Nani wanahusika kubadilisha mtaala wa elimu tanzania ?


C

candi

New Member
Joined
Nov 25, 2010
Messages
2
Likes
0
Points
0
C

candi

New Member
Joined Nov 25, 2010
2 0 0
Napenda kuchukua fursa hii kuwapongeza sana wana JF, you are real a home of GREAT THINKERS,huwa napenda sana kusoma mambo mbalimbali kutoka kwa wadau na nimejifunza mambo mengi sana,hatimaye nimeona na mimi nijiunge na wana JF rasmi ili niweze kutoa maoni yangu kuhusu mambo mbalimbali, na kubadilishana mawazo pamoja na uzoefu.

Kwa mara ya kwanza napenda wadau mnisaidie katika suala hili.nani wanahusika kubadilisha mtaala wa elimu hapa nchini na kwa vigezo gani? Ni jambo muhimu sana kubadilisha mtaala huu ili kuenda sambamba na mazingira halisi ya wakati husika sambamba na mabadiliko yanayotokea kila kukicha.Hata hivyo mabadiliko ya mara kwa mara yanaweza kuathiri kukua kwa elimu na kusababisha wanafunzi kukosa mwelekeo.

Napata utata kidogo kama kweli wale wote wanaohusika na masuala haya huwa wanashirikishwa kikamilifu,mfano walimu na wanafunzi ambao ndio wanaotendea kazi mabadilika hayo. Na kama hawashirikiswi,hasa walimu watawezaje kufundisha kwa kufuata mtaala mpya?na wanafunzi wataelewa nini?

Wadau nipenio mwanga katika hili.
 
M

mamakunda

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2010
Messages
371
Likes
1
Points
35
M

mamakunda

JF-Expert Member
Joined Jul 4, 2010
371 1 35
Nadhani umeuliza maswali haya kwa sababu hufahamu, ila tu wanaohusika na kubadilisha mitaala ni taasisi ya ukuzaji mitaala tanzania, mtaala unabadilishwa kutokana na mabadiliko mbalimbali yanayotokea katika jamii. mfano mtaala wa zamani haukuwa na somo la kompyuta lakini wa sasa unalo, kwa hiyo mitaala itaendelea kubadilishwa kila wakati kulingana na mahitaji ya jamii na maendeleo kwa ujumla, Pia vigezo vyote kama kushirikishwa walimu na mambo mengine huwa vinazingatiwa. Na mtaala ukipitishwa lazima ujaribishwe na kufanyiwa tathmini kama unafaa na ndipo utakapoanza kutumika rasmi. Mwisho watu wanaohusika na kubadili mitaala ni jopo la wasomi wa nyanja mbalimbali za elimu wakishirikiana na walimu.
 
M

mamakunda

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2010
Messages
371
Likes
1
Points
35
M

mamakunda

JF-Expert Member
Joined Jul 4, 2010
371 1 35
Kuhusu kushirikishwa kikamilifu si rahisi manake huwezi kuchukua walimu wote nchi nzima kinachofanyika wanachukuliwa baadhi tu, kuwakilisha wengine.
 

Forum statistics

Threads 1,238,296
Members 475,878
Posts 29,315,094