Elections 2010 nani yupo sahihi kwa hili kati ya silaa na lipumba?

faithful

JF-Expert Member
Aug 10, 2010
378
33
Wadau mnaotambua kwa undani katiba ya nchi na pia mnaoifahamu demokrasia ya vyama vingi naomba mnipe elimu kidogo.................nimefatilia kampeni za uchaguzi kwa makini sana haswa vyama vya upinzani...nimeona lipumba akifika kwenye mkoa fulani anaanza kwanza kuripoti ofisi za serikali kama ofisi ya mkuu wa wilaya husika au mkoa husika ili apate baraka za ya serikali iliyopo madarakani......kisha ndio anaendelea na kampeni zake....lakini sijawahi kumwona silaa akiripoti ofisi za serikali.........
JE NI NANI ANAFATA TARATIBU SAHIHI?
 
Ulishasikia hao wakuu wa wilaya wanalalamika kuwa hawatendewi haki kwa Dr Slaa kutokwenda kwao>
Dr Slaa huwa ni mgeni pale aendako na wakuu wa wilaya wanatakiwa wao kwenda kuwalaki wageni wa kitaifa. Sasa Slaa aende kwao kufanya nini kama wao hawakuja?
 
Hakuna mahali kwenye katiba au sheria inayomtaka mgombeaji kuripoti kwa mkoa au wilaya. Hivyo wote wako sahihi tu kwani ni kipenda roho tu na hakina shinikizo la kisheria.
 
Dr. Slaa (na wagombea wengine offcourse) walishawasilisha ratiba za mikutano yao ya kampeni kwa Tume ya Uchaguzi, ratiba hizo zinaonyesha pamoja na mambo mengine, mahali na tarehe atayofanya mkutano, taarifa hiyo inamfikia pia Mkurugenzi wa wilaya ambaye pia ni msimamizi wa uchaguzi katika wilaya husika, hivyo nadhani hakuna umuhimu wa kuripoti kwa mkuu wa wilaya kwani ujio wao unafahamika na umefuata taratibu zote.
 
Back
Top Bottom