Nani yupo nyuma ya mauaji haya ?

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,745
Kuna vifo ambayo vinapowatokea baadhi ya watu huonekana si vya kawaida na badala yake inavuma na kuonekana ni mauaji yametendwa na serikali au baadhi ya watu ambao wamo ndani ya serikali.
Sasa ni miaka mingi Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikwisha fariki na wakati wake kuna viongozi ambao walifariki kama Sokoine na Kolimba na kama wako wengine mnaweza kuongezea ,habari zilizovunwa kutokana na vifo vyao ni kuwa Mwalimu alihusika kwa njia moja au nyengine ,tumesota mpaka wakati wa Mkapa akafariki Dr.Omar Ali Juma napo pakavumishwa kuwa jamaa wamemtoa roho na hadithi ndefu zikiambatana kuhusishwa na kifo chake ,hivi sasa mambo mabichi ya juzi wamekufa viongozi kwa kupishana wengine wakipinduka na magari na kuvunjika mikono,kuna Amina Chifupa ,kuna yule waziri alieanguka na ndege kuna Balali ambae bado hadithi zake zinaendelea mitaani.
Mimi siamini kama watu hawa wameuliwa kwa kutumia serikali au kikundi fulani naona ni mauti ya kawaida tu ambayo kwa namna yanavyotokea hata raia wa kawaida nayo huwakuta tofauti ni rank za kimaisha ndizo zinazofanya mmoja kujulina sana na mwengine hujulikana na watu wa karibu yake na mtaani.Kuna nyengine nazo ni habari za kutaka kuhujumiwa kwa mfano iko tetesi ya Salim ahamedi wakati akiwa katika Uwaziri wa ulinzi ,lipo la Seif Sharifu kuchomekewa sumu na kuwahiwa Uingereza ,ajabu sijasikia waandishi wakiwahoji hawa waliokosewa juu ya tuhuma hizi ?
Tatizo ninaloliona ambalo linajijenga ni kuwa kiongozi wa Tanzania hafi ila kuwepo na watu wanaosababisha kifo chake kabla ya wakati au kwa lugha nyepesi ni kuwepo kwa kikundi kinacho au vhenye uwezo wa kuwahujumu viongozi wa Tanzania ni sawa na Nchi ya Pemba ambako hafi mtu isipokuwa atakuwa amelogwa wala huko hakutokei ajali isipokuwa wachawi wamefanya mambo yao ,ni itikadi ambazo zimejengeka na kufikia shida na tabu kuziondoa na kufutika kabisa.
Baada ya dibaji hiyo ndefu kidogo ili kueleweka suali kwa upande huu wa Tanzania ,ni kina nani ambao wamekuwepo tokea uhai wa Nyerere na wanaendeleza hii kazi ya mauaji ya viongozi ? Maana kama Nyerere alikuwa akihusika nilitegemea baada ya kifo chake mambo haya yangesita na kuondoka kabisa ndio hivyo hivyo baada ya kuondoka Mkapa lakini bado viongozi wanaokufa wanaonekana wamehujumiwa na hiki kikundi ,Je WaTanzania wenzangu mnaamini jambo hili ?
Ni mauaji ya kisiasa au kiutawala ?
 
Sijaielewa mada yako inahusu nini na inatoka wapi na kwenda wapi! Labda iweke sawa kabla ya kuichangia.
 
Nani yuko nyuma ya vifo hivi nasema ni shatwani tu maana Mungu hapendi watu wafe ina huwa anawaita mbele zake baada ya kuda wao kwisha hapa Duniani
 
Back
Top Bottom