Nani wakutoa Ahadi, Watendaji au Wanasiasa?

Kasheshe

JF-Expert Member
Jun 29, 2007
4,694
787
Niliwahi kumsikia siku moja Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Joseph Sinde Warioba. Akisema hivi "Kwenye Taifa kama la Tanzania ambapo Mkuu wa nchi ni Rais wa Jamhuri, Waziri Mkuu kazi yake ni kuhakikisha Ahadi za Ilani na za Rais zinatekelezwa..." Akimaanisha kwamba si busara Waziri Mkuu naye kutoa ahadi zake... juu ya zile za Rais wa Jamhuri... maana kazi yake ni kutekeleza zile za Mkuu wa nchi...zaidi ya hapo atakuwa na mgongano wa kimawazo na maslahi ambapo atazipa umuhimu zile za kwake tu. wanasema kauli ya Rais ni Amri... hivyo lazima itekelezwe...kazi ya Waziri mkuu hivyo basi ni kutumia mfumo wa utawala alionao kutekeleza ilani na ahadi za Rais.... mfumo huo ni kama kutumia taasisi zilizo chini ya serikali na viongozi kama wakuu wa mikoa, wilaya, tarafa, kata na kijiji...

Kwa maana hiyo hiyo nashindwa kuelewa ninaposikia... na Mtendaji wa kijiji naye anatoa ahadi, Mkuu wa Wilaya, Mkuu wa Mkoa... Mhandisi wa Mkoa naye anatoa ahadi,,, mkurugenzi wa halmashauri naye anatoa ahadi...

Mimi nilidhani viongozi watendaji tuwaambie hatutaki ahadi kutoka kwao, wao wanapoongea na sisi waseme tu yaliyotekelezwa... na changamoto zake sio zaidi ya hapo... maana tukikubali kila mtu awe mtoa ahadi mwishowe tunaishiwa hakuna wa kutekeleza....

Mungu Ibariki Tanzania.
 
Kwa maana hiyo hiyo nashindwa kuelewa ninaposikia... na Mtendaji wa kijiji naye anatoa ahadi, Mkuu wa Wilaya, Mkuu wa Mkoa... Mhandisi wa Mkoa naye anatoa ahadi,,, mkurugenzi wa halmashauri naye anatoa ahadi...
Kuna baadhi ya Viongozi bado wapo kwenye maisha ya kipindi kile cha kofia mbili, ndio maana hujiasahau na kutoa ahadi...

Jukumu la kutoa ahadi lipo kwa wanasiasa, (Wabunge, Madiwani) kwani wao ndio watungaji wa sera...
 
Back
Top Bottom