Nani yupo sahihi: Magufuli vs Lissu

NO! Ni kwamba wenye akili ndogo mpo wengi...hivyo Lisu lazma awe Nabii au Mungu kwenu..

Aya bhana, ila alishawashinda wote, sasahivi anashindana hoja na SMG, binadamu wa kawaida hawamuwezi tena....
 
Alichokua anaongea lisu ni mikataba mibovu ambayo tuliishangiria sana mmoja wapo Leo anatwambia tunaibiwa apo mlipokua mnapitisha hamkujua, au ao tunaowasema Leo wametuibia walituamulia tu nasisi tumewakubalia, Magufuli alikuwemo kupitisha mikataba hakujua inatunyonya amejua leo hii ,acheni kupumbazwa mkapumbazika , yaani mtu anatupa taka halafu anazizoa mnamsifu kwa kumshangilia hii itakua akili au matope
Kuna makosa yalifanyika/yalifanywa na serikali za awamu zote chini ya CCM, tena makosa ya makusudi na kuacha inchi ikivuja huku wakihongwa kidogo kisicholingana kile kinachoibiwa.........
Hoja ni kwamba hakuna room ya kurekebisha makosa tena? tukae tu kimya bila kutafta solution?
Na mikataba imebadilishwa na Barrick wamekubali hayo mabadiliko, Je hakuna mwanga mpya kwenye hilo?
 
Aya bhana, ila alishawashinda wote, sasahivi anashindana hoja na SMG, binadamu wa kawaida hawamuwezi tena....

Again NO! Guns do not kill people BUT people kill people! So Im sure Lisu akitakiwa kufa atakufa tu.Waliopiga risasi walitaka tu kuua news za rais kuhusu almasi na Tanzanite wangetaka kumuua risasi moja ilitosha kabisa.
 
.Waliopiga risasi walitaka tu kuua news za rais kuhusu almasi na Tanzanite wangetaka kumuua risasi moja ilitosha kabisa.[/QUOTE]

Siyo kwa upigaji ule........

Na sio kwamba akili hawana hata kuuwa wameshindwa huku wakiwa na bunduki....?
 
Kwani mpaka sasa tumepata nini? Hiyo dola milioni 300, kipindi chote uzalishaji uliposimama, tumepoteza kiasi gani kupitia kodi, uwekezaji, michango ya kwenye mifuko ya kijamii, mishahara ya wafanyakazi waliofukuzwa, na zaidi Tanzania kuonekana ni mahali hatari kwa mitaji ya nje?

Leo hii kati ya kampuni 160 zilizokuwa zikifanya utafiti zimesimama. Wafanyakazi wameachishwa kazi, kodi mbalimbali hazipo. Pesa zilizokuwa kwenye mzunguko kutokana na mapato ya wafanyakazi, hazipo tena. Makampuni yote yaliyowekeza Tanzania yamepotea thamani kwenye share markets kwa 30 - 60%. Unaelewa hiyo pesa iliyopotea ni kiasi gani? Una uhakika gani makampuni haya yatarudi tena Tanzania kuendelea na utafiti (kumbuka serikali haina uwezo na haiwezi kufanya utafiti)? Bila utafiti hakuna sustainability ya industry.

Hivi unafahamu kuwa hiyo 50/50 haina maana yoyote kwenye biashara ya madini? Unajua kuwa tuna 50% mgodi wa Mwadui lakini hatupati chochote? Unafahamu kuwa faida kubwa kwenye biashara ya madini haitegemei moja kwa moja mauzo ya madini?

Baada ya miaka mitatu hivi, turudi kujadili faida zilizopatikana kutokana na mabadiliko haya. Ongezeko la mapato litatokana na ongezeko la mrabaha kutoka 4% mpaka 7% lakini siyo kutokana na 50/50. Hata hiyo 7% itaongezeka kutoka kwenye operations zilizopo lakini itasababisha anguko kwenye utafiti na new developments.

Tulisema toka mwanzo Barrick kama kuna hela watatoa haitafikia hata bilioni 1, tukaonekana wajinga. Lakini leo ukweli umedhihiri. Tulisema taarifa ya Mruma ilikuwa ya uwongo, leo imedhihirika, Acacia hawakukutwa na hatia yoyote ya kukwepa kodi au kutoa taarifa za uwongo juu ya dhahabu iliyopo kwenye concentrates.

Nchi ni yetu sote. Kila mmoja ana cha kuchangia. Wapo wanaodhani Tanzania ni ya kwao zaidi kuliko wengine. Wote ni Watanzania, wote tunaitakia mema nchi yetu. Tatizo wengine wanajenga nyumba hewani, wengine tunajua kuwa nyumba ni lazima iwe na msingi jliojengwa ardhini.

Barrick versus Tanzania 84/16% share,

Je ni mwanzo mpya?
 
Back
Top Bottom