Nani wa kwanza kujulishwa mtoto anapozaliwa?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nani wa kwanza kujulishwa mtoto anapozaliwa??

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mbunge wa CCM, Dec 11, 2009.

 1. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #1
  Dec 11, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nimewahi kusuluhisha ugonvi uliotishia ndoa ya mtu mmoja.

  mkewe alipojifungua mtoto wao wa kwanza aliwaambia kwanza rafiki zake (mashosti au mashoga zake) wote na mmoja wao ndiye aliyemwambia kwa msg mume kuwa kapata mtoto na jinsia ya mtoto. mume akiwa haamini kam mkewe anaweza kujifungua bila kumjulisha alianza kwa kubisha na baadaye alipolkwenda kumtazama alipokuwa amepumzishwa alimkuta kweli mkewe kajifungua na alipokagua simu yake alijiridhisha kuwa amejifungua zaidi ya masaa mawili yaliyopita na muda wote huo tayari alikuwa kishawajulisha mashosti wake wote bila kumkumbuka mumewe, mume alidai mkewe kamdhalilisha sana na hampendi tena,

  kwa mujibu wa maelezo yao hawakuwa na ugomvi wowote na wakati wote mama alipokuwa kwenye chumba cha kujifungulia mume alikuwa nje katika maeneo ya hospitali anahangaika huko na huko kuweka mambo sawa mama amaliza shughuli salama.

  mnaonaje waungwana, nani anapaswa kuwa wa kwanza kujulishwa?
   
 2. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #2
  Dec 11, 2009
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Mhh
   
 3. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #3
  Dec 11, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mbona unashangaa tu? hayo ndio mambo yaliyomo ndani ya ndoa, leta ushauri wako tuwasaidie wenzetu
   
 4. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #4
  Dec 11, 2009
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Pole yake baba watoto ila mie nikijifungua napenda sna mzazi mwenzangu awepo pembeni yangu, hihih ihiihi ila mama kafanya makosa jamni sio vizuri!
   
 5. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #5
  Dec 11, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ndio maana siku zote nasisitiz matatizo mengi ndani ya ndoa yanaweza kuzuilika. cha ajabu mama nae alikuwa akibeza hasira na malalamiko ya baba muda wote wa usuluhishi, kuwa anfuatilia vitu vidogovidogo, hali iliyofanya usuluhishi uwe mgumu zaidi.
   
 6. Serendipity

  Serendipity JF-Expert Member

  #6
  Dec 12, 2009
  Joined: Jan 24, 2009
  Messages: 475
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Labda huyo mumewe hakuwa 'biological' father wa huyo mtoto akiyezaliwa, na ndio maana hakuona umuhimu wa wa kumtaarifu mapema!
   
 7. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #7
  Dec 12, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hapana mkuu. katka mashauriano yet na hata ukimtazama mtoto, yule ndiye baba halisi wa mtoto, hata mama alithibitisha hilo bila wasiwasi.
  mama yeye alidai kwa kwake jambo la nani kuwa wa kwanza au wa mwisho halina uzito anaweza kumchagua yoyote awe wa kwanza kuambiwa kadiri aonavyo kuwa vyema, na alimshutumu vikali mumewe kuwa ameleta ugomvi kwenye ndoa yao changa kwa sababu zisizo na msingi!
   
 8. Mvina

  Mvina JF-Expert Member

  #8
  Dec 12, 2009
  Joined: Aug 2, 2009
  Messages: 1,000
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Of course Lazima unijulishe kwanza mimi,vinginevyo hapatakalika hapa home!
   
 9. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #9
  Dec 12, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  huyo dada ni mgonjwa, hivi kweli mmewe yupo nnje ya hospital na ndie aliyempeleka alafu mtoto anazaliwa yeye (mumewe) anapewa taharifa na watu wa nje?
   
 10. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #10
  Dec 12, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  katika mashauriano yetu, ilifikia hatua mkanda uliorekodiwa kitchen party ya yule dada uliletwa ili nijiridhishe ni nini alifundishwa katika ile kitchen party.

  baada ya kuucheza mkanda mzima, nilijiridhisha kuwa kulisemwa mara nyingi sana kuwa katika mambo yote wa kwanza kuulishwa ni baba siku zote.

  lakini huyu mama alisisitiza mara zote kuwa kwake nani wa kwanza kujulishwa si suala la msingi! anaamua kdiri aonavyo kuwa vyema na katika kesi ile aliona vyema kuwajulisha rafiki zake kwanza!

  Mungu mkubwa tulifanikiwa kuepusha talaka pale lakini mwanmume hampendi tena kwa dhati kama mwanzo!!
   
 11. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #11
  Dec 12, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,373
  Likes Received: 3,135
  Trophy Points: 280
  aaahhhhhhhhh...........jamani
   
 12. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #12
  Dec 12, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mapenzi katika ndoa hii yamepungua sana kuliko ilivyokuwa mwanzo kwa sababu ya tendo moja dogo la mama na kubwa zaidi kugoma kwake kuomba msamaha.

  ni kwa rehema za Mungu tu bado ndoa hii ipo hadi leo. muhimu tupate fundisho kwetu na kwa watoto wetu ili ndoa zetu ziwe mahali pa furaha kwa wote.
   
 13. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #13
  Dec 12, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  mie nilivyomaliza tu ile safari mtu wa kwanza kumjulisha alikuwa ni mr, na bahati nzuri alikuwa around tu, baby wa pili alimshuhudia na kushika adabu yake.
   
 14. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #14
  Dec 12, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  eeh!
   
 15. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #15
  Dec 12, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  ndio hivyo baby boy, alizidisha huruma! hakuamini kama ningetoka salama pale.
   
 16. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #16
  Dec 12, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hongera kwa kumpa mwenzio nafasi anayostahili,

  kweli ukishuhudia shughuli ilivyo (mimi nimeshuhudia mara kadhaa kwa watu tofauti), utawaheshimu sana akina mama. siku nyingine nitaleta kisa kinachohusu "baba kushuhudia shughuli ya kujifungua"

  katiak maisha yangu nimebahatika kushauri kwa mafanikio mambo mengi sana juu ya ndoa na nitaendelea kuwaletea kisa kimoja baada ya kingine, lengo langu tujirekebishe panapotakiwa ili kujenga ndoa imara na zenye furaha.
   
 17. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #17
  Dec 12, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  hayo yalikwa ni maoni yake mapema mno, tukakubaliana, cha kushangaza kafika ndani anaziba uso/ ameshtuka kuona hali halic inavyokuwa na hakutegemea kwamba namtolea watoto mbali kiac hicho....ilimchukua muda kusahau.
   
 18. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #18
  Dec 12, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  AAH!aaah!
   
 19. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #19
  Dec 12, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  wewe leo ishia kushangaa tu....
   
 20. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #20
  Dec 12, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kuna tatizo la watu kudhani kuwa kutofahamu jambo fulani kuna maana kuwa jambo hilo halipo.

  ni kweli watooto wanatoka "mbali" lakini bado ni jambo la kawaida kwa sababu Mungu aliwapa wanawake "miundombinu" yote inayotakiwa kuwaleta watoto duniani, japo kwa uchungu mwingu.

  utafitu umeonyesha kuwa uchungu waupatao akina mama unawasaidia kupunguza "uchungu" usababishwao na msukumo wa mtoto kwenye njia ya uzazi wakati wa mtoto kujitokeza nje ya nyumba yake. siku moja nitalifafanua vizuri hili. muhimu tujue ni kawaida.

  mwanamke sawa na mwanume kila mmoja apewe nafasianayostahili
   
Loading...