Ncha Kali
JF-Expert Member
- Sep 19, 2019
- 14,501
- 27,000
Ni hoja ya swali.
Kesi dhidi ya Paul Makonda sasa imeiva, ni kuhusu kinachoitwa madaraka ya kulevya. Moja ya msingi inajengwa juu ya uvamizi wa kituo cha Runinga, Clouds Media.
Japo CMG wamekanusha hawahusiki, yaani ni kama wamejitoa [wamenawa] kiaina [kimtindo].
Inasemekana 'mainjinia' wakuu wapo Mtama na Bumbuli. Japo Bibie amejitahidi sana kumkingia kifua mtoto pendwa, lakini imebidi liachwe mikononi mwa Mawakili Wasomi wanaoitwa wa kujitegemea.
Wanene wengi wa mfumo wapo upande wa mawakili hao, ni vile tu hawataki kumfunga paka kengele hadharani. Wameshika kamba kwa umbali mrefu kidogo huku wakisubiria ONE, TWO, THREE wamtose kwenye kina.
Dah! Haya maisha haya. Akiba ya wema kwa MAMA ndo kitu pekee kitamwokoa kijana huyu.
Je, GSM atakaa kimya? Au naye ataungana na mawakili kushuhudia alivyoporwa 'Kasri' kule Kigamboni kwa kutapeliwa kuwa anamjengea Mzee Baba!
Ngoja inyeshe tuone panapovuja, tutarudi.
Ncha Kali.