NANI ZAIDI: Nilikuwa na Mashaka na Simba kumbe ni kweli wanatumia fumbate

demigod

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
8,250
15,116
Nimekuwa nikifuatilia kwa karibu sana suala la hii kampeni ya Nani Zaidi?

Kwa uwiano uliopo kati ya mashabiki wa Simba na Yanga, inawezekana vipi wapiga kura wa Simba wawe wengi mara mbili zaidi kuliko wale wa watani zao Yanga?

Hata ukizingatia tu uwezo na msukumo wa uchangiaji kutoka kwenye kampeni yao ya Ujenzi wa uwanja...Huwezi kuona uhalisia baina ya kapeni hizi mbili.

(kumbuka kuwa Simba walitumia miezi 6 kufikisha milioni 60)

Tena kwa kutumia michango ya mashabiki. Tena pasi na kuwekewa kuwango zuizi cha uchangiaji!

Sasa wamewezaje kufika milioni 100 ndani ya mwezi mmoja...?

Ukitumia ubongo wako mpenzi msomajinutagundua kuwa kampeni ya uchangiaji ilivamia na FUMBATE ya kuhamisha pesa ya klabu yao kwa lengo la kuwaaminisha wanachama na mashabiki wao kuwa wako vizuri, wakijua wazi kuwa mashabiki wao wataamini na hawatoweza hata kujiuliza maswali magumu.

Leo katika mkutano wa waandishi wa Habari wa klabu ndipo nikapata kuthibitisha shaka yangu kuwa niko sahihi 100%

Idara ya Klabu ya Yanga iliweka wazi mbinu iliyoyumika na simba ili kuuaminisha watu wao kuwa hawawezi kushindwa na Yanga kwenye kila kitu msimu huu.

Walichokifanya ni kutoe pesa mfuko wa kushoto na kupeleka kulia ili kuonyesha kuwa wako safi.

Hongereni Simba SC lakini msisahau kusajili kwa kuwa dirisha la CAF limesalia siku chache kutoka hii leo.

View attachment 2259739
 
Mimi ni Simba damu (rejea post zangu za nyuma) lakini Mo anataka atudanganye ili tusahau kinacho endelea pale Msimbazi, nasikitika kuwa Kigwangala akiomgea anaonekana lofa, ni kweli Kigwangala simpendi lakini kwenye hili la Simba yuko Sahihi, Moo usitudanganye hizo hela umeziweka wewe kwa ushawishi wa CEO
 
Hakuna shabiki wa Simba mpuuzi mpuuzi km wewe.Wewe ni uto uliyejivika usimba..period!!
 
Watu wazima wanacheza na mashabiki wao!
Ukienda katika followership ya timu hizi katika Social Media Simba wana followers mara mbili au zaidi katika kila mtandao. Simba Facebook wana followers 1M Yanga wana laki 5, Instagram Simba wana followers 3.8M Yanga wana 1.9M unashangaa nini kwamba Simba imeizidi Yanga mapato two times wakati hata followership mitandao Simba wanawazidi Yanga two times?

Inawezekana Yanga walipata peaa hizo 1B ( kama ni kweli maana sote twajua Manara ni mwongo mkubwa) ila kupata hizo pesa stratergy yake wala haihusiani na Uchangiaji huu.
 
Mleta mada naomba nikukumbushe Tu mambo kadhaa kuhusu Simba

1.Simba ndy club yenye vibe mtandaoni kuliko club yoyote kusini mwa jangwa la Sahara,na linapokuja swala km Hilo linakuwa km kumsukuma mlevi tu Kwa mashabiki wa simba

2.kwenye mitandao ya kijamii Simba imemwacha mbali sn yanga Kwa followers
Simba 934,000 wakati yanga 192,000(Twitter pekee)
Umejifunza nini hapa kuhusu hili linaloendelea?

3.Siku kadhaa nsemaji wenu white aliwahi kukiri kwamba Simba imemwacha mbali sn yanga kwenye hamasa za mtandaoni.Huoni hili Kwa Simba ni km kumwambia mtoto avunje biskuti?

4.Point yangu ya mwisho ni hii;Umesema kwamba huko nyuma Simba ilichangisha mil 60 Tu lkn umesahau kwamba wakati ule ilikuwa haishindani na yeyote lkn Simba linapokuja swala la kushindana,mashabiki wa Simba ni km wanakuwa vichaa Kwa kuisapoti timu Yao
 
Mimi ni Simba damu (rejea post zangu za nyuma) lakini Mo anataka atudanganye ili tusahau kinacho endelea pale Msimbazi, nasikitika kuwa Kigwangala akiomgea anaonekana lofa, ni kweli Kigwangala simpendi lakini kwenye hili la Simba yuko Sahihi, Moo usitudanganye hizo hela umeziweka wewe kwa ushawishi wa CEO
Ushawah kumpa hela mo mkuu?
 
Ukweli ni kwamba Simba kwenye nani zaidi wamehamasika kuchanga kwasababu wanashindana na mpinzani wao.
michango ya ujenzi wa uwanja ilianza pasi na ushindani,apakua na msukumo wa ushindani ni kutoa tu kwa hiari ndo maana machango ikawa kidogo.

ila michango ya sasa kwenye nani zaidi ni swala la ushindani,"mashabiki wa timu ipi wataongoza kuchangia timu yao,",,,hapo sasa kuna msukumo wa ushindani.

Mechi za kimataifa Simba ni kinara wa kujaza uwanja wa Mkapa,kuingia uwanjani ni kwa pesa sio bure.bado mashabiki wa Simba wanaingia na wanajaza uwanja full house.
mashabiki wa Simba kuanzia asubuhi mpaka usiku wanapanga foleni maduka ya Fred Vunja bei mikoa ya Mbeya,Mwanza,Dar n,k kwaajili ya kutoa 35,000/=ili kununua jezi za Simba.
Linapokuja swala le pesa mashabiki wa Simba wako vizuri kujitoa kwaajili ya timu yao.
JamiiForums1252849155.jpg
 
Ukienda katika followership ya timu hizi katika Social Media Simba wana followers mara mbili au zaidi katika kila mtandao. Simba Facebook wana followers 1M Yanga wana laki 5, Instagram Simba wana followers 3.8M Yanga wana 1.9M unashangaa nini kwamba Simba imeizidi Yanga mapato two times wakati hata followership mitandao Simba wanawazidi Yanga two times?

Inawezekana Yanga walipata peaa hizo 1B ( kama ni kweli maana sote twajua Manara ni mwongo mkubwa) ila kupata hizo pesa stratergy yake wala haihusiani na Uchangiaji huu.

Jibu lako ni hili:

Simba ilianza mapema zaidi kufanya social media investiment.

Followers wote hao sio mashabiki wa simba.

Kama mnawafuasi na mashabiki wengi kwanini YANGA SC iliwapiga gape kubwa kwenye mapato ya gate collection msimu ulio pita?
 
Back
Top Bottom