Nani walikuwa viongozi wa PSRC? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nani walikuwa viongozi wa PSRC?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rufiji, Apr 23, 2008.

 1. Rufiji

  Rufiji JF-Expert Member

  #1
  Apr 23, 2008
  Joined: Jun 18, 2006
  Messages: 1,628
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Kwa muda sasa tumekuwa tukisikia ni kwa jinsi gani viongozi mbali mbali wa serikali walivyoweza kujinunulia kampuni mbali mbali zilizokuwa zikibinafsishwa kwa bei ya chini kabisa . Cha kushangaza sijasikia hata mtu mmoja akiuliza ni sababu gani haswa zilizopelekea hii tume ya kubinafsisha haya mashirika bila ya kufuata taratibu kitendo ambacho kinachoashiria uzembe wa hali ya juu. Mimi ninachotaka kujua ni nani haswa walikuwa viongozi wa hii tume na jee ni sababu gani zilizowapelekea kufanya maamuzi yasiyo na kichwa wala miguu ?
   
 2. mwanatanu

  mwanatanu JF-Expert Member

  #2
  Apr 23, 2008
  Joined: Jan 22, 2008
  Messages: 845
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  http://www.psrctz.com/Main_Index.htm

  sasa hivi ni ALI KARAVINA ndio chairman
  hii cv yake

  EDUCATION

  Chartered Institute of Marketing -UK Marketing Courses 1991 - CERTIFICATE

  University of Wales (UK) MSc.(Transport Economics, Planning and Policy) 1984 1986 MASTERS DEGREE

  Chartered Institute of Transport (UK) B.A (Transport) 1982 - GRADUATE

  National Institute of Transport-Dar es Salaam Diploma in Transport Management 1979 - ADV DIPLOMA


  EMPLOYMENT HISTORY

  Tanzania Railways Co-operation(TRC) Deputy Head of Directorate of Trade and Markets 1992 2000

  Tanzania Railways Corporation Chief Costing & Pricing Manager 1986 -

  Tanzania Railways Corporation-TRC Principal Traffic Manager 1981 1983

  Tanzania Railways Corporation Traffic Manager 1978 1994

  East African Railways Corporation Traffic Officer 1971 1978
   
 3. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #3
  Apr 23, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Kuna mtu anaitwa Mbowe na mwingine anaitwa John Rubambe.

  John Rubambe alikuwa ndiyo sorta CEO wao kipindi cha Mkapa, ajamaa alitokea Bima, alikuwa classmate wa Mkapa.Nasikia alikuwa under great scrutiny -some would even say intimidation- kwa muda mrefu kabla ya kupewa hiyo kazi na Mkapa.Ilikuwa Mpaka simu yake ya nyumbani walimuwekea tap.By the way washua kibao hawako tayari kuongea ma issue mazito kwenye simu au email wanasema bongo kuna surveillance kichizi.

  So Rubambe, Mkapa pamoja na hawa viongozi wa mashirika ya umma wana a lot to answer.Wengine wanaweza kumtetea kuwa alikuwa anafanya alichoambiwa na Mkapa tu lakini still, angeweza kufanya bonge la expose kama angetaka.
   
 4. Rufiji

  Rufiji JF-Expert Member

  #4
  Apr 23, 2008
  Joined: Jun 18, 2006
  Messages: 1,628
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Pundit,

  Nakubalina na wewe kabisa viongozi wote wa tume hii kipindi cha Mkapa they have a lot to answer. Mimi ninachojiuliza ni kwa nini PSRC ilivurunda kila kitu ilichofanya ? Jee ni kwamba hawakuwa na wataalamu wa kutosha au ni kwa sababu hawakuweka maslahi ya taifa mbele ?

  Mimi nadhani kuna haja ya kufanywa investigation kubwa kuichunguza hii tume nini haswa ilifanya kipindi cha Mkapa.
   
 5. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #5
  Apr 24, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Mkuu waliohusika sana na hiyo kitu ya PSRC:-

  1. Mkapa, 2. Sumaye, 3. Idd Simba, 4. Kigoda, 5. Yona, 6. Masilingi, 7. Chenge, 8.Rubambe 9. Balozi Kazaura, 10. Mpungwe,

  Deal zote za hiyo kitu inahusisha hawa wakuu, in one way or another!
   
