Naomba CDM itawale nchi hii ya Tz/Tanganyika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naomba CDM itawale nchi hii ya Tz/Tanganyika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwiba, Jul 11, 2012.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Jul 11, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Uongozi au utawala si lelemama WaTanganyika wengi wanawekeza matumaini yai katika Chadema ,naombea sana Chama hiki kipate kuiongoza Tanzania hapo 2015 au hata kabla kwa mambo yanavyokwenda.

  Chadema ielewe kwamba mambo haya yaliyozuka hayatasimama yanaota na kuwa makubwa kama mbuyu ,natangulia kussema kuwa migomo haitosimama kila kona itaomba iwe na mishahara minono ,imani ya wananchi ni kuwa tutaishi kwa salama na amani bila ya kunyanyaswa na vyombo vya dola au majambazi wakiwemo vibaka wa mitaani kwani nao ni kero kubwa kuliko hata hao mafisadi

  Matumaini yanayojengwa na Chadema mbele ya macho ya wananchi ni kuwepo kwa utawala wa sheria usiojali cheo cha mtu kwa maana watu wote watakuwa chini ya sheria ,sheria itatawala kwa uwazi kabisa.

  Vinginevyo niseme mambo yatawageukia in a short period of time ikiwa mwananchi ataanza kuvunja matumaini kuwa maisha yake yamekombolewa ,hii itatokana na speed watakayoingia nayo CDM na vipi wataweza kuonesha mafanikio ndani ya muda mfupi zikiwemo siku mia za mwanzo na pia vipi wataweza kuonyesha ule moyo wa kuwakamata mafisadi bila ya kuwaonea huruma au kuwaonea haya ,kwa maana yale ya kulindana yatakuwa hayana nafasi tena baina yao ,kwa maana mambo yawe ya kutovumiliana baina yao panapotokea uzembe na itikadi hiyo ifike hadi ngazi za chini.
   
 2. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #2
  Jul 11, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Tunatawala mkuu ikulu ni kijiwe rais wa ukweli yupo mioyoni mwetu sio yule wa ikulu.
   
 3. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #3
  Jul 11, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Mbona unajipiga mitama sana!!. Kwa bahati nzuri sana CDM haina watawala kama ilivyo ccm, CDM ina VIONGOZI wa wananchi. Viva CDM, to HELL with ccm
   
 4. KALYOVATIPI

  KALYOVATIPI JF-Expert Member

  #4
  Jul 11, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,419
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  Chadema watakuja kutuongoza sio kututawala kama wanavyo tutawala ccm. kiongozi wa kweli ni yule asiye muoga wa kutumia sheria kuwatumikia watu wake na wala sheria aiangalii sura,pesa,umri,madaraka au jinsia ccm wamelishindwa hilo kwa miaka 5o watuachie tuipeleke tz pale watz wanataka kuwa
   
Loading...