nyumba za Aspen? Chukua muda kutafuta anayeendana na mtazamo wako. Kaa nae, mweleze ndoto zako, bishana nae na kitakachotoka kitakuwa ni chako!

Ila kama unataka kujenga kwa ajili ya kulangua, hilo no suala lingine!
 
Nakubaliana na mchongoma katika hili......si vibaya kupata different ideas........then unai-transform the way you would like it to be....ukimshirikisha architect ofcourse
 
:D

...Fundi Mchundo, basi yaishe basi kaka. Mimi na chaguo langu nawe una lako. Huwa napenda kutofautiana kwa kujadiliana bila kuhamakiana.

Shukran kaka.

Mchongoma!
Nimehamaki kwa sababu watu wengi wana msimamo kama
wa kwako. Ndiyo maana ukaona ushauri wetu ni 'kufunga milango' ya ufahamu. Hauoni, kama ambavyo wengi hawaoni, ubaya wa kuchukua michoro kwenye intanet na kuitumia. Aliyeanzisha mada alikiri kuwa anajua kuwa ni kosa kufanya hivyo lakini akaendelea kuomba awekewe michoro ili aweze ku'download'! To add salt to injury unamshauri kuwa baada ya kudownload au kupata hiyo michoro kwa njia nyingine atafute MCHORAJI (bila shaka huyu atakuwa Fundi Mchundo mwingine) atakaye tayarisha michoro kutokana nayo. Ukamalizia kwa kusisitiza kuwa asikubali watu wamtafutie michoro au hao ma architects wamchagulie mchoro! Nyumba si ya kwake. Hapa ndipo nikaona nyekundu maana huu ushauri wako ndiyo unaotumiwa na wengi wa wale wanaoporomosha majengo Kariakoo. Wanatoa michoro Dubai au kwa ankal, wanatafuta mchoraji halafu wanampa architect mwenye njaa apige mhuri kwa ajili ya kibali. Athari zake wote tumeziona. Na nyingine nyingi tutaziona.

Inaelekea, Mkuu, unaamini kuwa michoro yote imeshachorwa na hao ma architect kazi yao ni kufungua madawati na kukuchagulia! Hali sio hivyo.
Hivi mbona ukienda kwa daktari hauendi na sampuli za madawa uliyoyatoa katika mtandao na kumwambia akushauri ipi ni nafuu katika hizo? Si mwili wako? Kwa nini unakubali kuendeshwa na daktari?

Nakiri kuwa ma architects wenyewe wamechangia kwa kiasi kikubwa kuweko kwa imani hii potovu. Kutokana na uvivu wa kufikiri wengi hufanya hivyo, kumwonyesha mshitiri sampuli za ramani ambazo anaweza kuchagua. Sasa kama hali ndiyo hivyo, si ajabu basi mtu akimtafuta mchoraji anayemsaidia huyo architect amvutie mchoro kwa bei poa. Lakini upungufu huu hauondoi ukweli kuwa kazi ya architect ni kubuni na anatakiwa aanaglie best interest za client. ndiyo maana alienda shule. Ndiyo maana analipwa. Ni wajibu wa mshitiri kuhakikisha huyo aliyempa dhamana ya kutumia life savings zake anafanya hivyo kwa uwezo wake wote. Si kumlipulia.
 
Jaribu Search Engines Kama Google, Yahoo Au Jeeves

Mimi Nilipata Huko Na Nikaweza Kufanya Little Modifications And I Am Happy
 
Back
Top Bottom