 6. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #6
  Apr 24, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,400
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  George Mbowe alikuwa nafikiri DG wa kwanza wakati PSRC ilipoanzishwa. Kama wengi mtakumbuka huyu alikuwa TDFL( I think) ambako alifukuzwa kazi na Nyerere pamoja na Augustine Mwingira na Lawrence Mmasi kwa zile scandal za Mawasiliano kuruhusu ATC kununua zile 707 za George Habash na Tacoshili kuuza meli kwa Lord Rajpar.

  Pundit,

  If there was such high level of survillance, how come both PSRC na TIC walituingiza mkenge? Don't you think you are adding more fuel to the talk of irresponsible TISS?
   
 7. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #7
  Apr 24, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Alikuwepo mwenyekiti George Mbowe wakati wa Mwinyi, na John Rubambe wakati wa Mkapa. Sasa hivi yupo Ali Karavina. Katika mahojiano fulani, George Mbowe aliwahi kusema yeye pia ndiye aliyepewa na Mwalimu Nyerere jukumu la kuratibu utaifishaji wakati Azimio la Arusha 1967. Watu wamekula nchi muda mrefu mwanawane!
   
 8. J

  JokaKuu Platinum Member

  #8
  Apr 24, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 11,291
  Likes Received: 1,892
  Trophy Points: 280
  Kithuku,Pundit,Rufiji,

  ..George Mbowe inasemekana alikuwa rafiki mkubwa wa Cygwiyemwisi John Malecela.

  ..Mbowe ni mwenyeji wa Mbeya sifahamu kabila lipi though.

  ..Mtendaji Mkuu wa PSRC analipwa na World Bank. kuna kipindi wabunge walilalamika kwanini alipwe mshahara wa zaidi ya USD 6000 kwa mwezi.

  ..Mkapa basically alimfukuza kazi Mbowe. uteuzi wa Rubambe ulifanywa kwa siri kubwa na hata waziri wa fedha aliusikia redioni.

  ..Kikwete naye alipoingia amkampatia ulaji swahiba wake Alli Karavina. Appointment ya Rubambe imefutwa kabla hata mkataba wake haujaisha.

  ..sijui tatizo la PSRC ni nini. chukulia mfano wa ubinafsishaji wa TRC ulivyoborongwa, despite the fact kwamba Karavina aliwahi kuwa Mkurugenzi huku TRC kabla ya kujiunga na siasa.
   
 9. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #9
  Apr 24, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  This is dated but relevant

   
 10. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #10
  Apr 24, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,400
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  It is true kuwa wabunge walilalamika sana. Lakini WB si ndio walikuja na kutuambia tuache kuendesha mashirika na hivyo mzigo wa kuundwa taasisi hii ukawa mabegani mwao?

  As far as I know PSRC is no longer functioning. Kazi yao ya mwisho ilikuwa ni mkataba wa Karamagi wa TICTS!
   
 11. Rufiji

  Rufiji JF-Expert Member

  #11
  Apr 24, 2008
  Joined: Jun 18, 2006
  Messages: 1,628
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Rev Kishoka,

  Ni kweli kwamba PSRC ai-function tena na ndio maana swali nililouliza lilukuwa katika wakati uliopita , " Nani walikuwa viongozi wa PSRC ? ". Lakini hata kama aifunction aituzuii sisi kuuliza maswali haswa pale tunapoona ya kuwa tume hii ilifanya makosa makubwa sana katika mikataba mingi.

  Jee ni nini haswa kilichowapelekea kuextend mkataba na Karamagi (TICTS) kwa miaka 25 huku wakijua wazi ya kuwa serikali imepoteza mabilioni ya shilingi pale Bandari, Jee yalikuwa kwa manufaa ya taifa au manufaa binafsi .

  Mimi nadhani ni muhimu kuichunguza hii tume kwani hawa watu wanajua vitu vingi na kama kweli tunataka kujua undani wa ufisadi basi hawa watu ni lazima wajibu maswali mazito.
   
Loading...