Naomba CCM ishinde kwa 100% Eee Mungu nisaidie na nisamehe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naomba CCM ishinde kwa 100% Eee Mungu nisaidie na nisamehe

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Albedo, Jul 11, 2010.

 1. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #1
  Jul 11, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Tanzania ilirejea katika mfumo wa Vyama vingi vya Siasa mnamo mwaka 1992, toka kipindi hicho tumeshuhudia Chaguzi tatu 1995, 2000, 2005 na mwezi October 2010 tunatarajia kufanya Uchaguzi wa nne utakaoshirikisha Vyama vingi vya Siasa.

  Toka Mfumo huo uanzishwe tumeshuhudia juhudi kubwa zikifanywa na Wapinzani japo kwa Uchache wao Bungeni katika kuivua Nguo Serikali na Kuilazimisha wakati mwingine kufanya kile ambacho isingependa kukifanya kwa Hiari yake.

  Tumeshuhudia namna Wapinzani walivyoichachafya Serikali ya CCM katika Masuala ya Buzwagi, Meremeta, Mwananchi Gold, Dowans, Richmond na mengine mengi ambayo kabla ya hapo hakuna Mbunge wa CCM aliyekuwa na Ujasiri hata wa Kuyazungumzia hata hakiwa Chumbani na Mke/Mume wake achilia Mbali Bungeni. Ujasiri huu wa Upinzani uliifanya CCM kuwaruhusu ( Nimetumia neno Kuruhusu Makusudi najua litaibua Mjadala) Baadhi ya Makada wake kupiga Kelele aka kupiga Porojo ( Kwa sabau walijua wananchi wanapenda Mavuvuzela) lakini kwenye maamuzi waliishia Kunywea kama Kuku aliyona Mwewe.

  Pamoja na Mfumo usio huru wa Uchaguzi na hata wa Media Coverage Wapinzani wameendelea kuamini kwamba siku moja kitaeleweka tu.

  Pamoja na Wapinzani kuzunguka kila kijiji kueleza Uoza wa Chama cha Mapinduzi bado wameendelea kupata kura kiduchu katika Chaguzi kuu na hata zile Chaguzi Ndogo.

  Pamoja na Watanzania wengi kuenedelea kuwa Maskini Bado wanaendela kuiimbia Nyumbo za Utukufu na kuipa Ushindi CCM

  Pamoja na Wajawazito kuendelea kupelekwa Hospitali na Mikokoteni ya kusukumwa na Punda lakini bado wanaendela kuvaa vitenge vya CCM na kuimba nyimbo za Utukufu kwa CCM zilizotungwa na Wanaoshoba wachache akina Hadija Kopa

  Pamoja na Wagonjwa kulala chini mahospitali lakini pindi wanaporuhusiwa kutoka Mahospitali huimba Nyimbo za Kuitukuza CCM ambayo ndiyo iliyotengeneza Seriakali inayowalaza chini katika mahospitali

  Pamoja na Wanafunzi kukandamizwa na Serikali ya CCM, na pengine hata kupigwa na FFU laiki wao ndio wamekuwa mstari wa mbele kuiimbia na kuitukuza CCM, na wamekuwa msatari wa Mbele kuwaita Wapinzani Mavuvuzela ( very sad indeed)

  Pamoja na Wafanyakazi kuendelea kudhulumia toka enzi za Uhuru lakini wamekuwa ni Mawakala wazuri sana katika kukihakikishia chama hiki ushindi wa Kishindo

  Pamoja na Wakulima kuibiwa Mbegu zao za Ruzuku bado wamekuwa wakikipa chama hiki Ushindi mnono kila ya Baada ya Miaka Mitano

  Nasema najua watu wataniona mimi Hamnazo lakini niko Serious sana kwa 2010 NIKO TAYARI KUFUNGA NA KUOMBA CCM ISHINDE

  1: URAIS KWA 100%,
  2: UBUNGE KWA 100% NA
  3: UDIWANI KWA 100%

  Nasema hivyo kwa Sababu

  1: Pamoja na Wapinzani wachache kuonyesha japo kukuruka sisi wananchi tumekataa kuwaongeza Bungeni

  2: Nadhani tutakapokuwa na 100% may be wananchi wanaweza kuhisi Umuhimu wa Upinzani Imara katika Mfumo wa Kiutawala

  3: Na wakiwamiss akina Zitti, Slaa na Wengine May 2015 wanaweza kuamua kuwaingiza kwa Wingi

