Nani walipiga kura Arumeru? Je ni wavivu wa kufikiri? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nani walipiga kura Arumeru? Je ni wavivu wa kufikiri?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by PERECY, Apr 7, 2012.

 1. PERECY

  PERECY Member

  #1
  Apr 7, 2012
  Joined: Jan 11, 2012
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WanaJF,

  Swali hilo limenisumbua kwa takribani wiki sasa. Nimependa tuwaze pamoja: Nani walipiga kura Arumeru Mashariki? Je ni wavivu wa kufikiri?

  Swali hili lina mahusiano makubwa na kauli ambayo mara kadha rais mstaafu, Mh. Mkapa amekuwa akiwaambia wanaoonekana ni maadui wake kwa upande mmoja ama mwingine. Amewaambia wanahabari pale walipoweka nguvu kuhoji ukwasi wake baada ya urais wake. Amewaambia CDM kama wapinzani wa CCM katika kampeni Igunga na Arumeru Mashariki hapa karibuni.

  Kumwambia mtu MVIVU WA KUFIKIRI, tafasiri rahisi (yangu) ni kumwambia mtu hawazi na kuamua jambo kwa hekima. Inatosha kusema hivyo!

  Mh. Mkapa ametuambia hivyo sisi ambao mara nyingi tumeumizwa na mambo ambayo tungependa kuhoji kuhusu namna yeye alivyohusika, ikiwepo ubinafishaji wa mashirika ya umma kwa kasi kubwa wakati wa utawala wake, kujiuzia mgodi wa Kiwira, na mambo yanayofanana na hayo.

  Hoja yangu kuhusu wapiga kura wa Arumeru - ushindi kwa CDM na kauli yake ya kwamba watu ni wavivu wa kufikiri.

  Kwa matazamo wa juu juu, kauli yake ilikuwa kama inalenga kundi fulani la watu wachache - viongozi wa vyama vya upinzani, wanahabari na makundi ya wanaharakati (asasi zisizokuwa za kiserikali - ambazo zimekuwa zikihangaika kuhoji uadilifu katika utawala wake); hakuonyesha kuwambia wapiga kura kama ni "wavivu wa kufikiri".

  Tatizo la kumnyooshea mtu kidole kimoja, na kusahau kwamba vidole karibu vitatu vinakugeukia na kukunyoshea wewe linawakumba hata watu tunaofikiri wakati fulani wenye busara, na busara zao hazikupaswa kuanguka. Heshima ya Mh. Mkapa imeshuka sana wakati wa kampeni yake Arusha kuliko wakati mwingine wa uongozi wake hapa Tanzania - na yeye ndiyo anabeba maana halisi ya UVIVU WA KUFIKIRI!

  Ninapouliza nani walipiga kura Arumeru Mashariki, nauliza nikijenga maantiki katika takwimu kwamba uchaguzi wa mwaka 2010, mgombea wa CCM wakati huo, ambaye sasa ni marehemu, ambaye kifo chake kilisababisha uchaguzi wa Arumeru Mashariki kufanyika mwezi huu, Marehemu Jeremiah Sumari, alipata kura 34,661 (62.23%) dhidi ya Joshua Nasari (CDM), aliyepata kura 19,123 (34.33%) kwa tofauti ya kura 15,538.

  Sasa, baada ya mwaka mmoja tu, zaidi ya wapiga kura 13,500 ambao mwaka 2010 walionekana kuunga mkono CCM (au kwamba hawakupiga kura), lakini 2012 wanapiga kura kwa mtu ambaye mwaka 2010 alipata kura 19,123, na kusababisha apate kura zaidi 32,000, Aprili 2012; ni kumwambia Mh. Mkapa kwamba yeye ndiye mvivu wa kufikiri!

  Na ajue kwamba anapowaambia - viongozi wa vyama vya upinzani, wanahabari na makundi ya wanaharakati (asasi zisizokuwa za kiserikali - ambazo zimekuwa zikihangaika kuhoji uadilifu katika utawala wake) kwamba labda ndio wavivu wa kufikiri AJUE KUWA WAPIGA KURA NDIYO WANAFIKIRI NA KUAMUA JAMBO KWA HEKIMA! Zaidi sana, namwomba Mh. Mkapa asipende kurudia kauli hii ya kuwaambia watu ni wavivu wa kufikiri, utawala bora utakaposhika mizizi sawasawa anaweza kujikuta hata akiwa na miaka zaidi ya mia, anaweza kujikuta yuko katika vyombo vya sheria kujibu mambo ambayo anafikiri hayataulizwa tena, ambayo kwa namna moja ama nyingine yana uhusiano na uongozi wake.

  Nawatakia Pasaka Njema wanaJF wote!
   
Loading...