MLAU
JF-Expert Member
- Aug 23, 2007
- 4,726
- 3,358
Wanabodi wa JF tusaidiane mawazo ktk hili.
Ni muda sasa naona kumekuwa na mapambano na mashambulizi Mara baada ya Askofu Gwajima kutangazwa hadharani na Paul Makonda Mkuu wa Mkoa wa Dar kuhusiana na vita dhidi ya madawa ya kulevya.
Askofu Gwajima amekuwa kila Jumapili ktk Ibada zake ni kutoa mashambulizi dhidi ya Paul Makonda kitu ambacho sidhani kama ni fair sana kwa waumini wake lakini inaweza kuwa ni furaha kwa sisi wapenda story za udaku.
Kwa uzoefu wangu kijamii naona hali mbele ya safari si salama sana kwasababu mashambulizi ya kudhalilishana Mara nyingi mwisho wake huwa ni mbaya.
Na Askofu amediriki kusema jpili hii kuwa haogopi kufa sasa naona ameanza kuweka mazingira fulani kwa waumini wake kuwa kuna tukio linaweza kutokea na yeye yuko tayari.
Sasa mahubiri kama hayo kwangu Mimi si mazuri sana ...mfano siku imetokea bahati mbaya baya lolote limemtokea unafikiri waumini watafikiri nini cha kwanza??
Nilikuwa na mtazamo tu kabla hatujafika mahali pabaya naomba watu wenye busara waangalie namna ya kuwasuluhisha watu wawili ili amani moyoni mwao itawale.
Ni wazo tu lakini kwasababu naona mambo yanayoongelewa juu ya mwinhine ni mambo binafsi
Nawasilisha