  KWA MARA NYINGINE TENA NASEMA EE MUNGU NAOMBA USAIDIE CCM IPATE 100% Ili uwapumzishe wapiganaji wetu wa Ukweli akina Dr. Slaa ambao waa risk Maisha yao kwa ajili yetu, wamekubali kuwa Upande wa Maskini lakini sisi Maskini tumewakataa, Wamekubali kupiga kelele juu ya Wizi wa Raslimali zetu sisi maskini lakini sisi Maskini tumewaita Wapayukaji na Waliokosa Mwelekeo, Wangeweza kuweka Silaha Chini na Kujiunga wa Wenye Mirija lakini wamekataa na kuamua kukaa nasi

  Mungu Uwapumzishe wapiganaji hawa kabla hawajachoka, Labda kama Wakipumzika tutafunguka na Kutambua Umuhimi wao

  Nimetoa Ujumbe Machozi yakinilenga lakini ndilo lililopo Moyoni Mwangu
   
 2. kipipili

  kipipili JF-Expert Member

  #2
  Jul 11, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 1,499
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  mtaji wa maskini bni nguvu zake mwenyewe
   
 3. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #3
  Jul 11, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  ukiona mtoto anashirikiana na mwizi kumwibia baba yake ujue hapo kuna kazi
   
 4. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #4
  Jul 11, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Ndege ya uchumi, ujue kwamba ignorance is very expensive! Watu wetu wengi bado hawajajua maana ya Upinzani wa vyama. Na mbaya zaidi hata wasomi wa vyuo vikuu - matokeo ya kisomo karirishi. Vijana hawana uwezo wa kuwa na crirtical mind. Wanakuwa kama kasuku na bendera fuata upepo. Itachukua miaka mingi watu kuelimika (siyo kusoma tu) na kuona kile wanachopaswa kusimamia katika kweli na haki. Mkuu, ndege ya uchumi usije kuona ajabu hata kama CCM watachukua maviti yote sasa na hapo 2015 bado wakachukua maviti yote tena kwani watanzania bado tunapiga usingizi wa pono, na CCM kwa hakika wanajua udhaifu huo, na wanautumia effectively. Wamefikia mahali wanawadanganya wananchi kimachomacho bila haya wakijua kwamba wananchi hawajui kitu; na kwa hakika hawajui kitu. Ndo mana nikasema ignorance is very expensive. It costs the wananchi a lot. We need changes!
   
 5. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #5
  Jul 11, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kila kukicha Hali ndio inazidi kusikitisha yaani. Watu wanalalamika Maisha Magumu, Watu wanataka Mabadiliko lakini ikifika Kipindi cha Uchaguzi inakuwa kama Wamerogwa yaani

  Tunaweza kulaumu Upinzani kwamba hawapresent Wagombea Wanaokubalika na Wananchi, Lakini Hao Wagombea Wanaokubalika Wasipojitokeza Upinzani ufanye nini sasa
   
 6. Tuntu

  Tuntu JF-Expert Member

  #6
  Jul 11, 2010
  Joined: Jan 28, 2009
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nashawishika kuwa maombi yako yatapata majibu yenye error ya less than 15% kwenye uraisi, less than 9% kwenye ubunge, na less than 5% kwenye udiwani.
   
 7. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #7
  Jul 11, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Nitasikitika sana yani, nataka iwe 100%
   
 8. Tuntu

  Tuntu JF-Expert Member

  #8
  Jul 11, 2010
  Joined: Jan 28, 2009
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni impossible kwa sababu kuna Watanzania wa Visiwani ambao tayari wana chama mbadala.
   
 9. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #9
  Jul 11, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
   
 10. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #10
  Jul 11, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  naomba iwe vice versa
   
 11. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #11
  Jul 11, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,497
  Likes Received: 1,062
  Trophy Points: 280
  Hivi jamani waganga woote hawa hakuna anaeweza kutusaidia kuwashushia balaa wezi hawa wanaojiita viongozi!? yaani ikiwezekana hata kuungua ndege kama Poland...
   
 12. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #12
  Jul 11, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Hahaaa! Mzizi wa mbuyu umenichekesha kweli! Waganga hawana kitu ukienda ki-natural. Ila ukienda kishirkina /kimazingira hapo ndo utapambana na mazingaombwe yao, mana inakuwa kama simu iliyoona signals za network ndipo iitikie. Bila kuwepo signals simu inakuwa ineffective. Hivyo hivyo miganga ya kienyeji haina nguvu mbele ya mtu asiyejihusisha na mazingara. The network fails to be established.
   
 13. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #13
  Jul 13, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ndege ya Uchumi tafakari na fikiria masuala haya: Imagine tangu mwanzo wa vyama vingi, mali zote za CCM zilizozalishwa na Watanzania wote -- zingegawanywa kwa vyama vyote vya upinzani.

