Nani wanafaa kuunda Jopo la marekebisho ya KATIBA?

Supervisor

JF-Expert Member
Oct 29, 2010
559
207
Mh. Pinda kaonesha njia ya mahitaji ya katiba mpya. Je? Nani waunde jopo la kuangalia mapungufu ya katiba? Na waje na solutn ambayo wa Tz wote wataiafiki?
 
Askofu pengo. Askof peter kitula, shehe ponda, shehe basalee,mch gwajima, nabii mwingira, na wazake
 
marekebisho ya katiba ya Tanzania ni muhimu yakafanywa na jopo la wataalam kutoka kwenye taasisi mbalimbali, asasi za kiraia, madhehebu ya dini na vyama vya siasa. Siku hizi kuna wasomi wengi kwenye vyama vyetu vya siasa tofauti na zamani ambapo walikuwepo wale walioamini 'zidumu fikra za mwenyekiti'. Hawa wakiwa na uelewa mzuri wa kisheria itasaidia zaidi
 
Mh. Pinda kaonesha njia ya mahitaji ya katiba mpya. Je? Nani waunde jopo la kuangalia mapungufu ya katiba? Na waje na solutn ambayo wa Tz wote wataiafiki?

Wawakilishi watakaochaguliwa na vyama vyao labda watano toka kila chama (CCM, CHADEMA na CUF) Wanasheria mbali mbali hasa wale waliobobea katika mambo ya katiba/sheria mbali mbali. Timu ya watu kama 30 hata mpaka 50 ambayo itapewa majukumu ya kupita Tanzania nzima kukusanya maoni ya Watanzania kuhusu nini kiwemo katika katiba mpya na kisha kuyafanyia kazi na kuja na katiba mpya. Zoezi hili linahitaji budget yake kubwa tu na haitakuwa vibaya kwa budget ijayo likatengwa fungu maalum la kupata katiba mpya, Wapewe muda wa miaka 2 na nusu (kama wataanza July 2011 basi December 2013 watakuwa wamemaliza kazi yao na hivyo kuwa na miaka miwili ya kuandaa uchaguzi kwa kutumia katiba mpya na tume ya uchaguzi ambayo itakuwa huru na siyo hii ambayo ni kitengo cha CCM) ili waweze kuja na katiba mpya ambayo itatumika katika uchaguzi ujao wa 2015. Pia kwa maoni yangu tunaweza kuchagua katiba tatu toka nchi nyingine kwa mfano Kenya n.k. kuzipitia na kuona kama kuna mazuri ambayo yanastahili kuwemo kwenye katiba yetu au kuyafanyia modification ya hapa na pale ali mradi tu yanaongeza demokrasi katika nchi yetu.

Waelewa na wajuzi wa sheria kutoka
- Wabunge kutoka vyama vyote vya siasa vilivyo na uwakilishi bungeni
- Vyama vyote vya siasa
- Mashirika ya dini
- Taasisi muhimu za sheria,
- mawakili na wanashria
- Taasisi za haki za binadamu
- Majaji wastaafu nk
 
Jaji Kisanga awe mwenyekiti maana kazi alikwisha ifanya na ripoti yake na ya Jaji marehemu Nyalali iwe mojawapo ya rejea!
 
tusianze kuvua nguo kabla ya kufikia mto, tutaonekana wehu kutembea uchi kabla ya kuufikia huo mto. Tuongeze spidi ya kufika mtoni kwanza, tukifika ndio tuanze kuvua nguo ili togelee na kuuvuka.
 
Hiyo speed ndo ishaanza na wakuweka gavana hayupo sema INSHAALAH!
 
Kazi ya kwanza iwe ni kuanisha vikundi vitakavyowakilishwa kwenye mchakato wa kupata katiba mpya. Kazi ya pili ni kupata wawakilishi kutoka ktk kila kundi. Kazi ya tatu ni utekelezaji ikiwa ni pamoja na kuratibu mjadala wa kitaifa kuhusu mambo ya msingi ya kuzingatiwa kwenye katiba mpya.
 
Mh. Pinda kaonesha njia ya mahitaji ya katiba mpya. Je? Nani waunde jopo la kuangalia mapungufu ya katiba? Na waje na solutn ambayo wa Tz wote wataiafiki?

Haya ndio mambo ya kuzungumzia, mie nashangaa wanaopiga kelele, katiba, katiba, katiba. Waziri Mkuu anataka kuunda jopo, tayari habari za katiba zimeshakubalika kuzungumzwa na kufanyiwa kazi, sasa ni wakati muafaka wa kujadili hilo jopo liweje.

Heshima zangu kwako kwa kuwa a step ahead.
 
Wawakilishi watakaochaguliwa na vyama vyao labda watano toka kila chama (CCM, CHADEMA na CUF) Wanasheria mbali mbali hasa wale waliobobea katika mambo ya katiba/sheria mbali mbali. Timu ya watu kama 30 hata mpaka 50 ambayo itapewa majukumu ya kupita Tanzania nzima kukusanya maoni ya Watanzania kuhusu nini kiwemo katika katiba mpya na kisha kuyafanyia kazi na kuja na katiba mpya. Zoezi hili linahitaji budget yake kubwa tu na haitakuwa vibaya kwa budget ijayo likatengwa fungu maalum la kupata katiba mpya, Wapewe muda wa miaka 2 na nusu (kama wataanza July 2011 basi December 2013 watakuwa wamemaliza kazi yao na hivyo kuwa na miaka miwili ya kuandaa uchaguzi kwa kutumia katiba mpya na tume ya uchaguzi ambayo itakuwa huru na siyo hii ambayo ni kitengo cha CCM) ili waweze kuja na katiba mpya ambayo itatumika katika uchaguzi ujao wa 2015. Pia kwa maoni yangu tunaweza kuchagua katiba tatu toka nchi nyingine kwa mfano Kenya n.k. kuzipitia na kuona kama kuna mazuri ambayo yanastahili kuwemo kwenye katiba yetu au kuyafanyia modification ya hapa na pale ali mradi tu yanaongeza demokrasi katika nchi yetu.

Hiyo Katiba ya Kenya ina mambo ya Kadhi, iacheni kwa Wakenya wenyewe!
 
tusianze kuvua nguo kabla ya kufikia mto, tutaonekana wehu kutembea uchi kabla ya kuufikia huo mto. Tuongeze spidi ya kufika mtoni kwanza, tukifika ndio tuanze kuvua nguo ili togelee na kuuvuka.

Fafanua, hatua ipi ndio ya kufika mtoni na ipi ya kuvua nguo!
 
msibweteke kwa pinda kusema hivyo, hayo ni maoni yake binafsi yeye kama yeye, kwa wanao ota kuwa serikari ya ccm itarainika kirahisi hivyo wanapotoka, natoa tahadhari tena "WATANZANIA WANAOPENDA MAENDELEO YA TAIFA LAO MUWE TAYARI KWA LOLOTE"
suala la katiba ni vita kwani ndipo mizizi yote ya nguvu za ccm zilipo. mwenye macho aone mwenye masikio na asikie. ndio maana wamekaa kimya wakitafakari kasi na nguvu ya kudai katiba, kinacho wachanganya zaidi ni kuwa hiyo nguvu ni 'multidirectional' kuwa taasisi watu binafsi vyama wanasheria wasomi na hata nchi jirani ikitoa ushauri wanashindwa kuwakabili, na nguvu ya umma ikihusishwa sana kwa mafanikio, ccm byebye
 
Back
Top Bottom