Nani/ wapi wanahitaji kibarua/ mfanyakazi jijini Mwanza?

KimChi

Senior Member
Feb 14, 2018
122
159
Habari wana JF

Mimib ni Accounts graduate ambaye nimetafuta ajira(formal) bila mafanikio kwa miaka kadhaa na sioni matumaini yoyote. Hivyo naomba msaada wenu kwa yafuatayo;-

Kama unajua sehemu yoyote, kampuni, kiwanda, mradi, biashara ndogo binafsi nk. ambapo naweza kupata kazi, kibarua au shughuli yoyote ya kufanya naomba unijulishe tafadhali. Iwe wewe mwenyewe, unamjua mtu au mtu anayemjua mtu anayeweza kunisaidia kwenye hili naomba uniunganishe nae.

NB: Nahitaji shughuli yoyote ambayo kijana anaweza kuifanya bila kuzingatia taaluma tajwa japo nitapokea offer ya accounting job itakapopatikana.

Naomba kama kuna mapendekezo ya maeneo ambayo unaona kuna uwezekano wa kupata kibarua jijini mwanza naomba mnijulishe ili nikaulizie mwenyewe pia.

Ninahitaji sana ajira/kibarua wadau hivyo msaada wenu kwenye vitu nilivyoomba ni muhimu. Wakosoaji wa aina yoyote kwenye hili hawakaribishwi kuchangia ila ushauri na mapendekezo yanakaribishwa.

Asanteni
 
Pole kwa changamoto unazozipitia. Usijione mnyonge, tuko wengi tunao zipitia.

Nakupa wazo ambalo ukilifanya kwa ufanisi huenda likakusaidia walau kupata jero jero za vocha.

Kama uko mjini, tembea mitaa mbalimbali huku ukiulizia vyumba vya kupangisha kwa ajili ya makazi na biashara mbalimbali, mashamba na viwanja vinavyouzwa. Ukipata ongea na wahusika wakupe bei kisha ingia mtandaoni na mitaani kutafuta wateja.

Unaweza kufungua account ya facebook kwa jina la kibiashara, kama vile DALALI MSOMI, jiunge na online platform za kibiashara kama vile kupatana. Jiunge kwenye magroup ya madalali na biashara ya facebook. Print karatasi za matangazo ukijitangaza kama dalali wa nyumba, viwanja, maeneo ya biashara na mashamba zikiwa na maelezo mafupi na namba za simu, kisha zibandike maeneo mbalimbali ya mitaa ya jiji la mwanza.

Juhudi zako za kusaka wateja, ndio kipato chako. Dalali anapata si chini ya elfu tano kwa kwenda tu kumuonyesha mteja eneo husika. Na kuna malipo ya kiasi sawa na malipo ya mwezi mzima wa pango kwa dalali pale tu mteja atakapo ridhia eneo.

Mimi nimefanya hivyo na sio haba, kuna siku nilikuwa naamka sina hata mia napata zali la madili ya udalali. Ingawaje ni kwa Dar es salaam, sijui hali ilivyo kwa jiji la Mwanza.

Pia connection na madalali wengine ni muhimu sana.

Yangu ni hayo. Kila lakheri
 
Hili nadhani ni tatizo la wengi sana, kwanini hukumbuki kuweka contacts zako kwenye post yako. Just do it now
 
Hili nadhani ni tatizo la wengi sana, kwanini hukumbuki kuweka contacts zako kwenye post yako. Just do it now
Ni PM ndugu, naona si vyema kwa yeyote kutoa personal contacts hadharani mapema. Tutumie JF/PM kwanza mpaka hapo ulazima wa kupeana contacts utakapofika
 
Ni PM ndugu, naona si vyema kwa yeyote kutoa personal contacts hadharani mapema. Tutumie JF/PM kwanza mpaka hapo ulazima wa kupeana contacts utakapofika
Yani wewe ndo unashida halafu tena unadictate terms?
nakutakia kila la kheri
 
Back
Top Bottom