  Au fikiria CCM ingekuwa ni mojawapo tu ya vyama vilivyoanzishwa wakati wa ujio wa vyama vingi -- yaani baada ya sheria ya vyama kupitishwa, CCM ingefutwa kabisa na kuanza with a clean slate, the situation that would have bee fair to all parties. Au pia fikiria mwaka 1995 Mwl Nyerere angekubali kukaa above party politics na asingeipigia kampeni CCM.

  Fikiria pia iwapo NEC ingekuwa huru kweli -- yaani isingeteuliwa na mgombea wa urais wa CCM.

  Jee Ndege ya Uchumi, haya mambo yote yangekuwa yamefanyika, wapi ingekuwa CCM leo. Bila shaka kulikotokomea UNIP ya Zambia na KANU ya Kenya. Hili halipingiki.

  Ni aibu kuisifia CCMN kiasi hicho huku wafahamu kuwa hakuna level playing field! Unafanya makusudi tu. Unajua ukweli lakini huutaki kuukubali.
   
 14. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #14
  Jul 13, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,945
  Likes Received: 2,090
  Trophy Points: 280
  Tatizo ni Tume za uchaguzi kurekebisha tarakimu!
   
 15. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #15
  Jul 14, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mkuu Nadhani Hujaelewa Nilichoandika
   
 16. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #16
  Jul 14, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Ndege ya Uchumi, naweza kushiriki katika maombi yako ili CCM ipate ushindi aslimia 100 kwani watu wanaudhi wanatetewa lakini wanadharau, tuwaache muda kidogo wateseke then watajua mchango wa vyama vya upinzani nini. Mana kwa sasa wanaona CCM ni Mungu wao. Natafakari kama ntakuunga mkono ili ombi lako lijibiwe unavyotaka
   
 17. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #17
  Jul 14, 2010
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Shortcut ni kwashauri wapinzani wote wasigombee popote wala kushiriki uchaguzi, vinginevyo 100% is impossible
   
 18. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #18
  Jul 14, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  I wish ningekuwa na Uwezo huo ningewashauri wasigombee au wakigombea kwenye Kampeni zao wawambie wananchi mkitaka mtuchague msipotaka msituchague

  Watanzania wanahitaji kupata Mateso Fulani kama waliyowapata wana wa Israel, Pamoja na kwamba tuna tume isiyo huru ukweli wa Mambo ni kwamba Watanzania wengi wanaichagua CCM tena wale Maskini ndio wanaopiga kura na kuichagua CCM
   
 19. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #19
  Jul 15, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  watanzania haswa Walala Hoi Wengi wao wamelala Usingizi ngoja kwanza Wachapwe na Viongozi Mafisadi Miaka 5 ijayo waipate ndipo watakapoamka. Na huo muda wa kuamka utakuwa kwao hao walala hoi Nchi yetu itafika kama Zimbabwe Mtu unakuwa na Mapesa Mengi lakini yote ni makaratasi hayana thamani. Itafika hapo Bongo Kuku mmoja atauzwa Shilingi Millioni moja yai la kuku moja itafika shilingi Elfu kumi ndipo hao Walala hoi watakapo Amka na kuchaguwa Viongozi wa vyama vizuri,viongozi wanaopenda Nchi yao sio hao viongozi Mafisadi. Mwenyeezi Mungu hawezi kuisaidia nchi yetu mpaka sisi wenyewe Tujisaidie na kuamka toka ujingani au toka katika usingizi mzito WaTanzania bado wapo Usingizi mzito.
  Kuna Msemo mmoja usemao kuwa (MTU ALALAYE USIMWAMSHE UKIMWAMSHA UTALALA WEWE) sisi huwa tunajitahidi kuwaamsha WaTanzania haswa walala hoi wawachaguwe Viongozi wazuri bado WaTanzania Walala Hoi wanawachaguwa Viongozi Mafisadi tuamkeni WaTanzania asanteni.
   
 20. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #20
  Jul 15, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Wewe, kama walivyo makada wengi wa CCM, na 'wafuasi' lukuku, hukuelewa kabisa nilichoandika simply because pamoja na yote uliyosema bado unan'gan'gania CCM hushinda kwa njia ya halali kabisa in a very level playing field. Kwa mfano, kwa jinsi akili yako ilivyogandia upande mmoja, katika topic yalo hukuitaja kabisa NEC (tume ya Uchaguzi) jinsi isivyo halali na huru! Na hiki ndicho kitu kikubwa kulikoi vyote katika chaguzi za kidemokrasia halisi.

  Kama bado unao ubavu kuhusu hili la NEC, tulijadili kwa kinana uone iwapo CCM imekuwa ikishionda kwa halali. Come on....
   
Loading...