Naomba aliyemwelewa Waziri Dkt. Mwakyembe juu ya hili anisaidie kunielewesha tafadhali

Status
Not open for further replies.

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,546
108,876
Jana alipopewa ' Fursa ' ya kuzungumza wakati wa ' Show ' ya Saida Karoli Waziri wa Habari, Michezo, Utamaduni na Sanaa Dkt. Harrison Mwakyembe alisema namnukuu " Nipende tu kutoa shukran kwa Waandaji na hasa kwa Msanii Saida Karoli kwa kuweza kuamka tena ila nipende tu kuwataarifu kuwa nimekuja hapa Kuburudika nanyi lakini Mke wangu Mpenzi hivi ninavyozungumza nanyi yupo ICU hivyo naomba wakati tunafurahi pamoja hapa basi pia tumuombee " mwisho wa Kumnukuu Waziri Dkt. Mwakyembe.

Mimi binafsi kama GENTAMYCINE sijamuelewa na hata ' moyo ' wangu hadi sasa ' unakataa ' kabisa kumuelewa kwa kile kitendo cha kumuacha ' Mkewe ' ICU halafu na ' kukimbilia ' Escape One ' kutiririka ' na ' kuserereka ' na Mwanamama Saida Karoli.

Naamini kabisa kuwa humu JF kuna ' Watu ' wengi ' Vichwa / Vipanga ' kabisa hivyo hamtashindwa kunisaidia ' kunielewesha ' juu ya hili jambo ili pengine baada ya ' Ufafanuzi ' wenu basi ' moyo ' wangu uweze ' Kufunguka ' rasmi na nimwelewe Waziri Mwakyembe.

Nawasilisha.
 
" Nipende tu kutoa shukran kwa Waandaji na hasa kwa Msanii Saida Karoli kwa kuweza kuamka tena ila nipende tu kuwataarifu kuwa nimekuja hapa Kuburudika nanyi lakini Mke wangu Mpenzi hivi ninavyozungumza nanyi yupo ICU hivyo naomba wakati tunafurahi pamoja hapa basi pia tumuombee "

Umeruka maneno

Kama hukuyasikia yote mwenyewe nenda kaangalie video ya jana

Iliwekwa humu.

Mumuache Mzee wa watu alielezea kufikia hapo na maneno kayalete uweke sawa

Mkitaka kuuliza muwe mnanukuu kila neno sio kudakua tu.

Kwa kweli sio kitu cha kuandika na kumsema mtu, inalekea hujawahi kuuguliwa wewe... sijapenda huu uzi kabisaaaaaaaa

Siasa wakati mwingine zina mipaka kwenye maisha binafsi ya mtu.

Tumuombee Mama Mwakyembe apone haraka.
 
Duuh alishindwaje hata kumuachia naibu wake??

Halafu GENTAMYCINE ' nikiwachana ' humu JF kwa ' madhaifu ' yao yaliyotukuka ' wananuna ' na ' Kunimaindi '. Hivi ' PhD ' yake aliipatia katika Chuo Kikuu gani ili kama vipi ' nikitembelee ' kwa ' Kukiperuzi ' tu niweze kukijua na niweze kufanya ' mlinganisho ' na Waziri aliyemwacha ' Mkewe ' ICU na kukimbilia kwenda ' Esikepu Moko ' jana.
 
Mwanasheria mkuu yule alipatia PHd yake Ujerumani Hamburg university
 
Umeruka maneno

Kama hukuyasikia yote mwenyewe nenda kaangalie video ya jana

Iliwekwa humu.

Mumuache Mzee wa watu alielezea kufikia hapo na maneno kayalete uweke sawa

Mkitaka kuuliza muwe mnanukuu kila neno sio kudakua tu.

Kwa kweli sio kitu cha kuandika na kumsema mtu, inalekea hujawahi kuuguliwa wewe... sijapenda huu uzi kabisaaaaaaaa

Siasa wakati mwingine zina mipaka kwenye maisha binafsi ya mtu.

Tumuombee Mama Mwakyembe apone haraka.

Nadhani utakuwa umenijibu ' Kimihemko ' na ukaongeza na ' Upumbavu ' wako ' uliokukomaa ' kwa muda mrefu. Kwa kukusaidia tu nimeandika huu ' uzi ' kwa masikitiko makubwa kutokana na kwamba hakuna jambo jema kama kutanguliza Kwanza Upendo wako kwa Mke / Mume wako hasa pale akiwa na shida / matatizo.

Hata kama ' utajitutumua ' kujifanya unamtetea Waziri Mwakyembe ila ukweli utabaki pale pale kuwa hayo maneno aliyasema pale ' Ukumbini ' na kwa faida yako tu siyo Mimi peke yangu ambaye nilishikwa na ' butwaa ' bali almost ' Njemba ' nyingi sana pale ' Esikepu Moko ' nazo zilimshangaa Waziri.

Jifunze kujenga ' Hoja ' na acha kuwa na ' Mahaba ' ya Kingumbaru / Kijinga na namalizia tena kwa kusema nikijiamini kabisa kuwa Waziri Mwakyembe jana hakumtendea haki ' Mkewe ' ambaye alikuwa hoi ' ICU ' na Yeye kwenda katika ' Show ' ya Saida Karoli. Kwa Mtu mwenye ' akili ' zilizomtosha hawezi kumuelewa.

Nasubiri urudi tena ili nizidi ' Kukufundisha ' jinsi ya ' Kufikiri '.
 
Mwanasheria mkuu yule alipatia PHd yake Ujerumani Hamburg university

Sasa mbona hafanani na ' Wajerumani ' wenyewe waliompa ' Taaluma ' hiyo? Nijuavyo ni kwamba hakuna ' Watu ' makini duniani kama ' Wajerumani ' na hawana huo ' Ukengeukaji / Upotokaji ' ambao tumeuona kwa ' Daktari wa Falsafa za Kisheria ' kwa kumuacha ' Mamie / Mke ' wake na ' Kutimba ' Esikepu Moko.
 
Mimi sielewi hata imekuaje...Pole nyingi zimfikie mkewe
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom