Naogopa kuitwa M'MBEA

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,427
154,270
Rafiki yangu alifunga ndoa miezi miwili iliyopita na mchumba wake wa siku nyingi.
Kutokana na ukali wa foleni huwa ninakuwepo maeneo ya mjini nikipata moja baridi, moja vuguvugu na nyingine moto.

Kila siku huwa namuona huyu shemeji yangu akiwana na kasharobaro kamoja kenye kuvaa milegezo huku wakinyweshana pombe, denda kidogo na kutomasana kwa fujo.

Natamani kumwambia mumewe licha ya kuwa naumia moyoni.
Najua nikimwambia mumewe nitaharibu uhusiano wao, na siku wakipatana wataniita M'MBEA.

JE NIFANYEJE?
 
Subiri kidogo, ina maana huyo shemeji nae hua anaona kuwa umemuona? Kaaa kimya kaka, waweza kuta jamaa ndio kamtuma mama, sidhani kama yanakuhusu sana japo inauma sana na inauma kwasababu na wewe unakuwa na mawazo kama hayo kuwa huenda shem anakufanyia hivyo...au nadanganya?

Hama hio bar maana kama jamaa atakuja kumfumania mkewe na akijua kuwa ulikua unajua na hukumwambia bado itakuwa tena shida kwako, vizuri acha kupata hizo za baridi, za uvuguvugu na za moto, kajikalie kwenye foleni uwahi nyumbani, hii ina faida mbili; utaepusha ugomvi na rafiki yako endapo atatambua kuwa ulikua unaona mkewe akiiba na ukakaa kimya lakini pia utakuwa na muda mzuri na familia yako na kuondoa lile wazo kuwa wawezasaidiwa kumlea shemeji...karibu nguruwe, na mimi nasubiri foleni hapa jirani jirani tu
 
Buji mshikaji wako ana mahela sana? Mahusiano ya nyuma ni vigumu sana kuyaacha, dah sharobaro bila shaka ni kidumu cha huyo shemeji yako. Na huwenda demu yuko kifedha zaidi
 
Subiri kidogo, ina maana huyo shemeji nae hua anaona kuwa umemuona? kaaa kimya kaka, waweza kuta jamaa ndio kamtuma mama, sidhani kama yanakuhusu sana japo inauma sana na inauma kwasababu na wewe unakuwa na mawazo kama hayo kuwa huenda shem anakufanyia hivyo...au nadanganya? hama hio bar maana kama jamaa atakuja kumfumania mkewe na akijua kuwa ulikua unajua na hukumwambia bado itakuwa tena shida kwako, vizuri acha kupata hizo za baridi, za uvuguvugu na za moto, kajikalie kwenye foleni uwahi nyumbani, hii ina faida mbili; utaepusha ugomvi na rafiki yako endapo atatambua kuwa ulikua unaona mkewe akiiba na ukakaa kimya lakini pia utakuwa na muda mzuri na familia yako na kuondoa lile wazo kuwa wawezasaidiwa kumlea shemeji...karibu nguruwe, na mimi nasubiri foleni hapa jirani jirani tu
mimi huwa nakaa gizani kama kawaida yangu noctunal, hanioni, ila mimi namuona.
 
Simple
Mchukue huyo rafiki yako kaa nae
Hapo .. kunyweni kuleni chekeni..
Bibie akijitokeza mwache ye ajionee mwenyewe.. then hapo hautakuwa mmbea..
Bali utakuwa wa A _town / Manyara ..karibu.

Umenena vyema.
 
uitwe mmbea mara mbili? maana wewe ni mmbea balaa? bujibuji mchezo....
 
kama unaona ni sahihi kukaa kimya na ukae kimya milele ila kama unahitaji jamaa ajue nbasi wewe jennga na jamaa mazoea ya kukaa nae bar mbalimbali lkn ukiwa na lengo la kumpeleka wanapokutana hao watu then ataona mwenyewe ... ila hakikisha jamaa humwelezi nia yako
 
Buji, usiseme ww shuhudia tu na acha hivyo hivyo mambo ya mapenzi ni maumivu ya kichwa sana, mwache ajue mwenyewe asipo mwache aishi kwa raha zake coz hajui.
 
Buji, usiseme ww shuhudia tu na acha hivyo hivyo mambo ya mapenzi ni maumivu ya kichwa sana, mwache ajue mwenyewe asipo mwache aishi kwa raha zake coz hajui.
Morio umenena lililo jema mbele za wanadamu na mbele za Mungu pia.
Nimesikia, nimetii na nitatenda.
 
Rafiki yangu alifunga ndoa miezi miwili iliyopita na mchumba wake wa siku nyingi.
Kutokana na ukali wa foleni huwa ninakuwepo maeneo ya mjini nikipata moja baridi, moja vuguvugu na nyingine moto.
Kila siku huwa namuona huyu shemeji yangu akiwana na kasharobaro kamoja kenye kuvaa milegezo huku wakinyweshana pombe, denda kidogo na kutomasana kwa fujo.
Natamani kumwambia mumewe licha ya kuwa naumia moyoni.
Najua nikimwambia mumewe nitaharibu uhusiano wao, na siku wakipatana wataniita M'MBEA.
JE NIFANYEJE?

Hii issue ngumu sana...yaani unasign death certificate ya rafiki yako hivi hivi kwa kuogopa kuitwa m'mbea! Wait till he is down with HIV, thats when you can tell him, na hutaitwa m'mbea kwani vipimo vitathibitisha kuwa we si m'mbea!
 
Buji isije ikawa na wewe una agenda ya siri (unataka na wewe upone njaa hapo) sasa unasubiri tu siku ukishikika umwambie halafu akikataa umtishie kuwa akikataa utamwambia mumewe mambo yako...hahahaaaa nimeisoma janja yako
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom