Nani wa kwanza kujulishwa mtoto anapozaliwa??

haaa ackuambie mtu mami.....

kweli, l

akini ni kawaida, mwanmke amepewa na Mungu miundombinu yote ya kuhimile ile shughuli. na utafiti wa msuala ya saikolojia unaonyesha kuwa kila mwanamke anapojifungua anaboresha afya ya mwili na akili mara nyingi sana kuliko kula chakula bora kwa kipimo cha kawaida kwa miaka kumi mfululizo!!!

wajuzi wa mambo ansema kila mama akijifungua mwili wake hubadilika kwa kiasi kikubwa sana, kuanzia ndani ya mwili, kama nyonga na hata nje ya mwili kana kifua nk. haya yanahitaji mada inayojitegemea, lakini ndiyo afya yenyewe. tena usipozaa una hatari mara nyingi zaidi ya kupata maradhi kama saratani ya ziwa ama ya njia ya uzazi! uzazi ni afya!!!!!!!!!!!!

tusogope kuzaa na wala tusiwatishe wasichana wetu
 
Nafkiri uyo kwa kuwa ni mtoto wake wa kwanza labda alikuwa na furaha mpaka hakujua aanze kufanya nini zaidi akaona heri awambie rafki zake kwanza kwa kuwa mumewe yupo around anaweza kuwa anajua ameshajulishwa na madoct! Pamoja na hayo inatakiwa akiri kosa sababu kwa lolote mumewe angetakiwa kumkumbuka first. Ajiulize ingekuwa ni mumewe kapandishwa cheo kazini alafu anze kuwambia mabest zake first alafu yeye atumiwe msg na mmoja wa mabest wa mumewe kuwa mumeo kapandishwa cheo bwana,, angejisikiaje!!?
 
nimewahi kusuluhisha ugonvi uliotishia ndoa ya mtu mmoja.

mkewe alipojifungua mtoto wao wa kwanza aliwaambia kwanza rafiki zake (mashosti au mashoga zake) wote na mmoja wao ndiye aliyemwambia kwa msg mume kuwa kapata mtoto na jinsia ya mtoto. mume akiwa haamini kam mkewe anaweza kujifungua bila kumjulisha alianza kwa kubisha na baadaye alipolkwenda kumtazama alipokuwa amepumzishwa alimkuta kweli mkewe kajifungua na alipokagua simu yake alijiridhisha kuwa amejifungua zaidi ya masaa mawili yaliyopita na muda wote huo tayari alikuwa kishawajulisha mashosti wake wote bila kumkumbuka mumewe, mume alidai mkewe kamdhalilisha sana na hampendi tena,

kwa mujibu wa maelezo yao hawakuwa na ugomvi wowote na wakati wote mama alipokuwa kwenye chumba cha kujifungulia mume alikuwa nje katika maeneo ya hospitali anahangaika huko na huko kuweka mambo sawa mama amaliza shughuli salama.

mnaonaje waungwana, nani anapaswa kuwa wa kwanza kujulishwa?
Mkuu nimechelewa mada lakini inakuwaje mtu hujui due date ya mkeo hadi usimuliwe??

Mimi naamini one of the most binding action kwa mwanaume ni kuwa na mkewe zile saa za kujifungua, si lazima aingie chumbani kuona uzazi wenyewe (au operesheni) lakini ni muhimu awe karibu na mkewe na ikiwezekana awe wa kwanz kupokea mtoto

Mwanamke ana kosa lake la kutomwambia mwezi wake, lakini katika hali ile sijui alipitiwaje (labda kuna namna) na mwanaume tatizo lake ni kutokua karibu na mkewe kwenye muda ule

Cha maana hapo ni kujirudi wote wawili tu
 
huachelewa mkuu

karibu hoja zote ulizotoa nilishazifafanua vizuri, lakuni kwa kifupi, mume alikuwa zero distance muda wote isipokuwa tu hakuruhusiwa kuingia labor na alibaki pale pale hospitali muda wote kuhakikisha shughuli inisha vizuri

mama alitumia simu yake kujuisha mashosti zake, hivyo utaona alipokagua simu aliamini kuwa alitumia watu wengi sana lakini bila kukumbuka kuwa mume yupo nje ya labor na anaweweseka kwa maombi mkewe atoke salama

mke anapuuza malaalamiko ya mumewe na anadai mumewe analalamikia mambo madogomadogo hadi anataka kuvunja ndoa yao, anasisitiza kuwa kimamntiki mume kuwa wa ngapi kuambiwa kwake sio ishu, anawza kumfanya mtu yoyote awe wa kwanza kujua kadiri aonavyo kuwa vyema

kama utafuatilia vizuri mtililiko mzima wa hii hoja utaona majibu mengi mkuu
 
Mkuu, kwa maelezo haya its definite kwamba jamaa hayuko peke yake katika kupanda dice hapo shambani

The good news is kuna DNA test, akafanye tu!!!
 
Nafkiri uyo kwa kuwa ni mtoto wake wa kwanza labda alikuwa na furaha mpaka hakujua aanze kufanya nini zaidi akaona heri awambie rafki zake kwanza kwa kuwa mumewe yupo around anaweza kuwa anajua ameshajulishwa na madoct! Pamoja na hayo inatakiwa akiri kosa sababu kwa lolote mumewe angetakiwa kumkumbuka first. Ajiulize ingekuwa ni mumewe kapandishwa cheo kazini alafu anze kuwambia mabest zake first alafu yeye atumiwe msg na mmoja wa mabest wa mumewe kuwa mumeo kapandishwa cheo bwana,, angejisikiaje!!?[/QUOTE]

mfano mzuri mkuu,

kuna aina fulani ya maumivu waakati mwingine mtu hatayajua hadi yamfike,

kweli katika mazungumzo yetu, mwanaume alikiri kuwa baada ya kufanyiwa hivi kuna mambo mengi amefanya bila kumwambia mkewe kutokana na mapenzi kupungua, mfano alikiri kununua viwanja vitatu bila mkewe kujua, alimwmambia baada ya kuanza kulima kimoawapo! na hadi wanakuja kwangu kuna kimoja bado hajapata muda wa kumpeleka akione!!! na mwanamke kusikia hivi nae alianza kulalamika kuwa mumewe anamdharau!!!!!!!

busara muhim sana ndani ya ndoa
 
Huyo dada anaakiwa naye akapimwe akili.haiwezekani kumfanyia mwenzake haya wakati alikuwepo eneo la hosp.Hata kama angelikuwa nje ya nchi angetafuta tu jinsi ya kumjulisha.hii ni dharau kabisa hata kama wana matatizo yao kwenye ndoa hapo alitakiwa aaweke tofauti zake pembeni hawa mashosti hawamsaidii kitu zaidi ya kubomoa.
 
Jamaa mwema..
Na alivo na kiburi..Waislam wana bahati pande hizo
Fasta mwenzie
 
Jamaa mwema..
Na alivo na kiburi..Waislam wana bahati pande hizo
Fasta mwenzie

hahhahhaaaaaaaaaaaaa
lakini mwenzie sio dawa ya kiburi mzee! sana sana kama ana wivu ndio umeweka petroli kwenye moto nyumbani
 
Mke yuko kwenye show ya ndoa? Au hajakua kuwa mke anajali ushosti akimchunguza zaidi atapata bp sababu hana heshima labda na mapenzi kivileeeee.

Na instagram, facebook, whatsapp groups, snapchat, etc hizo zinakimbiza kujionyeshea na wengi kutothamini ndoa....pole yake

Mmh anachepuka au na hampendi mumewe.
 
Experience yangu inaniambia wanawake wanawachukiaga sana waume zao soon baada ya kujifungua! Wanahisi uchungu waluoupata wakati wakujifungua umesababishwa na waume zao, so hakuna la kushangaa baba mtoto kutokupewa taarifa
 
Ewe Mwenyezi Mungu tunaomba huruma yako, shetani kashika fahamu zetu tunashindwa kutofautisha Jema na Baya kama mama huyu anaeshindwa kutambua nani ni muhimu katika ndoa yake Amen.
 
hongera kwa kumpa mwenzio nafasi anayostahili,

kweli ukishuhudia shughuli ilivyo (mimi nimeshuhudia mara kadhaa kwa watu tofauti), utawaheshimu sana akina mama. siku nyingine nitaleta kisa kinachohusu "baba kushuhudia shughuli ya kujifungua"

katiak maisha yangu nimebahatika kushauri kwa mafanikio mambo mengi sana juu ya ndoa na nitaendelea kuwaletea kisa kimoja baada ya kingine, lengo langu tujirekebishe panapotakiwa ili kujenga ndoa imara na zenye furaha.

.....mimi nimeshuhudia mara kadhaa kwa watu tofauti....dini inakuruhusu kuwa na kadhaa?!
 
Back
Top Bottom