Naomba connection kupata suppliers kutoka Dubai

Habarini ndugu.

Nimekuwa nikiagiza vitu mara kadhaa kutoka China hasa kwa kutumia Alibaba, 1688 na Taobao.

Ila kwa sasa nahitaji kupata connection pia ya namna ya kupata suppliers wa kutoka Dubai, kwa hivyo ndugu zangu, naomba yeyote mwenye connection anipe ABC za namna ya kutimiza jambo hili.

Natanguliza shukrani zangu kwenu.
Mkuu naona nakutumia sms dm naona nashindwa. Nichek kwa kujua mengine zaidi kaka.
 
Kuagiza kutoka Alibaba, kwanza unafungua account Alibaba, kisha unatafuta bidhaa unazohitaji, baada ya hapo unachat na supplier husika, ambapo utamwelekeza akufikishie bidhaa yako kwa kampuni zinazo safirisha kuleta Tanzania, ambapo mimi huwa nawapa address ya Silent Ocean iliyoko China (ukiingia Insta kwenye page ya silent ocean huwa wanaweka address yao ya China utaipata huko), kisha utamwambia akutengenezee order, then utabonyeza sehemu ya order utafanya malipo kwa VISA CARD AU MASTER CARD. (Pia zingatia kumwambia supplier wako aandike jina lako na namba yako ya simu kwenye mzigo).

Baada ya kufanya malipo, utamwambie akupe tracking number ambayo kupitia hiyo utaona kama mzigo wako umewafikia Silent Ocean kwenye ofisi zao za China.

Then, kama umefika, download app ya silent Ocean play store halafu utaweza kuingiza namba yako ya simu ya kujua siku ambayo mzigo utafika Tanzania, pamoja na gharama za usafiri kutoka China to TZ ambazo utalipia mzigo utakapofika.

ZINGATIA
Unapochagua supplier angalia mambo yafuatayo
1. Amekuwa verified? Kama hapana je, ni Gold supplier?
2. Je account yake ina miaka mingapi?
3. Je, walio nunua kwake wame_comment nini kuhusu bidhaa zake na uaminifu wake?
4. Je, amepata rank gani kwenye rate? 1 ni mbaya zaidi na 5 ni nzuri zaidi
Muhimu: Hakikisha malipo yote yanafanyika kwa kutumia Alibaba, kataa kabisa akitaka umlipe kwa njia nyingine nje ya Alibaba utalizwa.

Hivyo vigezo hapo juu ni kwa mujibu wa uzoefu wangu wa kutumia Alibaba kuagiza mizigo.

Sorry, najijua sina uwezo mzuri wa kuwasilisha ujumbe kwa maandishi, ikiwa una swali nitakujibu

NB: japo si kwa umuhimu, nimetoa mfano wa kusafirisha kwa kutumia kampuni ya Silent Ocean kwa kuwa ndio ambao nimekuwa nawatuma mara kwa mara, sina uzoefu na wasafirishaji wengine.

lakini bado nasubiri connection ya Dubai
Mkuu Silentocean wanatumia muda gani mzigo kufika Tanzania?
 
Nishawahi ila sio kibiashara ilikuwa project tu kwenye kampuni moja hivi maeneo ya ras al khaima

Kwanini usingelienda mwenyewe ukatengeneza connection nzuri halafu ndio ukatulia ukawa unaagiza,? kwa tumia ma agent moja kwa moja kununua mizigo kwa maduka ambayo hujwahi kuenda unaweza kupigwa cha juu bila ya kuelewa mkuu, unless uwe una deal direct na kiwanda hapo haina shaka yoyote.
 
Kwanini usingelienda mwenyewe ukatengeneza connection nzuri halafu ndio ukatulia ukawa unaagiza,? kwa tumia ma agent moja kwa moja kununua mizigo kwa maduka ambayo hujwahi kuenda unaweza kupigwa cha juu bila ya kuelewa mkuu, unless uwe una deal direct na kiwanda hapo haina shaka yoyote.
Mkuu hela yangu nahisi haitoshi kwenda huko 8M inatosha kama mtaji kwa kuanzia maana sina uzoefu
 
Back
Top Bottom